South Africa yapinga bidhaa za Israel

ELFU-ONEIR

Senior Member
Jun 27, 2012
181
64
Nchi ya afrika kusini imepinga hatua ya bidhaa zinazotoka israel zisiandikwe "made in israel" wanataka ziandikwe "made in makazi ya walowezi wa kiyahudi" hii inamaanisha nini?

Source" habari za mitaa: Africa kusini yapinga bidhaa zilizo andikwa israel
 

Attachments

  • ISRAEL.jpg
    ISRAEL.jpg
    13.1 KB · Views: 432
safi sana!israel na usa wauaji wakubwa!hata tanzania tumekataa ubalozi wao.
 
Africa Kusini inaanzisha mgogoro na taifa teule la Mungu? Ona sasa wameanza kuuwana, huu ni mwanzo wa laana kwao. Mfano halisi ni tanzania, taifa lenye rasilimali nyingi zisizowanufaisha wananchi wake, hii ilitokana na laana kama hiyo.
 
Africa Kusini inaanzisha mgogoro na taifa teule la Mungu? Ona sasa wameanza kuuwana, huu ni mwanzo wa laana kwao. Mfano halisi ni tanzania, taifa lenye rasilimali nyingi zisizowanufaisha wananchi wake, hii ilitokana na laana kama hiyo.

Hivi hiyo Afrika Kusini, Mungu alimpa nani amsaidie kazi ya kuisimamia ? maana Mungu kachagua taifa moja tu kuwa lake !
 
ni kweli hakuna ubalozi wa israel tz?
Ni kweli hatuna uhusiano wa kibalozi na Israel. na nchi zote zisizo na uhusiano na Israel, zina laana. Hii ndiyo maana pamoja na kuwa na rasilimali nyingi, bado laana ile ile inatung'ang'ania. Hatutaepuka laana hii mpaka tuwe na uhusiano na taifa teule la Mungu.
 
Ni kweli hatuna uhusianio wa kibalozi na Israel. na nchi zote zisizo na uhusiano na Israel, zina laana. Hii ndiyo maana pamoja na kuwa na rasilimali nyingi, bado laana ile ile inatung'ang'ania. Hatutaepuka laana hii mpaka tuwe na uhusiano na taifa teule la Mungu.
Hivi haya mataifa mengine kama Tanzania baada kususwa na Mungu, tunamtegemea nani ? halafu taifa teule mbona Mungu amelipa kashamba kadoogo ka kugomeana na wenziwe ? huyu Mungu yuko rational kweli ?
 
Hivi haya mataifa mengine kama Tanzania baada kususwa na Mungu, tunamtegemea nani ? halafu taifa teule mbona Mungu amelipa kashamba kadoogo ka kugomeana na wenziwe ? huyu Mungu yuko rational kweli ?
Hawa wamepewa eneo dogo, na takatifu. Hawa hawako milioni 45 kama watanganyika, bali ni nchi ndogo yenye akili. sio kubwa jinga.
 
Hawa wamepewa eneo dogo, na takatifu. Hawa hawako milioni 45 kama watanganyika, bali ni nchi ndogo yenye akili. sio kubwa jinga.

kweli wewe bado ji.nga wakuamini israel ni taifa teuke,

mungu anawapenda na kuwalinda taifa linalo ongoza kwa ushoga na uchafu ?

hebu tuwe tunatumia hata akili kidogo tu
 
Naomba ufafanuzi zaidi kuhusiana na kuteuliwa kwa hilo Taifa takatifu na utakatifu upi hasa unafanywa na Taifa hilo.Naomba sana nauhakika wengi watapenda kujua huu utakatifu kwa melezo itakayo toa mifano ambayo itakayokubalika duniani.
 
Kwa kadri ya uelewa wangu,ni vigumu sana kupata bidhaa iliyoandikwa Made in Israel,ni sheria ndani ya Israel kwamba hairuhusiwi kabisa kuandika made in Israel kitu chochote isipokuwa kama malighafi iliyotumika kutengeneza kitu hicho kwa kadri ya asilimia hamsini 50% imetoka ndani ya Israel yenyewe.

Kwa mantiki hiyo,labda ndizi kama nazo zinakuwa MADE au matunda mengineyo kama yanakuwa MADE ndo inawezekana yakaandikwa,kwa bidha zingine nyingi sana mali ghafi zinatoka nje ya Israel hivyo kukosa uhalali wa kuandikwa MADE IN ISRAEL,sasa hawa South Africa hadi kufikia hapo sijui walikuwa wanazungumzia bidhaa zipi ? kwani ni sawa na kuweka Caranteen ya nyama ya kitimoto kutoka Pemba,wakati ukweli si tu kwamba kitimoto hakizalishwi pemba bali hata biashara ya hicho kitu haipo, labda kama wamesema hivyo ili kuwavika WAPALESTINA kilemba cha UKOKA. Kama ni bidha za kutoka Israel hazikwepeki,labda kama ugunduzi na technology visiwe bidhaa kwa minajili hiyo.
 
naona hawa south afrika wanawalipizia kisasi baada ya israel kussport apaetheid afrika kusini
 
Naomba ufafanuzi zaidi kuhusiana na kuteuliwa kwa hilo Taifa takatifu na utakatifu upi hasa unafanywa na Taifa hilo.Naomba sana nauhakika wengi watapenda kujua huu utakatifu kwa melezo itakayo toa mifano ambayo itakayokubalika duniani.

KIBIBLIA ZAID. HII ILITOKEA PALE MUNGU ALIPOMWITA ABRAHAM, ABRAHAM AKAITIKIA WITO WA MUNGU NA AKAFANYA ALIYO AMRIWA KUFANYA NA MUNGU AKAMUAPIA ABRAHAM NA KUMWAMBIA ATAMFANYA KUWA TAIFA KUBWA. ABRAHAM AKAJITAFUTIA MTOTO (KINYUME NA AHADI YA MUNGU) AITWAE ISHMAEL. LAKIN MUNGU HAKUMTUPA ABRAHAM HIVYO MUNGU AKAMZAWADIA ABRAHAM MTOTO WA AHAD ISAKA.

ISAKA AKAWA NA WATOTO WAWILI YAKOBO(AMBAYE BAADAE ALIITWA ISRAEL) NA ESAU. BAADAE YAKOBO AKABARIKIWA NA BABA YAKE (BAADA YA KUMZIDI MAARIFA KAKA YAKE).

YAKOBO AKAWA NA WATOTO 12 AMBAO NDO MAKABILA 12 YA ISRAEL

MY TAKE: HAPO KWENYE NYEKUNDU (BABA YAKE WAKATI ANAM-BARIKI ALIMWAMBIA: MWANZO 27:28-29 UNASEMA
[SUP]28[/SUP]Mungu akumiminie umande wa mbinguni;akupe ardhi yenye rutuba,nafaka na divai kwa wingi.[SUP]29[/SUP]Jamii za watu zikutumikie,na mataifa yakuinamie kwa heshima.Uwe mtawala wa ndugu zako,watoto wa kiume wa mama yako wakuinamie kwa heshima.Kila akulaaniye na alaaniwe,kila akubarikiye na abarikiwe!"
)

HAPA NDIPO ILIPO SIRI YA MAFANIKIO
 
South wamesema hivi ......... Bidha ambazo hazijatengenezwa Israel ila zimetengenezwa mahali pengine hata kama ni wairael basi zioneshe made in location ile na sio israel. Ndivyo nilivyoelewa lakini hawakusema wanakataa bidhaa za israel
 
Wanaompenda na kumfuata Mungu kwa kuzishika sheria zake ndio taifa teule
 
Back
Top Bottom