Spika Anne Makinda Bunge limemshinda kuongoza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Anne Makinda Bunge limemshinda kuongoza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Jul 26, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Baada ya Uchaguzi mkuu wa 2010,Chama cha Mapinduzi-CCM kiliamua kwa maksudi kufanya mageuzi kwenye uongozi wa Bunge la JMT kwa kumwondoa aliyekuwa Spika kwa wakti huo Mhe.Samwel Sitta aliyekuwa akijitanabahisha kama Spika wa Viwango na Kasi(Standard and Speed) hivyo kulifanya jina lake lisomeke kwa herufi 5 za 'S' au penta S (Speaker of Standard and Speed Sammy Sitta- SSSSS).

  Ni ukweli usiopingika kuwa Mhe. Samwel Sitta aliliendesha Bunge la Tanzania kwa viwango vya kimataifa na kasi ya ajabu.Kila Mtanzania ni shuhuda wa mambo makubwa,muhimu na yenye mwelekeo wa kulijenga Taifa letu kwa uadilifu mkubwa yalifanywa na Mhe.Sitta. Bunge likawa Bunge lenye mvuto,ushawishi na hamasa ya kusikilizwa na kutazamwa na kila Mtanzania. Baada ya Uchaguzi mkuu wa 2010 ilionekana kwamba kulikuwa na hujuma ya kumwengua Mhe. Sitta kwa maksudi kutokana na sababu ambazo zilikuwa wazi kabisa kwamba Spika Sitta alikuwa akiruhusu Wabunge wa Upinzani na upande wa Chama Tawala ndani ya Bunge kuikosoa serikali kwa waziwazi kiasi cha kuipelekea serikali kuweweseka na kupoteza mwelekeo!Wengi watakumbuka sekeseke la Richmond jinsi Spika Sitta alivyolisimamia kwa kuunda tume ya Bunge iliyopelekea kujiuzulu kwa PM Edward Lowasa na hivyo kuvunja Baraza la Mawaziri!

  Jambo hili halikuwafurahisha Watawala wengi ndani ya Serikali na hasa Mafisadi na majeruhiwa wa Richmond hivyo kusuka mipango na mikakati ya kumng'oa SSSSS. Kwa kutumia ujanja na hila za hali ya juu kuliwekwa kigezo cha Spika wa 2010 awe MWANAMKE kigezo ambacho Sitta asingeweza kukipata kwani yeye si mwanamke. CCM walijua walichokuwa wanakifanya na mwisho wa siku tulishuhudia mwanamke Anne Semamba Makinda akichukua kiti cha Spika!

  Mimi nilikuwa mmoja wa watu waliokosoa sana kwa Anne Makinda kupewa kiti hichi na nikasema kuwa huyu mwanamke asingeweza kuhimili vishindo vya Bunge la sasa la Tanzania lenye Wabunge mchanganyiko kwa maana ya vyama vingi(Tawala na Upinzani) na lenye Wabunge wengi Vijana,Wasomi na Weledi wa maswala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Sasa tumeingia mwaka wa pili baada ya Uchaguzi wa 2010 na tayari imedhihirika kuwa Heshima na Ubora wa Bunge la Tanzania inazidi kuporomoka siku hadi siku!

  Tatizo ni Spika Anne Semamba Makinda ambaye ame-prove failure kuliongoza na kulisimamia Bunge letu. Mama Makinda anaonekana kuyumba katika kila hatua ya bunge hili kuanzia kwenye Kanuni,Sheria na taratibu za Bunge kwa ujumla wake. Tunachoshuhudia sasa ni marumbano kati ya Spika,Naibu wa Spika,Wenyeviti na Wabunge hasa wa kambi ya Upinzani. Anne Makinda,Job Ndugai na wenyeviti wao wameonyesha ushabiki wa wazi kabisa wa kutetea serikali ya CCM hata pale ambapo Kanuni,Sheria na Taratibu za Bunge zinapokanyagwa maksudi ili kuiokoa Serikali kutokana na kibano toka Upinzani na wabunge mmoja mmoja toka ndani ya Chama Tawala-CCM. Tumeshuhudia hoja za msingi kabisa toka kwa Wapinzani zenye mwelekeo wa kulijenga Taifa letu zikizuiliwa na Spika,Wenyeviti na Wabunge wa CCM kwa hoja,taarifa na zomezomea!

  Ili kurudisha nidhamu ya Bunge la Tanzania itahitaji Spika mwingine wa aina ya Sammy Sitta-SSSSS ambaye sijui atapatikana lini! Hakuna siri tena kuwa mama Anne Semamba Makinda kazi ya Uspika wa Bunge imemshinda na anatakiwa ajiuzulu au apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye maana kazi imemshinda.

  Nawasilisha.
   
 2. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya yote watz wanayaona na ilimradi watz wa leo sio wale basi acha tuendelee kukusanya uchafu unaofanywa na ccm....tutawahukumu kwa maneno na matendo yao 2015 sio mbali
   
 3. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Asa79

  Tuko pamoja mheshimiwa. Kama ulivyoweka bayana hukumu ya CCM ni 2015 ili kuondoa uoza huu unaoisumbua nchi yetu.
  Tuombe kila Mtanzania anayeitakia mema nchi hii alione hilo na achukue hatua mwaka 2015 ajaliapo Mwenyezi Mungu ingawa wao CCM wanadai kuwa watatawala Tanzania milele! Mbunge wa CHADEMA Mhe. Msigwa aliwauliza CCM Bungeni hivi juzi kuwa,''Kwamba CCM wanataka watawale milele na hali hii tuliyonayo watanzania,SO WHAT??"

   
Loading...