Sophia Simba azua balaa UWT Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia Simba azua balaa UWT Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamadari, Apr 28, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WIKI chache kabla ya mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba kufanya ziara mkoani Arusha, mambo si shwari ndani ya umoja huo mkoani hapa baada ya wanachama kujipanga kuwashitaki baadhi ya viongozi wao kwa madai ya ufisadi. Wanachama hao, pia wanadai wanaandaa ushahidi wa maandishi watakaoufikisha mbele ya mwenyekiti huyo. Ushahidi huo ni ule wa madai kuwa walitakiwa kutoa Sh100,000 kila mmoja kwa ajili ya ziara hiyo ya Simba, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora). Walisema kuwa malalamiko mengine watakayofikisha kwa mwenyekiti huyo ni pamoja na ubadhirifu wa mamilioni ya fedha walizochangishwa ambazo hawajui zilitumikiaje kutokana na kutosomewa taarifa za mapato na matumizi kwa muda mrefu huku wakitakiwa waendelee kuchanga fedha. Wakizungumza na Mwananchi, wanachama hao walidai kuwa tuhuma dhidi ya viongozi hao ni nyingi na kwamba wanashangaa kwamba hadi leo hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya viongozi wanaodaiwa kutosimamia vizuri matumizi ya fedha za saccos ya umoja huo na kusababisha bodi ivunjwe. "Hatutachanga hizo laki moja kwa ajili ya mapokezi ya mwenyekiti wetu kwa kuwa hata yeye mwenyewe hapendi sisi tunyonywe kwa mgongo wake. Akifika tutamweleza yote na ikiwezekana, basi viongozi wanaohusika wavuliwe madaraka mapema ili kupisha uchunguzi," alsema mmoja wa madiwani ambaye ni mwanachama wa UWT. Walidai kuwa walishachangishwa kiasi cha Sh30,000 kila mmoja kwa madai ya kumshika mkono Rais Jakaya Kikwete, lakini haikuwa hivyo na hawakuona matumizi sahihi ya fedha hizo na hivyo hawapo tayari kuchanga fedha nyingine kwa ajili ya kumshika mkono kiongozi yeyote. UWT mkoani hapa iko kwenyer mgogoro mkubwa kutokana na kundi la wanachama kuwatupia shutuma viongozi wao likidai kuwa ni mafisadi na kusababisha saccos hiyo ishindwe kufanya vizuri kazi yake ya kukopeshana http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/1068-sophia-simba-azua-balaa-uwt-arusha
   
 2. m

  magee Senior Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ubatili mtupu..........uwt!!!!!
  wanaojiunga pia ni ubatili mtupu na mnaupungufu wa kupembua mambo.........
  tujiunge kutafuta maendeleo na si kujiunga kuwaneemesha watu,eti 100,000 ya maandilizi ya mapokezi huku mtoto wako hana ada,huku zahanati yenu ya kijiji haina dawa,30,000 kumshika mkono mtu wakati mtu huyo mshahara wake mamilioni.watanzania ni lini mtaamka na kuacha upumbavu????mmeneemeka nini na uwt zaidi ya wachache wenu kukitumia kama chombo cha kupandia na kupata madaraka kwenye serikali kuu.
  wanawake ni jeshi kubwa...........embu tuungane kuleta mageuzi
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nawasikitikia masikini wanaosogea kwenye chama kama hicho...Hawa wanaendesha mambo yao kwa fedha bana..kama hujui kuiba unakufa na umasikini wako...Mbona wanaweka wazi kwamba kama huna kitu hutathaminiwa kwenye chama hicho, nyie mnaking'ang'ania cha nini kama ni makapuku?
   
 4. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dah kazi kweli kweli
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  laki moja ya mapokezi?....30 ya kumshika JK mkono? jamani jamani hizi siasa uchwara kazi kweli.
   
 6. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huwezi kuamini Tanzania watu wana matatizo sana, toka lini uwt ukamshika mkono JK, hayo si masihala jamani, nao wanashangalia na kushangilia, halafu viongozi wao wanawaona mabwege!!,

  WAKE UP women, changieni shughuli za maendeleo, kama kuboresha mashule, maabara mashuleni, mahospitali na huduma nyingine za jamii, hicho chama kimewaroga????? mpaka hamuwezi hata kufikiri?
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hahahahh, yaani Inzi asimamie usafi wa jalala? Imeshakula kwao maskini
   
Loading...