Sophia Simba zao la mafisadi?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Sophia Simba zao la mafisadi?

Na Mbasha Asenga

MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

SOPHIA Simba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, amemtuhumu Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, akisema hana haki ya kutaja “mafisadi papa.”

Anauliza kwani Mengi ni nani? Na anahoji: Katika utawala wa nchi hii, Mengi ni nani? Simba ana ng’ang’ana kwamba “nchi hii inafuata mfumo wa sheria ambao mtuhumiwa ni mtu safi hadi athibitishwe na mahakama.”

Hivyo ndivyo kila mmoja anavyoamini. Hata Mengi hakuhukumu. Alichofanya ni kutuhumu na kuiachia serikali kufanya uchunguzi na kuchukua hatua.

Lakini ni jambo la fedheha mno kwamba anayetoa kauli za kutetea “mafisadi” ni Waziri mwenye dhamana na Utawala Bora. Huyu ndiye aliyechimbia kwenye kichaka cha “watuhumiwa.” Anasema kwa sasa, hakuna mtuhumiwa hadi itakapothibitishwa na mahakama.”

Serikali yenye watendaji makini, ilitarajiwa kusema, “tumezisikia tuhuma hizo na tunazifanyia kazi.” Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa. Serikali imejitosa kupambana na mtoa taarifa.

Hebu nimuulize waziri; hivi ni nani mwenye hatimiliki ya kupiga mbiu uhalifu unaotendeka ili watu wajihami? Ni waziri tu? Polisi, au ni TAKUKURU tu? Au nani hasa?

Je, si kweli kwamba kila mwananchi anao wajibu wa kusaidia serikali kwa kutaja mshukiwa au mtuhumiwa yeyote na ikibidi kuwa tayari kusaidia uchunguzi? Kila raia si mlinzi wa nchi yake?

Kama waziri Sophia anadhani kuwa Mengi amekwenda nje ya mipaka yake, atueleze basi, kama watu waliotajwa hawana tuhuma zilizoorodheshwa na vyombo vya habari kwa zaidi ya mwaka sasa!

Hivi waziri Sophia mara ya kwanza alisikia lini kuhusu Kagoda Agriculture Limited, kampuni iliyoasisi wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)? Anaweza kusema hili?

Aseme basi ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya wamiliki wa kampuni hiyo waliochota zaidi ya Sh. 40 bilioni za EPA ambazo zilipata kuhojiwa na maodita wa Deloitte and Touche kabla ya kufurushwa na kupewa kazi ya ukaguzi wale wa Ernst & Young.


Waziri Sophia hajapata kueleza hili. Hajasema upelelezi wa Kagoda umefikia wapi na lini utakwisha. Kinachoonekana na jitihada za serikali kutaka wananchi wasahau.

Waziri Sophia analia kwa kusikia wametajwa Rostam Aziz, Jeetu Patel, Subhash Patel, Tanil Somaiya na Yussuf Manji kuwa ni watuhumiwa ufisadi wakubwa.

Katika hawa, watatu wanakutwa katika karibu kila kashfa kubwa iliyopata kusikika nchini. Ufisadi wa rada yumo Somaiya ambaye Mkachero wa Makosa Mkubwa ya Jinai wa Uingereza (SFO) wamemtaja wazi.

Si Sophia wala serikali imenyanyua mkono kumwita na kumuuliza sababu za kufilisi taifa. Somaiya anatesa na kusaidia CCM.


Rostam anatajwa kuhusika na Kagoda, Richmond na Dowans; anatajwa kama mtu mjanja anayetanguliza maofisa wadogo wa ofisi yake ili kujilinda. Tungeambiwa amehojiwa lini, atashitakiwa lini?

Jeetu anatajwa kumiliki makampuni tisa kati ya 22, yaliyoiba Sh. bilioni 133 za EPA. Angalau huyu amefikishwa mahakamani kwa kesi tano. Yupo Subhash anayetuhumiwa kurubuni wananchi ili achukue ekari 1,000 za ardhi yenye madini ya chuma cha Liganga kwa mikataba sawa na ile ya wakoloni na Chifu Mangungo.


Na Manji amehusishwa katika ufisadi kupitia majengo ya NSSF na PSPF akiwa ameuza kwa bei kubwa mali aliyouziwa kwa bei ndogo tu baada ya muda mfupi.

Ni kwa namna hii mtu anashindwa kujua nini hasa maana ya watu hawa kulindwa na kutetewa?

Lakini inajulikana zipo fununu kwamba Sophia alitumia fedha nyingi ili kupata uenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-CCM).

Mtu aliye safi hawezi kuhangaikia kuongoza jumuiya ambayo imepata kutumika kudhoofisha mshikamano wa wanawake bila ya kujali itikadi zao kama ilivyotokea mwaka 1995 ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa UWT, Rhoda Kahatano kuvuruga mkutano wa Baraza la Wanawake wa Tanzania (BAWATA).

