Spika Ndugai ongoza Bunge Kwa kanuni Na Sheria Sio Kazi yako kuvichagulia vyama Wagombea

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Katika mahojiano Na kituo kimoja cha Televisheni Spika Ndugai amesikika akikilaumu CHADEMA eti kwanini kimewateua wagombea kutoka Mwanza Na kwanini kisiteue kutoka sehemu nyingie hata Zanzibar.Kauli ya Spika inazidi kuthibitisha Chuki yake na wabunge wa CCM dhidi ya wagombea wa CHADEMA.

Spika Ndugai Kazi yako ni kusimamia kanuni na sheria zilizowekwa Kwa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki si vinginevyo .CHADEMA hizo nafasi ni zao Kwa mujibu wa Sheria Na sio hisani Na huna uwezo wa kuzipokonya. Viache Vyama vitafute wagombea wao wanaoona wanafaa.
 
Tatizo ajamaliza dozi yake huyo ndugai ndo maana yan sometime anajitoa ufaham kama ajielew vile...
Nadhan amalize dozi kwanza ndo aje kuliongoza bunge
 
Kwani tuna Bunge au Idara ya ule mhimili uliojichimbia chini zaidi?!
 
Kwa hili lililotokea bungeni la kupigiwa kura chache masha na wenje inaonekana kuna haja ya kubadili kanuni za kuwapata wabunge wa afrika mashariki. Napendekeza vyama viwe na maamuzi ya mwisho ya kuchagua wabunge wao wa east Africa, na wabunge hao watakuja bungeni dodoma kuhojiwa ufahamu wao na malengo yao ya kuomba nafasi hizo lakini si kupigiwa kura. Nasema hivi kwasababu wabunge wa upinzani na chama tawala hawana hawaivi chungu kimoja, na tusitegemee kama wanaweza kupigiana kura ili mmojawao ashinde. Hii ngumu kutokea. Vyama ndio viwe na maamuzi ya mwisho kuchagua wabunge wao.
 
mtia-nia-jpg.492241
 
Euphransia: Nilimsikiliza sana Spika Ndugai kwenye hayo mahojiano. Spika amesikika akihoji yafuatayo:
1. Kwa nini Chadema ilete wagombea wote kutoka Nyamagana? Ina maana sehemu nyingine hakuna watu?
2. Kwa nini Chadema imeleta wakristo tu? Ina maana wa dini nyingine kama waislamu hawapo?
3. Kwa nini Chadema imeleta wa kutoka Tanzania bara tu? kwani Zanzibar hawako?
4. Kwa nini Chadema imeleta wanaume tu? Ina maana Chama hakina wanawake?

Kwangu mimi haya mambo anayohoji Ndugai ni hatari sana kwa Taifa. Tukianza kuchaguana kwa misingi ya huyu Ndugai tutalipasua Taifa. Tunapochagua wawakilishi wetu wa ndani na nje ya nchi tuangalie uwezo au ubora wa mtu na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom