Special kwa wadada

Special kwa wadada

Kama nyumban kwenu huwez fanya kaz usitegemee ukwen utaweza.. Jamani shughuli za nyumban ni kipaji inabidi mtu uanze kukipenda toka uko kwa bibi mkubwa wako
Malkia waambie wenzio ng 'ombe hanenepi siku ya mnada hata ukimpa mashudu.
 
kupika ni kipaji kama ilivyo music😀😀😀

ndio maana wengine wanafundishwa,ila bado wakipika ,wanapika madudu.😀🙄
 
SPECIAL KWA WADADA

Umepata Bwana, Umempenda Kweli kweli na Umemlalamikia Sana Eti Kwanini Hakupeleki Kwa Wazazi Wake Kukutambulisha, Jamaa Akagoma Sana mwishowe akaona isiwe Kesi Akakupeleka

Wewe badala hata utake hiyo advantage umefika tu Siku ya Kwanza Umeshinda Unachati, Siku ya Pili Umeshinda Unachati Tena ndio unajisifia kwenye groups upo ukweni Kumbe Wao Wanakutazama Tu na kukupimia Wala Hawakwambii Kitu

Siku ya Tatu Wanakwambia Leo Ni Zamu Yako Kupika, Unaingia Jikoni unaona Kila Kitu Kigeni
Vya Huku Unaweka Kule, Vya kule Unaweka Huku (Yaani Hujui Kupika Chochote)

Sufuria Unashika Kama Umeshika Power Bank, Unapika Na Lipstick, Mdomo Mwekunduuu Utafikiri Mtoto wa Jini Katoka Kufundishwa Kunyonya Damu tena huku Umevaa Saa, Umevaa Culture Zimejaa Nusu Ya Mkono, Umevaa Mini Skirt Kama Wafanyakazi Wa Emirates

Msosi wa Wakwe Huwezi Kupika. Ukiambiwa Hufai Kuolewa Unavuta Mdomo Utafikiri Umenyimwa USB Cable Ubust Smartphone Yako
Unaanza Kulalamika Wakwe Hawakupendi, Unalalamika Weee, Unashindwa Kuelewa Kuwa Wewe Ndo Tatizo.

Usitake Kuolewa Ukidhani Mumeo Atakula Chips na Wewe Utakuwa Utakula Pizza Kila Siku, Jifunze Hata Kuchemsha Chai Basi Au Unadhani Google Wataleta App Ambayo Unaweka USB Kwenye Simu Yako Alafu Unaielekezea Kwenye Sahani Inaproduce Msosi

[HASHTAG]#JIPANGE[/HASHTAG] DADA Usidhani Ndoa Ni Kama Kupiga selfie
Ilishatokea kwa shangazi yangu tumekutana ukoo mzma akapewa kazi ya kukata kachumbeliilikua kama vipande vya nanasi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom