Source Mwananchi 28/10/2011 - Sudan ilifadhili Mauaji ya Muammar Gaddafi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Source Mwananchi 28/10/2011 - Sudan ilifadhili Mauaji ya Muammar Gaddafi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Diehard, Oct 29, 2011.

 1. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Rais wa Sudan, Omar Al Bashir amesema nchi yake ilitoa msaada wa wapinzani wa Libya waliomuondoa madarakani Kanali Muammar Gaddafi.

  Katika hotuba kupitia televisheni, Bashir alisema hatua hiyo ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa Gaddafi kutokana na yeye kuwaunga mkono waasi wa sudan miaka mitatu iliyopita.

  Sudan na Libya hawajawa na uhusiano mzuri kwa miaka mingi. Rais Al Bashir alisema kundi la JUSTICE AND EQUALITY MOVEMENT (JEM) ambalo ni la waasi kutoka Dafur lilivamia Khartoum miaka mitatu iliyopita wakitumia magari ya jeshi la libya, vifaa, silaha, na pesa kutoka serikali ya Muammar Gaddafi. Alisema Mungu amewapa Sudan fursa ya kulipiza mashambul;io kwa kutuma silaha na msaada kwa raia kwa utawala uliofanya mapinduzi.

  Tafsiri yangu:

  Kumekuwa na takwimu nyingi zisemazo Gaddafi alikuwa mtu mwema na kutolewa mtiririko wa mengi aliyowafanyia raia wake na wengine kujaribu kukataa maovu yake wakisema kuwa ni propaganda za kimagharibi lakini wanasahau kuwa Gaddafi alileta jeshi lake kupigana na Tanzania katika vita isiyomuhusu ambayo inasemekana wanajeshi wake wapatao 600 walikufa leo unasema alipenda raia wake.

  Ikumbukwe Gaddafi amewahi kuwasaidia waasi Chad na Sudan miaka ya nyuma, alihusika na kupotea kwa mwandishi wa habari wa Lebanon Shia imam Musa al-Sadr , ni huyu huyu Gaddafi aliyekuwa na shule ya kijeshi na moja ya graduates wake na ambao waliokuwa wanasapotiwa na Gaddafi ni hawa hapa Charles Taylor - Liberia, Foday Sankoh - mwanzilishi wa Revolutioneray United Front, Jean Bedel Bokassa dictactor wa Afrika ya kati, Blaise Compaore wa Burkina Faso aliyechukua nchi kwa kumuua Rais Thomas Sankara, Ni Gaddafi huyuhuyu aliye kuwa akilifinance kikundi cha waasi wa Ethiopia cha Mengistu Haile Mariam moja ya vikosi vibaya kuwahi kutokea Afrika katika mauaji.

  Kifupi Gaddafi aliwafadhiri waasi wa nchi nyingine ili tawala za nchi hizo zianguke alifanikiwa kwa kiwango chake na kwa kuwa aliishi kwa upanga na yeye kaondoka kwa upanga GAME ON NGOMA DRAW, Aliwafadhili waasi na waasi waliomuondoa walifadhiliwa na wengine kumbe mpaka Sudan labda na T+Z maana mauaji ya Gadafi yanapingwa kwa nguvu
   
 2. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Vyombo vyetu vya habari na kudesa,kopy and pesiti.Hii habari ilijurikana siku ameuwawa gadafi alafu hawa ndo wanaileta,wamekosa habari au?
   
 3. WILLY GAMBA

  WILLY GAMBA JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Aliwafukuza wapalestine 30,000 kutoka Libya na kuwaita ma ******,south America ameivuruga kwa pesa zake , karibia vita zote huko sponsor yeye
   
 4. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,263
  Likes Received: 10,455
  Trophy Points: 280
  kazi ipo.
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,754
  Likes Received: 6,029
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red; ongezea na tukio baya la ulipuaji wa ndege ya Pan Am huko Lockerbie, Scotland 1988 ambapo mamia ya raia wasio na hatia waliuawa. Halafu baadaye kwa kiburi kabisa kaja kumpokea kwa mbwembwe kama shujaa gaidi alilolituma kulipua ndege hiyo. Baada ya matukio mengi ya kushangaza ya Ghadafi, kama kuna tukio ambalo liliwaudhi mataifa ya magharibi ni hili la kumpokea gaidi kama shujaa. Kwa kituko hiki hata mimi "nilitabiri" mwisho wa Gadafi ulikuwa umewadia.

  Huyo Al-Bashiri wa Sudan naye asitake kujipatia "ujiko" hapa hana lolote huyo. Kwanza anatakiwa sasa hizi awe kwenye vizimba vya ICC huko The Hague akihojiwa na o'Campo. Alivyowafanyia weusi wa Sudan ya Kusini na Darfur, ni heri hata ya Gadafi.
   
 6. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kunaubaya gan? yeye si aliuwa pia kwa msaada wa marekani?
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  subiri wafuasi wake waje hapa!
   
 8. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pamoja na hayo zingatia kuwa Gaddafi alioa dada yake Al Bashir.
   
 9. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada hueleweki sijui kama unamsupport al bashir na mauaji yake ya watu weusi huko Dafur na South sudan? Kama gadaf alitoa msaada wa kusaidia watu wa dafur wanaouawa na serkali yao wenyewe basi alifanya vyema hata sisi tanzania tuna wanajeshi wetu huko dafur ili kumzuia al bashir kuua zaidi? Serkali nyingi za kiafrika ni kama hii ya ccm hapa kwetu, hazina haki wala demokrasia ndiyo sababu kuna waasi wengi afrika. watanzania kama tusingekuwa waoga na wajinga lazima tu waasi wangekuwepo hapa nchini kwetu. Waasi wanadai haki na lugha ambayo wakandamijazi kama ccm wanaoielewa ni vita na mauaji.
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, umemaliza kila kitu kwenye hii post yako
   
 11. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45


  Mkuu simsampoti Gaddafi najaribu kuonyesha kilichompata ni matokeo ya ya ukauzu wake
   
Loading...