Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,034
- 1,003
Spika Job Ndugai na naibu Tulia kwa kweli jinsi mnavyoliendesha Bunge mnalifanya liwe kituko na sio mhimili uliohuru tena. Bunge limekuwa haliisimamii serikali. Bali serikali imekuwa ikilisimamia bunge. Ni kweli bunge ni la chama kimoja ila tuangalie maslahi mapana ya taifa. Bunge limekosa utamu kabisa. CAG alisema bunge dhaifu hakukosea amesema iliyo kweli kabisa; ila kwakuwa hamtaki kuambiwa kweli mnampeleka kumhukumu kwenye hiyo kamati iliyokosa weredi na uhuru. Watanzania tuamke, tupo hatarini hili bunge sio kabisa vinginevyo uwe mnafiki ama huipendi nchi yako.