Mbinu hizo zilifanikisha BAWATA kupigwa marufuku. Lakini tayari furaha ya wengi imerejea baada ya Mahakama kutamka kwamba BAWATA ilisajiliwa kihalali.

Kwa hiyo Sophia alipewa fedha ili kutafuta kiti hicho. Tunamjua Sophia, hana kampuni yoyote ya kuzalisha fedha, hana mgodi wa dhahabu wala almasi, mshahara wake wa uwaziri na marupurupu yote si siri.


Hivyo basi, hata kama tangu ashike wadhifa wa uwaziri hajatumia hata senti moja ya mapato yake halali ya uwaziri, wapambe wake wasingeweza kuwa na fedha za kuhonga kiasi kilichoonekana kule Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi.

Tunajuliza ile takrima iliyokuwa ikitembezwa kwa jina la Sophia, ni fedha zake au kuna watu walijitolea kumsaidia na walifanya hivyo kwa malengo gani? Kumpa uenyekiti ili iwe je?


Sasa swali la kujiuliza: Waziri kama Simba anamsaidia vipi rais Jakaya Kikwete katika kupambana na rushwa na ufisadi? Lakini swali gumu zaidi ni hili: Waziri Simba anaweza kusema amefanya nini tangu akabidhiwe jukumu la kuongoza serikali?

Akiwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, kabla ya kuhamishiwa alipo sasa, kote huko Simba anaweza kusema amefanya nini? Ataje moja! Ninaamini na pengine si uchimvi kusema kwamba hana analoweza kusema alilisimamia na kwa maana hiyo amelitekeleza. Hana. Badala yake, Simba anaongoza kwa kugombana na wasaidizi wake.

Ni waziri, labda kwa sababu alijitoa muhanga katika mtandao wa mwaka 2005, basi! Hana anachosaidia taifa hili, huyu ni Waziri wa Utawala Bora, lakini ni Waziri anayethubutu kusema uongo.

Ni Simba aliyesema kwamba vyombo vya habari havikuwa vimetaarifiwa kufika Ikulu, siku kamati ya Rais Kikwete ya “Sakata la EPA” ilipokabidhi kazi yake. Huyu ni waziri wa utawala bora lakini anapenda kufanya mambo uvunguni.
 
unajua sina uhakika kama huyu mama ni fisadi au la ila anaelekea ni mswahili. kashazoea taarabu ambapo mtu akisikia tu mwimbo wa mwenzie ana kupuruka nae kutoa ya kwake. Nadhali kaulu yake ilikuwa ya kukupuruka. Ajira anaipenda kwa hiyo kwa mawazo yake ana taka kujiweka upande anaozani uta shinda. I just think she is not an intelligent person. Kama ni mtetezi wa mafisadi au la sijui ila inavyo elekea ni kuwa huyu mama ana upeo mdogo.
 
Gazeti linaonyesha kutumika hakuna lolote lile ni majungu tu wote ni wezi huyo simba ni mwizi na gazeti ni la mwizi ,mwaga moga namwaga ugali ndivyo walivyo.
 
At least she can speak! Allow her to speak so we can learn and understand our government perspective. If what she is saying was against the government, it would have reacted. Lets go beyond Sophia Simba my people!
 
mtawasema CCM mwaka huu mpaka mtachoka, nadhani mnazidi kukokotoa hesabu ambayo jibu lake linajulikana!

CCM wote hamna kitu, hakuna hata mmoja, sijamuona bado
 
mtawasema CCM mwaka huu mpaka mtachoka, nadhani mnazidi kukokotoa hesabu ambayo jibu lake linajulikana!

CCM wote hamna kitu, hakuna hata mmoja, sijamuona bado

That a generalized statement! I will not say all CCM are hopeless, while i know few of them.

Let's get out of generalization, it will help us to move ahead!
 
At least she can speak! Allow her to speak so we can learn and understand our government perspective. If what she is saying was against the government, it would have reacted. Lets go beyond Sophia Simba my people!

Nakubaliana na wewe kwenye hili. Bora waongee wakiongea pumba tuwajue. Wakiongea at leat we will know where they stand.
 
alitetewa hapa na Mzee Mwanakijiji kwa sauti nzito...watu walipohoji kuhusu statement zake alipopata U-wenyekiti wa bosheni, sasa mnaona? she has shown her true colors..khalaghabaho....!
 
- Huyu mama hata kumuongelea ni waste of time, ni samaki mdogo sana anayejaribu kuwa mkubwa kwa nguvu sana lakini hakuna anayemjali! na hawezi kutuondoa kwenye mada muhimu ya mafisadi papa!

