Spika Ndugai: Jerry Silaa lazima aombe radhi kwa umma

Spika Ndugai: Jerry Silaa lazima aombe radhi kwa umma

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
1630408257597.png

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Jerry Silaa lazima aombe radhi kwa umma kwa kosa alilofanya

Jerry Silaa ambaye ni mbunge wa Ukonga alikutwa na hatia ya kuongea uongo kuhusu mishahara ya wabunge kutokatwa kodi

Kamati ya Maadili ya Bunge ilipendekeza asihudhurie mikutano miwili ya bunge na avuliwe ujumbe wa Bunge la Afrika(PAP)
 
wametoa mapovu hatr ingekuw na kweny maslah ya wananchi wanawaka ivo tungekuw dona kantry
 
Aombe radhi kwa umma kivipi, wakati umma hawajamtuhumu kwa lolote, malizaneni wenyewe msianze kuingiza umma kwenye swala ambalo haliwahusu.
 
Huyo Jelly siyo mpumbavu aseme hakatwi wakati anakatwa. Mnajaribu kuficha tu ili kutudanganya wananchi. Kuleni, mlishapewa wala msiigope. Hata kama hamlipi hatuna pakuwapelema
 
Huyo Jelly siyo mpumbavu aseme hakatwi wakati anakatwa. Mnajaribu kuficha tu ili kutudanganya wananchi. Kuleni, mlishapewa wala msiigope. Hata kama hamlipi hatuna pakuwapelema
Halafu Slaa ni mtu makini Sana siamini alitamka kitu asichokijua.
 
Hawa wapumbavu wameshaishiwa pumzi,tatizo Mbadala wao wananchi hawauoni
Mbadala wa kwanza ni John Heche kuwa waziri wa mambo ya ndani,John Mrema kuwa waziri wa mambo ya Nje, John Mnyika waziri Mkuu,Zitto waziri wa fedha na raisi Mbowe kwani Lissu hatapata watu wa kumsaidia kufanya kazi kwani yeye kasoma saana na watanzania hawana elimu ya kuweza kufanya kazi na yeye,,,oop Fatma Karume atakuwa waziri wa sheria na katiba
 
Na akiomba radhi watanzania tutamwona mjinga,akitala heshima bora akomae nao tu ikiwezekana aitishe press kuelezea anachokisimamia
 
Mwisho wa kuwalaghai wananchi ni sasa. Hizo posho wanazolipana zote ni kwa ajili ya kazi za Kibunge. Wakati umefika ziunganishwe kwenye mshahara wa jumla wa Mbunge ijulikane kwa mwezi wanalipana shilngi ngapi tulinganishe na mishara na posho za watumishi wengine uraiani wenye hadhi eqivalent na wabunge mfamo majaji, mahakimu wafawidhi , Maprofesa, Wahadhiri waandamizi nk.

Pia tujue mishahara na posho za madereva na makarani wa bunge tulinganishe na walimu wanaopigwa vumbi la chaki kila uchao au hawa polisi walio uwawa juzi kwa kusikitisha na Hamza sheikh Mohamadi.
 
Back
Top Bottom