Spika Aikataa Ripoti ya Jairo, Wabunge Wamgomea Waziri. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Aikataa Ripoti ya Jairo, Wabunge Wamgomea Waziri.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Matola, Apr 23, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD] Spika aitupa ripoti ya Jairo
  • Wabunge wamgomea waziri

  na Tamali Vullu, Dodoma


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema hajaridishwa na majibu ya serikali kuhusu taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kamati ya Bunge kuhusu sakata la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, hivyo kuirudisha serikalini.
  Spika Makinda alitoa kauli hiyo jana, baada ya Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse, kutaka mwongozo wa Spika katika suala hilo kutojadiliwa huku mkutano wa Bunge ukiwa unaahirishwa.
  “Mheshimiwa Spika naomba kupata mwongozo wako katika order paper inaonekana Bunge linaahirishwa leo, lakini hakuna taarifa ya serikali kuhusu utekekezaji wa maazimio ya kamati ya Bunge kuhusu suala la Jairo na mpaka sasa hatujaambiwa chochote,” alisema.
  Akijibu Spika Makinda alisema, “Tulikuwa tuweke katika mkutano huu, lakini mimi nimeyakataa majibu kwa kuwa sijaridhishwa, hivyo nimerudisha serikalini,” alisema Spika.
  Jairo, alisimamishwa kazi kutokana na sakata la kuzichangisha fedha taasisi zilizokuwa chini ya wizara hiyo kwa lengo la kufanikisha kupitisha bajeti bungeni.
  Kutokana na hali hiyo, Bunge liliunda Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani, kuchunguza uhalali wa utaratibu wa wizara hiyo kuchangisha fedha hizo na kubaini kasoro kadhaa kabla ya kutoa mapendekezo yake.
  Kamati hiyo iliundwa baada ya kuibuka mvutano baina ya mihimili miwili ya dola, Bunge na Serikali baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kutangaza hadharani kumrejesha kazini Jairo aliyekuwa amesimamishwa kazi kwa tuhuma hizo zilizotolewa bungeni dhidi yake.
  Hata hivyo, siku chache baada ya wabunge kuja juu kupinga uamuzi huo wa Luhanjo, Ikulu ilitangaza rasmi kushughulikia tuhuma za rushwa zinazomkabili Jairo, baada ya Rais kumpa likizo yenye malipo na alipofanya uteuzi wa makatibu wakuu alimwacha pembeni na nafasi hiyo akampa Eliakimu Maswi.
  Wakati huohuo, Spika wa Bunge alisema leo wabunge wamelazimika kujadili kamati ya mipango baada ya kuahirishwa kwa Bunge kutokana na kubanwa na kanuni ya 94.
  Alisema kutokana na hali hiyo, kuna haja ya kuiangalia upya kanuni hiyo, hivyo mjadala wa kamati hiyo utafanyika katika ukumbi wa Msekwa.
  “Kanuni ya 94 imekuwa na ugumu katika utekelezaji, hivyo kamati ya uongozi imeamua mjadala wa mpango wa maendeleo ya taifa kwa mwaka 20012/2013 ufanyike kesho (leo) katika ukumbi wa Msekwa, ili Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na maofisa wengine waweze kushiriki katika mjadala huo na kutoa majibu kwa hoja zitakazoibuliwa na wabunge,” alisema.
  Wabunge wamgomea waziri
  Katika hatua nyingine wabunge wawili wote wa Chama cha Mapinduzi wamegomea majibu ya mawaziri waliyoyatoa jana katika kipindi cha maswali na majibu, wakisema yamejaa ubabaishaji mkubwa.
  Wabunge hao ni Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi (CCM), ambaye alikataa majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Filipo Mulugo, kuhusu ujenzi wa vyuo vya ufundi.
  Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua ahadi ya serikali ya kujenga Chuo cha Ufundi VETA katika wilaya ya Mbozi tangu mwaka 2008 lakini ahadi hiyo imeshindwa kutekelezwa hadi sasa.
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo alisema kuwa dhamira ya serikali ni kujenga chuo cha ufundi stadi kila wilaya lakini kutokana na ukubwa wa mahitaji na uhaba wa fedha, serikali inajenga vyuo hivyo kwa awamu.
  Naibu Waziri alisema wilaya hiyo iko katika orodha ya wilaya 28 zitakazojengewa vyuo vya ufundi katika awamu ya kwanza na akashauri katika kipindi ambacho serikali inatafuta fedha, ni vema wananchi wa wilaya hiyo kupata mahitaji katika chuo cha ufundi stadi Mbeya.
  Majibu hayo yalimkera Zambi ambaye alisimama na kudai kuwa hoja ya waziri haikuwa na faida yoyote kwa wananchi wa jimbo lake.
  Naye Mbunge wa Nkenge Assumpter Mshama (CCM), alisema kuwa majibu yanayotolewa na mawaziri mara nyingi hatoi matumaini kwa wananchi.
  Mshama alitoa hoja hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza kwa kuitaka serikali ni kwa nini isiweze kuweka ruzuku kwa ajili ya kununua dawa ya ugonjwa wa migomba.
  Mshama alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa migomba ni kwa nini serikali isitoe ruzuku kwa wakulima kwa ajili ya kununua dawa za ugonjwa kutokana na dawa aina ya jiki kuuzwa kwa bei ya shilingi 6000 kwa lita.
  Aidha aliihoji serikali ina mpango gani kuhusu kuwapeleka wataalamu wa kilimo kwenda nchini Uganda kwa ajili ya kujifunza jinsi ya kumenya ndizi na kuzihifandhi kwa ajili ya kuzisafirisha nchi za nje.
  Akijibu maswali hayo Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Magembe, alisema kuwa serikali inatambua kuwa gharama ya kununua dawa ya migomba aina ya Jiki ni kubwa lakini hakuna ruzuku kama alivyoshauri mbunge.
  Alisema kuwa kwa sasa kinachoweza kusaidia katika kupambana na ugonjwa wa migomba ni wakulima kuhakikisha wanatumia vifaa ambavyo vimekuwa katika hali ya maelekezo ambayo wakulima wanatakiwa kufuata, majibu yaliyomkera mbunge huyo wa Nkenge.


  [​IMG]


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Na game likaishia hapo hahahhahahahahaaaaaa wabunge wa ccm bana???! kama maigizo fulani vile......
   
 3. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Viazi na nzi mbovu hizo
   
Loading...