FMEs!
 
binafsi sijui kinachofanya muungwana kumuacha huyu mama katika baraza lake pamoja na upeo MDOGO MNO alionao..ukimsikia anavyoongea tu unajua hakuna kitu kichwani,na kumruhusu kufunua mdomo wake hadharani...ni aibu huyu!
hivi ni kweli huyu mama ni mke wa al-maaruf Kitwana Kondo?
 
Jamani Sophia Simba kaokoka anasali kwa mama lwakatare, aliposhida UWT alitoa shukrani yake kanisani kwa mama lwakatare. ki ukweli ni kwamba ana upeo mdogo sana
 
Kimsingi Tanzania kama taifa tuna tatizo kubwa sana la kiuongozi kwa sasa! Something must be done!
 
Inasikitisha sana, just think of the guy at the top office, if these are the kind of people he is working with!! Nadhani kama mdau mmoja alivyosema, ni kupoteza muda kuongelea nonsense za huyu Sophia if I may call her by her first name! Yupo hapo kutimiza aliyoambiwa atimize, period, kulinda waliomweka pale!! Ni sisi ndio tunaoweza kusema sasa ubabaishaji kama huu lazima ufike mwisho nchi hii!!
 
Jamani Sophia Simba kaokoka anasali kwa mama lwakatare, aliposhida UWT alitoa shukrani yake kanisani kwa mama lwakatare. ki ukweli ni kwamba ana upeo mdogo sana

Inatoa picha gani kwenye Kanisa hilo? Inatia wasi kuona vibosile wengi wa Serikali wamo ndani ya kanisa hilo. Kulikoni?
 
unajua sina uhakika kama huyu mama ni fisadi au la ila anaelekea ni mswahili. kashazoea taarabu ambapo mtu akisikia tu mwimbo wa mwenzie ana kupuruka nae kutoa ya kwake. Nadhali kaulu yake ilikuwa ya kukupuruka. Ajira anaipenda kwa hiyo kwa mawazo yake ana taka kujiweka upande anaozani uta shinda. I just think she is not an intelligent person. Kama ni mtetezi wa mafisadi au la sijui ila inavyo elekea ni kuwa huyu mama ana upeo mdogo.
Duuh, unajua huyu ndio kamanda wa watu wa intelligence sasa kama yeye mtupu jamaa watakuwa wanaleta nini? Au hizo taarabu unazohisi ndo zinaweza zikawa zimemsukuma kuongea kama anataka kusutana!
Well, what we do define who we are. Majority have not learned the hard lesson that times change.Sio suala tena la kuongea halafu ukafikiri umeongea nini. Inatakiwa unafkiri kwanza kabla ya kusema.Vinginevyo itakuwa ngumu kusurvive in this prevailing political storm
 
Inatoa picha gani kwenye Kanisa hilo? Inatia wasi kuona vibosile wengi wa Serikali wamo ndani ya kanisa hilo. Kulikoni?

kwani unadhani viongozi wana mungu, hawana mungu wao ni pesa tu misikitini na makanisani ni ili waonekane
ingekuwa wanamuogopa mungu wasingekuibia......
mapadri na masheikh wenyewe wezi na kila siku wanasali
 
kwani unadhani viongozi wana mungu, hawana mungu wao ni pesa tu misikitini na makanisani ni ili waonekane
ingekuwa wanamuogopa mungu wasingekuibia......
mapadri na masheikh wenyewe wezi na kila siku wanasali

Taratibu mkuu nisije ikana imani bure!
 
Yu wapi mwanamama Mh. Sophia Simba na kundi lake la TOT kumkemea Rostam Aziz alionyesha kumkemea RM. Je yeye na kundi lake wanabariki majibu ya RM. Au fedha za kumwingiza madarakani??? Ameongea mfadhili na mtafuta fedha za kampeni za CCM wote wanapiga makofi je yeye hajamwita RM fisadi kwanini Mh. mama ya fisadi asitoe kauli???
 
Yu wapi mwanamama mh. Sophia Simba na kundi lake la TOT likiongozwa na Mkuchika au wanamwacha mwizi wao RA kusema atakalo ila mwingine ni kosa?.
 
Yu wapi mwanamama Mh. Sophia Simba na kundi lake la TOT kumkemea Rostam Aziz alionyesha kumkemea RM. Je yeye na kundi lake wanabariki majibu ya RM. Au fedha za kumwingiza madarakani??? Ameongea mfadhili na mtafuta fedha za kampeni za CCM wote wanapiga makofi je yeye hajamwita RM fisadi kwanini Mh. mama ya fisadi asitoe kauli???

Amejificha kwenye moja ya ofisi za kufuatilia vyama vya upinzani (wao wanajiita usalama wa taifa) akiandaa kesi dhidi ya Mengi. Huu mchezo aliuanza Masha na sasa mama Simba naye ameingia kumalizia mechi.

Kikwete bado hajajua amtumie nani kummaliza Mengi. Bado anazunguka zunguka tu. Moto umemwakia na hajui cha kufanya.
 
Back
Top Bottom