Spika Job Ndugai ataja sifa za mbunge kutibiwa nje ya nchi

Hata kama ni uteam ila Team Lumumba mmetisha kwa uongo. Mmeumbuka! Spika kapigiwa na balozi wa Ujerumani kamjulisha personally kabisa kwamba huyu jamaa anagharamikiwa na Ujeruman, japo haizuii kupambania haki zake za kimatibabu kutoka kwa Bunge. Sasa ikawaje team [HASHTAG]#LumumbaBaby[/HASHTAG] mkasema katelekezwa kibrazani, analala sebuleni huko Ubelgiji?

Jamani matango pori yanalika, ila bila chumvi kwakweli ni kuuawana. Ni kama Nandy, saivi nyimbo zake naona ni kelele, hata kwenye simu yangu naziona ni mzigo, maana kwa kuvujisha utupu alidhani ndio kiki kumbe watanzania wa sasa sio wa miaka hiyo. Hata ukiangalia Hollywood, trend iliyopo sasahivi ni Mahakama, watu wanafukuzana na mahakama tuuu…mara kakamatwa, kesho anaripoti, mara jela miezi 3 n.k.. Trend za utupu hata nashangaa Diamond aliingiaje kingi.

Anyway, team Lumumba mmeshindaJ
 
Mh Job Ndugai naomba nikuseme leo,katika kitu ambacho umekosea kimkakati ni udhaifu uliouonyesha katika kujibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini.

Kwa swala la Mh.Tundu Lissu halikuwa alikiitaji mwalimu,kwani hile ilikuwa daharula ofisi yako ilitakiwa iingilie kati bila kusubiri kibali cha Muhimbili wala Katibu Mkuu,au kibali cha Rais.
Wewe unataka kuona ni swala la kawaida Risasi 38.
Naona ntu mzima ukivuliwa nguo chutama.
Umenikumbusha wale wahalifu wawili waliosulibiwa pamoja na Yesu....... Mmoja alimdhihaki Yesu ilhali wote wako katika mateso yanayofanana!
 
Mungu ni mwingi wa huruma na neema. Hubatilisha nia mbaya na huinua zilizo njema. Bila kujali uchama au ubaguzi wa aina yoyote, Ndungai na wenzake wameonyesha nia mbaya sana katika suala zima la matibabu ya Lissu.
 
Kwa hiyo Ujerumani siku hizi imegeuka kitengo cha bima ya afya ya bunge la Tanzania!?
 
Tunashukuru Mungu kuwapa maelekeo kina Mh. Mbowe na wanafamilia kwamba Lissu asije Muhimbili hosp, vinginevyo tungekuwa tumeshamsahau siku nyingi.

Mungu wa Yakob, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Eliya -huwa anasimama kwenye upande wa mwenye haki. Lissu yupo upande wa haki; aliyemponya atamsimamia.
 
Nimesikiliza kwa juu juu jana ufafanuzi wa spika wa bunge la Tanzania akijibu mwongozo wa mh. Lema (mb). Nijuavyo mimi, ufuataji wa taratibu za matibabu za rufaa si tu hutegemea aina ya ugonjwa umsumbuao mtu BALI hali ya mgonjwa kwa ugonjwa huo. Ni rahisi sana na ni utaratibu wa kawaida pale mtu anapohisi kuumwa kwenda hospitali na kwamba kabla mgonjwa huyo hajapewa rufaa ya kwenda hospitali ya ngazi nyingine, madaktari wa ngazi husika hutathmini ugonjwa na uwezo wa kitabibu na vifaa tiba vya hospitalini hapo kama vinakidhi kutibu tatizo la kiafya alilonalo mgonjwa na kama wanaweza kuokoa maisha ya mgonjwa husika kwa ngazi hiyo.

Kwa hiyo, kwa magonjwa ya kawaida yanayoibuka mwilini, mhanga atapaswa kufuata taratibu zote za kitabibu zilizoainishwa kabla ya kwenda hospitali ya ngazi ya juu kwa matibabu zaidi. Lakini utaratibu huo hauwezi kuhusika kwa asilimia zote kwa matukio ya dharura kama vile ajali (Majanga mbalimbali) lakini pia kuugua ghafla magonjwa ya ajabu.

