Spika adai Kuchafuliwa Kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika adai Kuchafuliwa Kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitia, Apr 9, 2008.

 1. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2008
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huku ndio naita kujibu hoja kwa hoja...

  Sitta orders expenditure report in bid to clear his name

  2008-04-09 09:42:56
  By Judica Tarimo, Dodoma

  Speaker of the National Assembly Samuel Sitta yesterday instructed the office of the Clerk to the National Assembly to prepare his official expenditure since he assumed office in the wake of allegations of abuse of office and financial embezzlement levelled against him.

  ``I have already directed the Parliamentary Office to prepare a comprehensive and printed report showing my official expenditure including allowances since I was sworn in as Speaker,`` said Sitta at the end of the question-and-answer session yesterday morning.

  Sitta`s clarification has been triggered by accusations posted on the Internet and other sources, linking him to abuse of office and embezzlement of funds in allowances, salary and other emoluments.

  Some sections of the local media were recently quoted as saying that the Speaker had set up an environment that guaranteed him huge allowances and payments out of official trips and other official duties.

  It is understood that unknown individuals circulating these reports had gone to the extent of sending insulting text messages to Sitta`s children, belittling and tarnishing his reputation as Speaker of the National Assembly, one of the crucial state pillars.

  In what could be seen as an attempt to clean up his name, the Speaker said in the National Assembly yesterday: \"I am ready to face these people who are seeking to spoil my reputation before the eyes of the public.

  I have already instructed the Parliamentary Office to prepare my official expenditure including allowances and other official payments since I assumed office.

  * SOURCE: Guardian
   
 2. Pope

  Pope Senior Member

  #2
  Apr 9, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Spika wa Bunge la Jamhuri Mh Samuel Sitta amedai kuchafuliwa jina kisiasa na kudai kuwa kwa sasa amejidhatiti kukabiliana na watu hao.

  "Ninalo ombi moja kwa hawa ndugu zangu, waache kuichafua familia yangu, kama kuna mtu aliyewaudhi ni mimi, na ninao uwezo wa kujibu mashambulizi, nimejiimarisha vya kutosha, ” aliendelea kutamba.

  Alisema katika kuweka sawa kumbukumbu za malipo ya posho zake tangu ashike wadhifa huo, amemwagiza Katibu wa Bunge, aandae taarifa ya malipo yake yote ambayo itatolewa kwa wabunge wote.

  Spika, alisema masuala mengine ya kijamii ambayo amekuwa akichafuliwa, hayawezi kujibiwa na Katibu wa Bunge.

  “Nimemwambia katibu wa bunge aandae taarifa ya malipo ya posho zangu tangu nimeanza, ili kuonyesha pia utaratibu wa posho,” alisisitiza.

  Kumekuwa na malalamiko ya kupakana matoke baina ya makundi hasa baada ya kuachia madaraka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mh Edward Lowasa kwani kuna kundi ndani ya Chama ambalo lilikuwa lina msupport Lowasa na jingine lilikuwa likimuuma kichinichini.

  Mtazamo wangu.
  Inaonyesha kutatokea mpasuko mkubwa wa Kisiasa ndani ya Chama siku za mbeleni na wallah kama wasipokaa vizuri ndio kwaheri.
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo wazee wetu hawa hawajisafishi kwanza kabla ya kuanza kusafisha nchi. Matokeo yake wanajiweka vulnerable kwa maadui zao kuwafanyia siasa chafu na hivyo kuathiri mapambano wanayoyaongoza na mustkabali mzima wa nchi yetu...

  Vijana wa leo tuna mengi ya kusoma hapa. Haya tunayojidanganya ni masuala binafsi huishia pale unapoamua kujiingiza katika utumishi/uongozi wa umma. Siasa za nchi zinabadilika, yaliyokuwa ya kawaida kwa wazee wetu si ya kawaida tena. Huko tuendako ndio kabisa...

  Tanzanianjema
   
 4. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Spika atangaza mapambano dhidi ya wanaomchafua kwa siasa chafu

  Written by Ramadhan Semtawa, Dodoma
  Wednesday, 09 April 2008
  CHECHE za mkutano wa 11 wa Bunge zimeanza kujitokeza, kufuatia Spika, Samwel Sitta kuvunja ukimya kwa kujibu mapigo dhidi ya wanaomchafua na kuwapiga vijembe kuwa, wanacheza siasa za kiwango cha chini.

  Kauli hiyo ya Sitta imekuja wakati kukiwa na taarifa ambazo zinadaiwa kulenga kumpaka matope hasa tangu kumalizika mkutano wa 10 wa Bunge, ambao ulishuhudia maamuzi mazito ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Edward Lowassa, kutoka nafasi ya Uwaziri Mkuu baada ya kuhusishwa na kashfa ya mkataba wa Richmond .

  Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu, Sitta alitamba kuwa, amejiimarisha vya kutosha kupambana na watu hao.

  Spika huyo ambaye alionekana kuwapiga ‘dongo’ baadhi ya wanaodaiwa kumchafua, alisema ataendelea kulifanya Bunge kuwa na maamuzi sahihi kwa mujibu wa kanuni, bila hofu.

  “Nashukuru sana ndugu zangu ambao wamekuwa wakinipa pole kutokana na yote yanayonikuta, kuchafuliwa na watu ambao wanacheza siasa za kiwango cha chini cha majitaka,” alisema Sitta, huku ukumbi ukiwa umetulia.

