[/SIZE]
Nami nashangaa kama kweli hili ni jambo la kujadili. Sheria inakitaja chama na siyo muungano wa vyama. Hata kama hao wengine wataungana, hiyo haitatambulika. Tunataka chama chenye viti vingi bungeni. FINITO.
Kanuni za kudumu za Bunge, toleo la 2007:
14.-(1) Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atachaguliwa
chini ya utaratibu ulioainishwa kwenye fasili za Kanuni hii
zinazofuata.
(2) Wabunge wote wa Upinzani wanaweza kuunda Kambi Rasmi
ya Upinzani iwapo idadi yao itakuwa si chini ya asilimia kumi na
mbili na nusu ya Wabunge wote.
(3)
Chama cha Upinzani hakitakuwa na haki ya kuchagua
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, isipokuwa tu kama kina idadi ya
Wabunge wasiopungua asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge
wote.
(4)
Endapo kutakuwa na Vyama vya Upinzani zaidi ya kimoja
ambavyo kila kimoja kina Wabunge asilimia kumi na mbili na nusu
au zaidi, basi Chama chenye idadi kubwa zaidi ya Wabunge kuliko
vingine ndicho kitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, lakini, ikiwa kutakuwa na vyama viwili
au zaidi vyenye idadi sawa ya Wabunge ambao ni zaidi ya asilimia
kumi na mbili na nusu, Wabunge wa vyama vinavyohusika
watachagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni chini ya utaratibu
watakaokubaliana wenyewe.
Sitaki kuamini kuwa Spika mpya anabisha kuwa CHADEMA hawastahili kuwa official opposition.
Kama anabisha kuhusu kiongozi wa upinzani hilo nalo ni kosa la wazi,
Siku moja makosa mawili, mwaka mmoja siku 365, miaka mitano siku 1865, siku 1865 Makosa 3650. Tutafika kweli???
Mbombo ngafu.