sony watangaza game lao jipya la playstation 4

sony watangaza game lao jipya la playstation 4

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,074
Reaction score
43,530
sony wamezindua game lao jipya la playstation four litakalokua na specs nzuri kidogo kama x86 based processor, cpu yenye core 8, ram 8gb na enhanced gpu kucompare na ile ya ps3.

Vitu muhimu kwenye hii playstation 4 ni hivi hapa

-itakua na uwezo wa kustream game (hudownload game bali linakua online kwa kutumia internet connection utacheza)

-uwezo wa kucheza game huku unalidownload. Lets say game lina gb 8 then umedownload gb 2 then utaanza kucheza huku linaendelea kudownload.

-watu watachat, kushare picha na video kwa kutumia ps4 zao. Mfano kuna game unaliweza sana mwenzako hata hajui aanze vipi unarekodi part ya game una upload kwenye server za sony mwenzako anadownload kuona umechezaje.

-pia kuna playstation vita (game lao la mkononi kama psp) wataliunganisha na ps4 liweze kushare games

-pad zake dualshock 4 zitakua na touchpad (kama ya pc) kwa ajili ya kunavigate vizuri kwenye ps yako cheki picha chini
LB_0365_large_extra_large.jpg

pia pad zake zitakua na 3d camera kutrack motion

-user interface imechange kabisa itakua kama hivi
LB_0440-1_large_extra_large.jpeg

sad thing ni kwamba ps4 haitacheza game za ps3 so nayo inaanza upya magame

hii demo ya game la killzone la ps4
LB_0788_large_extra_large.jpg
 
WoW!! Kwahyo Hapo Wataonunua Wajipangie na Budget Ya Games za playstation 4!!
 
WoW!! Kwahyo Hapo Wataonunua Wajipangie na Budget Ya Games za playstation 4!!

ila sababu kuna mambo ya streaming nahisi cost kubwa itakua internet badala ya kununua game.
 
ila sababu kuna mambo ya streaming nahisi cost kubwa itakua internet badala ya kununua game.

Unadhani Streaming itakuwa bure ?

Games Console Industry imeshaflop long time, sidhani kama watapata success waliyopata kwenye PS2.., anyway kila kitu na wakati wake.., its about time Sony wajiangalie kama kampuni .., ni wapi wanaweza kwenda (maybe invest in more in mobile devices)
 
Walichoudhi Sony ni kufanya uzinduzi bila ya kuionyesha console yenyewe, kama hawakuwa tayari kulikuwa hakuna haja ya kufanya uzinduzi jana. Hata hivyo hizi huduma kama streaming, sharing video n.k. Si mambo mapya kwa vile kwa kutumia PS3 haya yote yanawezekana. kwa hiyo sijui kivutio n cha mauzo kitakuwa jambo gani?
 
Toka alivyo retire Ken kutaragi.. Sony has no future on video game industry,, vitu karibu vyote wanavyosema PS3 inafanya.. So sijui wateja watababaika na nini?

Let's wait microsoft x box 720 tuone nao wamekujaje?
 
Yana addiction mbaya hayo ma PSP acha kabisa
 
Walichoudhi Sony ni kufanya uzinduzi bila ya kuionyesha console yenyewe, kama hawakuwa tayari kulikuwa hakuna haja ya kufanya uzinduzi jana. Hata hivyo hizi huduma kama streaming, sharing video n.k. Si mambo mapya kwa vile kwa kutumia PS3 haya yote yanawezekana. kwa hiyo sijui kivutio n cha mauzo kitakuwa jambo gani?

yah kweli umeongea mkuu huwezi ukazindua kitu then usikioneshe kitu chenyewe je likija kama kabati hilo game
 
Unadhani Streaming itakuwa bure ?

Games Console Industry imeshaflop long time, sidhani kama watapata success waliyopata kwenye PS2.., anyway kila kitu na wakati wake.., its about time Sony wajiangalie kama kampuni .., ni wapi wanaweza kwenda (maybe invest in more in mobile devices)

mkuu unadhan why wanaflop? Sababu hawana innovation wanachange design tu then na kuongeza specification basi nothing new wakati kuna computer kibao unapata games za maana.

Nimependa idea ya ps vita ya kuwa na 3g ili mtu utumie kama game na ueke line na bundle utumie na browser kudownload movies na kubrowse. Walitakiwa wafanye addition za namna hii nyingi ili kusave games zao.

Pia ile concept ya ilumiroom ya microsoft wanatakiwa waimplement fasta kama na wao wanataka kusurvive
 
Back
Top Bottom