PostGE2025 SPika: 'Baba Levo' sio jina lako anza upya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wakati Mbunge mteule wa Jimbo la Kigoma Mjini, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama “Baba Levo,” akila kiapo cha uaminifu Bungeni, amejikuta akirudia kiapo hicho baada ya Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu, kukataa kutumia jina la utani “Baba Levo” kwa kuwa si jina lake rasmi.

Tukio hilo limejiri leo, tarehe 11 Novemba 2025, wakati wa hafla ya uapisho wa wabunge wateule iliyofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

Pia Soma: Baba Levo ajitambulisha Bungeni, atamba, "niliangusha Mbuyu"
Your browser is not able to display this video.
 
Tuacheni utani hii nchi hatuko serious aisee... Just imagine Baba Revo anatutungia sheria na kutupangia bajeti... Ningekua na uwezo ningeondoka niende hata nikaishi hata Eswatini niwaachieni nchi yenu maana huku ni kukwamishana kabisa.
 
Tuacheni utani hii nchi hatuko serious aisee... Just imagine Baba Revo anatutungia sheria na kutupangia bajeti... Ningekua na uwezo ningeondoka niende hata nikaishi hata Eswatini niwaachieni nchi yenu maana huku ni kukwamishana kabisa.
9/12 usiondoke Wana kuhitaji
 
Baba levo ndo anaenda kutunga sheria bungeni ambazo profesa wa tz anatakiwa kufuata. Kuna mda ccm embu jaribuni kuona kuwa hii ni nchi.
Mkuu haya mambo ukiyafikiria kiundani unatajikuta uko barabarani kabla hata hiyo Dec 9..... Huu upumbavu unaumiza sana iwapo kama una akili timamu kichwani..
 
Tutaishia kufa tu. Uwezi kuitoa ccm kwa maandamano. mzigo unatakiwa kupigwa usiku kwa usiku tena kushtukiza. Asubuhi kila mtu yupo kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…