Spika makinda hatimae aumbuka,ajikosha

Chenge alimaanisha nini alipo sema kuwa anasikitika sana bunge lililopita halikuwa linaruhusu wala kuchukua mawazo mazuri ya wapinzani kama ilivyo sasa.
Hii inamaana anampiga madongo Samweli Sita au vipi?

Chenge ama kweli mnafiki. Mwenyewe naye alikuwa waziri wakati huo, sana yeye mbona alikuwa haungi hoja za wapinzali wakati huo?
 
Unafiki wa magamba unaweza kuwa tija kwa wanaojali na kuipenda nchi. huo ni mwanzomengine mbele kwa mbele
 
Wajuzi wa lugha wanisaidie maana halisi ya neno NDUMILAKUWILI nisije nikalitumia vibaya hapo baadae.
 
Nafuatilia bunge,baada ya Kamanda Lissu kumaliza hotuba ya kambi rasmi juu ya marekebisho ya rasimu ya katiba bi mkubwa akasimama akasema 'huo ndo ukweli wenyewe na hao ndo wakweli tuwaunge mkono' kwa hili laonekana hawa jamaa wa magamba wameshinikizwa kuujadili hawana jinsi,namsubiria tena leo Mama Kilango aliyeshadadia mwaka jana na kuiponda chadema je atasemaje.CDM 4EVA

Ndo ubaya wa wabunge wa CCM na CCM B wanafikiri kwa kutumia matumbo
 
Chenge alimaanisha nini alipo sema kuwa anasikitika sana bunge lililopita halikuwa linaruhusu wala kuchukua mawazo mazuri ya wapinzani kama ilivyo sasa.
Hii inamaana anampiga madongo Samweli Sita au vipi?
Ndugu usipoteze bure muda wa kutafakari kauli za kina Chenge,huyo Chenge yupo hapo kimaslahi zaidi yupo tayari wakati wote kumpaka mafuta Sita,nafikiri kisa unakijua,huo ndio ubinafsi wa Chenge,hasemii hilo swala kwa nia njema yeye ana mtazamo wake ni sawa na unapumona mamba akitoa machozi akikukosa sio kuwa anakuhurumia NO bali ni ugwadu wa kukukosa/

Viongozi wa Tanzania visasi haviwaishi mpaka kaburini
 
aibu yao wenyewe! kumbe wanapokuwa wanashangilia upumbavu wanakuwa wanajua kabisa ni upumbavu ila hawana jinsi tu. Kweli Tanzania nakupenda
 
Ndo ubaya wa wabunge wa CCM na CCM B wanafikiri kwa kutumia matumbo

Mbona unawapendelea hivyo. Anayewajua vizuri ni Meya Masaburi wewe nenda kamuulize atakueleza wanatumia kiungo gani kufikiri.
 
Mkuu kweli maskini akipata hujisifia. Mapendekezo yaliyochukuliwa ni asilimia 5 tu ya yote, rais bado ana madaraka makubwa na katika ikiisha bunge la katiba analiteua yeye, hapo huoni hay a marekebisho ni kiini macho? Tafakari kabla ya kuandika

Hata mimi bado siamini kama kweli haya mabadiliko ni ya dhati na yanalenga kupata mchakato huru utakaoleta katiba ya wananchi. Siamini pia kuwa mara hii CCM wamebadilika ghafla na sasa wanataka KUANDIKA Katiba mpya badala ya KUHUISHA Katiba iliyopo. Lazima kuna kitu wameweka humo kwenye mapendekezo yao ya mabadiliko ya sheria ambacho kinafifisha (neutralize) mantiki ya mabadiliko yote waliyopendekeza CDM.
 
Mkuu kweli maskini akipata hujisifia. Mapendekezo yaliyochukuliwa ni asilimia 5 tu ya yote, rais bado ana madaraka makubwa na katika ikiisha bunge la katiba analiteua yeye, hapo huoni hay a marekebisho ni kiini macho? Tafakari kabla ya kuandika

LunaticBrain
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom