Spika Makinda, historia itakuhukumu.

Spika Makinda, historia itakuhukumu.

mantegi

Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
27
Reaction score
20
Wanajf, tunapoanza mwaka nimeona nizungumzie mwenendo wa bunge letu tukufu yaani bunge la kumi chini ya spika Anna Makinda [Bi Kiroboto]
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010, wengi tulitarajia bunge la kumi lingekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa letu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wapinzani bungeni ambao wangeweza kukosoa serikali tofauti na wabunge wa ccm ambao siku zote ni kupitisha hata kama hoja haina tija kwa taifa eti wanaitetea serikali ya chama chao.
Napenda kuwapongeza wabunge wa upinzani kwani wamejitahidi kufanya kile wengi walitarajia na vilevile niwashauri wabunge wa ccm kujihoji kwanza kabla ya kutetea hoja kwani hoja zingine hazitetei maslahi ya chama wala taifa bali hutetea maslahi ya watu binafsi hasahasa mafisadi.
Wanajf, juhudi za wabunge wa upinzani zinazimwa na spika wa bunge kwa kukataa hoja zenye maslahi kwa taifa kujadiliwa bungeni. Hoja nyeti zilizokataliwa ni kama vile ajali za meli zilizotokea ndani ya taifa letu, mgomo wa madaktari, mgomo wa walimu, kuteswa kwa dokta ulimboka, hoja ya waziri mkuu kulidanganya bunge, hoja ya rushwa bungeni na hoja ya katiba mpya ambayo baadae iliwaumbua.
Kama hizi hoja zingejadiliwa bungeni bila shaka tungepiga hatua mbele kwani hoja hizi zilikuwa za msingi kabisa na zingine bado zinatusumbua hadi leo mfano mgomo wa walimu.
Nasikia anafanya haya eti kwa sababu ametangaza kuwa hatagombea tena ubunge lakini nimshauri kwamba familia ya mwl Nyerere inaheshimika kutokana na uongozi wa Baba wa taifa. Napenda tutambue kuwa Anna Makinda ni janga la taifa kwani ameonekana kukandamiza hoja ambazo zingeleta tija kwa taifa letu. Naomba kuwasilisha.
 
Huyu mama ni tatizo kubwa sana, nina wasiwasi na uwezo wa ubongo wake, kwa sababu hata anapopinga jambo anapinga ili apinge,hana analolijua ni maimuna
 
Mama hatuliii, anasafiri utafikiri ni mtendaji, mpaka anasahau kuwa sio kila mwaliko wa spika anakitawa aende yeye, sometimes anatakiwa amwachie naibu.....uspika ni taasisi sio mtu.... jimboni siku hizi hakanyagi inachukuwa miezi mingi tu ndio anaenda huko tena kwa siku chache. mama tulia kidogo azimia hivyo mwaka huu, inawezekana
 
Ameshatangaza kuwa hagombei tena,anakusanya kila cent inayokatiza mbele yake!ili astaafu vizuri!
 
Back
Top Bottom