Spika aagiza kuondolewa maneno katika hotuba ya upinzani kuhusu Wizara ya Ulinzi

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa mara nyingine ameelekeza kuondolewa kwa baadhi ya aya za hotuba ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kwa maelezo kuwa yamekiuka kanuni za uendeshaji wa Bunge.

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameamuru baadhi ya maneno yaondolewe kwenye hotuba ya kambi hiyo kuhusu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/18.

Amesema maneno hayo yanahatarisha usalama yakitumiwa vibaya na maadui wa Taifa.

Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Mwita Waitara amesema kuwa kisu cha ngariba kimepitia kwa hiyo hatasoma

Chanzo: Mwananchi
 
pic+spika+aamuru.jpg

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameamuru baadhi ya maneno yaondolewe kwenye hotuba ya kambi hiyo kuhusu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/18.

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa mara nyingine ameelekeza kuondolewa kwa baadhi ya aya za hotuba ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kwa maelezo kuwa yamekiuka kanuni za uendeshaji wa Bunge.

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameamuru baadhi ya maneno yaondolewe kwenye hotuba ya kambi hiyo kuhusu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/18.

Amesema maneno hayo yanahatarisha usalama yakitumiwa vibaya na maadui wa Taifa.

Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Mwita Waitara amesema kuwa kisu cha ngariba kimepitia kwa hiyo hatasoma.
 
CCM bado wako kwenye zama za mawe, ukiizuia hotuba ya kambi ya upinzani ni sawa na kuzuia BOMU kwa Tumbo, hotuba tayali imeshasambaa na watu wanayo, tuone Kama itakuwa hatali kwa usalama wa nchi,
 
Hao ndio huwa wanazuia mambo yasijadiliwe mfano ishu ya mauaji ila kila siku vifo vinaongezeka!
Cc jenista mhagama
 
Badala ya kupambana na magaidi wanaoua raia wasio na hatia kule Rufiji, wao wanapambana na maandishi yaliyomo kwenye hotuba kwamba yanahatarisha usalama wa nchi!!!
 
Mkuu kama inawezekana iweke hapa.
CCM bado wako kwenye zama za mawe, ukiizuia hotuba ya kambi ya upinzani ni sawa na kuzuia BOMU kwa Tumbo, hotuba tayali imeshasambaa na watu wanayo, tuone Kama itakuwa hatali kwa usalama wa nchi,
 
CCM NCHI ILIPO FIKA AYA MAMBO AMUWEZI KUZUIA,SOMENI ALAMA ZA NYAKATI
NISAWA NA KUZUIA HARUFU YA MAITI KWA PAFYUM
 
Duh hali mbaya. Sasa kama hatuna wa kutusemea itakuwaje? Maana sasa pension ya Brigadeire gen. ni sawa na mtumishi mwenye diploma ya afya yaani Clinical Officer. Wakati hadhi zao ni tofauti, shida ni kuwa huku kwetu tumejaziwa posho lakini mshahara ni kiduchu sasa unapofikia kusitaafu unaambulia kidogo then unarudi kulinda mbao.
 
Unapotakiwa kuzima moto unaufunika na KARATASI ati hakuna moto,utakapopamba moto tutataka kuuzima
 
Back
Top Bottom