  Aliwataka watu hao kuacha kuchafua familia yake wakiwemo watoto, kwani kama kuna mtu aliyewaudhi ni yeye na si familia yake.

  Alifafanua kwamba, binti yake ambaye aliolewa hivi karibuni, alichafuliwa kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu ambao umejaa maneno machafu.

  "Ninalo ombi moja kwa hawa ndugu zangu, waache kuichafua familia yangu, kama kuna mtu aliyewaudhi ni mimi, na ninao uwezo wa kujibu mashambulizi, nimejiimarisha vya kutosha, ” aliendelea kutamba.

  Alisema katika kuweka sawa kumbukumbu za malipo ya posho zake tangu ashike wadhifa huo, amemwagiza Katibu wa Bunge, aandae taarifa ya malipo yake yote ambayo itatolewa kwa wabunge wote.

  Spika, alisema masuala mengine ya kijamii ambayo amekuwa akichafuliwa, hayawezi kujibiwa na Katibu wa Bunge.

  “Nimemwambia katibu wa bunge aandae taarifa ya malipo ya posho zangu tangu nimeanza, ili kuonyesha pia utaratibu wa posho,” alisisitiza.

  Tangu kumalizika mkutano wa 10 wa Bunge, kumekuwa na harakati mbalimbali zinazodaiwa kueleza mabaya ya Spika, ambayo ni pamoja na kwamba amekuwa akitumia mbinu ikiwa ni pamoja kujiingizia posho.

  Awali katika matangazo yake, Spika alieleza kutiwa saini kwa miswada mitatu ya sheria ambayo ilipitishwa na Bunge.

  Spika alifafanua kwamba, miswada hiyo ambayo ilipitishwa na Bunge na Rais kuitia saini ni pamoja na ya Maambukizi ya Ukimwi, Sheria ya Utalii na Sheria ya Uendeshaji Mashitaka, yote ya mwaka 2008.
   
 5. Pope

  Pope Senior Member

  #5
  Apr 9, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado wanamtandao wananguvu!!
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Apr 9, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..kwanini Spika asiandae hiyo taarifa ya malipo yeye mwenyewe?
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Spika aje clean aseme kila linalo pigiwa kelele atoe maelezo kwa uwazi then aacha tuamue cha kufanya aache vitisho hapa na hadithi za visungura .
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pamoja na dawa za milioni mbili kwa wiki.
   
 9. Pope

  Pope Senior Member

  #9
  Apr 9, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine unaweza kudhani unajisafisha kumbe ndio unajipaka kinyesi maana kwenye kujibu shutuma usipokuwa na busara za ziada utabaki kupayuka unawapa watu cha kusema!!
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mtanzania ndiyo maana nasema aje clean na ahalalishe risiti zake za 2m kwa wiki na kuumwa ni mguu ambao hakuwahi kukosa Bungeni ama kulazwa kisa mguu .Vimada na hata maeneo wanayo kaa pia aje na maelezo ya kina .
   
 11. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #11
  Apr 9, 2008
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Sasa kusema utajibu hoja ndo inakuwa umejibu?
  Mbona mafisadi walisema wmesha instruct wanasheria wao wafungue kesi?hivi zilifunguliwa?

  Hao aliowinstruct wanareport kwa nani? kwani sio kwake?maana huwezi kutoa instuction kwa mtu ambaye haripoti kwako.Kwani kuna mbunge liyemuuliza swali kuhusu hili? au ndo ukigongwa na nyoka hata unyasi unakshtua.6 kumbuka mwosha huoshwa.Hivi siku hizi wabunge ndo wamekuwa auditors wa expenditure za spika? jibu hoja ndo tuzichambue.ila mpaka sas a hamna hoja iliyojibiwa ila kulialia tu kwa Mhe.Spika.
   
 12. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #12
  Apr 9, 2008
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mods,
  nadhani hii iunganishwe na thread ya spika adai anachafuliwa kisiasa iliyoanzishwa na Lunyungu
   
 13. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sasa kama katibu wa bunge ndiye atatoa hiyo taarifa ya matumizi ya spika,sisi tuta reconsaili wapi,hapa ana kwepa kikaango ili kesha haje na hadithi nyingine.Spika wewe ndio tunaomba hesabu yako na sio katibu wa bunge,kula ule wewe kisha ujifanye ujui.
   
 14. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwani Mr Six alikuwa haujui mtandao?asilalamike amuulize Salim A. Salim mtandao ulimfanya nini kwenye kinyang'anyiro cha urais.Moja ya sera za mtandao ni kuchauana sasa joka limekuwa kubwa linaanza lumeza watoto wake heheheheh tutasikia mengi mwaka huu...
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Sokomoko fafanua kauli yako .Six anasoma sana hapa ili apate ujumbe kikamilifu
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Bora angetupa hesabu yake na Katibu wa Bunge atupe ya kwake ili tu odit .
   
 17. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Yaani ni hivii yeye Mr Six yupo mtandao matumaini sasa wale mtandao Maslahi ni watu wakupakana matope kwahiyo sio kweli kama hajui kundi lake lililomweka alipo hajui moja ya objectives zake ni kuchafuana. Sasa Mr Six kwa ushauri wa bure usife peke yako kwani wewe hujui skendo zao? Mr Six ni senior member humu JF tupostie mavituzzz tuone uozo wao ukilalama haisaidii you have to fight back mzee.
   
Loading...