Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,948
- 709
Kwa wale waliofuatilia mjadala wa leo asubuhi bungeni, bila shaka wataungana nami kusema spika hakutenda haki ktk uamuzi alioutoa.
Kilichotokea ni kwamba mh. Ngeleja alitoa maneno ya kuudhi au kejeli alipokuwa akichangia na alitamka kwa kejeli kwa kuifananisha bajeti mbadala ya kambi ya upinzani na bajeti ya maandalizi ya harusi.Baada ya matamshi hayo na katika hali ya kushangaza mh.spika alimuacha aendelee kuchangia bila kumkatisha kwa maana ya kumtaka afute kauli yake kitu ambacho hakikuwa sahihi.Cha ajabu ni pale mh.Mdee aliposimama na kutoa taarifa kusahihisha upotoshaji wa Ngeleja na yeye bila shaka kwa kutaka kulipiza kisasi akaamua kumkejeli Ngeleja kwa kusema inaonekana Ngeleja ana uchungu wa kukosa uwaziri.Ghafla spika baada ya kauli hiyo ya mh Mdee akasimama na kumtaka afute kauli yake hiyo akidai kuwa kama hiyo ndio hoja bora asiendele kuchangia.Baada ya kauli hiyo ya mh spika, mh Mdee alikubali kufuta maneno yake.Sasa huu kama sio upendeleo au kutokutenda haki tusemeje?Mbona mh.Ngeleja alipotamka kuwa bajeti ya upinzani ni kama bajeti ya maandalizi ya harusi hakumtaka afute kauli yake!
Kwa kifupi spika,naibu wake na wenyeviti wa bunge hawatendi haki na kamwe wasitarajie kuwa bunge litakuwa na nidhamu kama mambo yataachwa yaendelee kama yalivyo.
Simamieni haki na usawa kwanza kabla ya kudai nidhamu ya wabunge mnaowaongoza.Vinginenyo ipo siku ngumi zitaibuka humo bungeni.
Kwa wenzetu CCM harusi inaandaliwa kwa mabilioni ya fedha labda ndiyo maana Spika aliamua kuwa biased kwa Ngereja. Umesahau vijisenti?