Special Thread; Mahitaji ya visa na lolote kuhusu maswali yahusuyo nchi za nje......

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
19,166
37,177
Habari za wakati huu wandugu na jamaa.....

Nimepitia nyuzi mbali mbali zinazohusu waTanzania wanaoishi huko nje.....nimegundua kuwa Watanzania wengi wana muamko mkubwa wa kusafiri na kwenda nje....iwe kwa kusoma au kutafuta maisha....

Lakini kama mnavyojua kuwa hili ni jambo geni kwenye jamii yetu kwa hiyo siyo wengi wenye kujua taratibu na habari zinazohusu kusafiri kwenda nje ya nchi.....kwa kuwa kila nchi ina taratibu zake na sheria zake kwa yeyote atakaye kwenda huko.....

Nimeweka thread hii ili wale wote wanaoishi au waliowahi kufika sehemu mbali mbali za dunia hii....wajumuike nasi hapa na kutupa uzoefu wao na kuwapa habari mbali mbali wale walio na nia ya kufika huko kwa nia moja au nyingine......
Ingawa kuna mitandao husika inayoelezea kinaga ubaga taratibu hizo...lakini hapa tutazipata za live kutoka kwa wahusika.....

NB; Mimi sijawahi kusafiri popote nje ya nchi hii.....kwa hiyo sifahamu lolote kuhusu mambo ya nje huko nje ya Tanzania.....
 
Mimi nataka kujua kama tunahitaji transit VISA through Italy anayejua atujuze please.Kuna hii website ya www.kiwi.com naomba kufahamu iwapo it can be trusted.

Asanteni
 
Back
Top Bottom