Tumeshuhudia matukio mengi ya dharura ambayo yalipelekea wahanga kupewa rufaa za moja kwa moja bila kwanza kufuata taratibu lengo likiwa ni kunusuru maisha yao. Tumeshuhudia wahanga wa ajali za barabarani na hata anga kupewa rufaa za haraka kwenye hospitali kubwa ili kuwahikikishia uzima wao. Hata kama matakwa ya taratibu za rufaa yalikuwa ni muhimu kihivyo bado mgonjwa angeweza kupelekwa hospitali husika kwa msaada zaidi wakati taratibu za kitabibu za rufaa zinafanyiwa kazi, lengo likiwa ni kuokoa maisha ya mgonjwa au mhanga.

Nadhani si sahihi kuyapa uzito sawa matukio yote ya kiafya ambayo kwayo maisha ya mhanga yanaweza kuwa shakani. Tukio la ajali haliwezi kupewa uzito sawa na ugonjwa wa kawaida usiyohitaji udharura; kwa maana tukio la ajali linaweza kupelekea kifo kwa mhanga ikiwa hatapatiwa huduma haraka katika weledi na vifaa tiba takiwa.

Tukio la kumininiwa risasi kama mvua lililomkumba Binadamu mwenzetu, Mtanzania mwenzetu, Mtoto wetu, mwakilishi wetu, mtaalam wetu wa sheria, mwanaharakati wetu Mh. Tundu Antipas Lisu (Mb) lilikuwa ni tukio baya kuwahi kutokea katika nchi yetu. Lilikuwa ni tukio la kuua (Deadly Event), ni tukio la dharura sawa na matukio ya ajali hatari. Ilihitaji hatua zozote na maamuzi yoyote yanayochukuliwa, yatazamwe katika udharura pia pasi hivyo uchelewevu wowote katika maamuzi na bila uwepo wa Mungu Mkuu, tungempoteza Mh. Tundu Lisu. Asante Mungu kwa kuwa ulijua nia za wauaji na washirika wao katika kutekeleza mpango wao ovu na hivyo kuwaibua watu ambao walipata ujasiri mkuu kufanya maamuzi magumu ya kunusuru hatari ya kifo iliyokuwa imedhihiri kwa mtanzania mwenzetu!

Ukubwa na udharura wa tukio lile ndio unaonifanya sasa nione kuwa Mh. Spika ambaye naye husumbuliwa na maradhi yasiokuwa ya dharura amekosea kutoa maelezo yenye msimamo juu ya sababu ya bunge kushindwa kugharamia matibabu ya Lisu (mb). Pengine kama ni kwasababu ya kuumwa umwa mh. spika kayumba kidogo kama sivyo basi spika ajitathmini. Taratibu za rufaa haziwezi kuwa muhimu kuliko maisha ya binadamu.

Nadhani mh. spika angejibu kwa namna nyingine lakini kwa majibu aliyoyatoa hayakidhi matakwa ya kwanini bunge halijamhudumia mhanga na hayajengi taswira nzuri ya mamlaka za bunge na serikali.

Wadau huo ni mtazamo wangu, I stand to be challenged and corrected!
 
Kazi Ndugu Hai anasumbuliwa na Gitaa la Dali kimoko na minjingu anayoiamini ni ya India
 
Lissu amesema Mungu akimjalia kurudi salama atalipelka bunge na serikali mahakamani na atajiwakilisha mwenyewe
 
Vibali vibali! Cha bunge, cha muhimbili, na cha Rais. Asingeweza kuvipata vyote bila kwanza kufa.

Nafikiri hili jambo lipo wazi sana kwa sasa. Haiihitaji akili nyingi kujua nini kilitakiwa kutokea. Kuna mchangiaji aliwahi kusema hili la matibabu halikutegemewa....halikupangwa. Je, ni kweli kazi ilipaswa kuishia eneo la tukio?
 
Vibali vibali! Cha bunge, cha muhimbili, na cha Rais. Asingeweza kuvipata vyote bila kwanza kufa.

Nafikiri hili jambo lipo wazi sana kwa sasa. Haiihitaji akili nyingi kujua nini kilitakiwa kutokea. Kuna mchangiaji aliwahi kusema hili la matibabu halikutegemewa....halikupangwa. Je, ni kweli kazi ilipaswa kuishia eneo la tukio?
Mungu atawalipa kwa kazi walioifanya!
 
Back
Top Bottom