Sonona! imenielemea. Msaada!

Duh! Ila hii Dunia Kweli imejaa changamoto 😥

Pole Sana mkuu kwa yote unayopitia Mungu akufanyie wepesi jamani 🙏
 

Asisahau pia kujiombea na yeye mwenyewe ili mwenyezi Mungu aweze kuamua moja kati ya kumponya na matatizo yanayo mwandama au kumchukua mapema ili akapumzike alipoandaliwa.
 
Sijui niandike nini nimeishia Julia tuu na kukumbuka mapito yangu hakika mng wa mbinguni anayo sababu na hatokuacha.Amini wapendwa wako wamekwenda kupumzika na mateso ya hapa Duniani
 
Pole sana muombe mungu atakusaidia
 
mwezi huu tareh 20 nikapoteza tena mwanangu wa mwisho wa miaka minne
Pole sana mkuu Mungu akufanyie wepesi.
Naona hapo umepitiwa, huu ni mwezi wa pili tarehe za mwanzo. Urekebishe ili kuweka kumbukumbu vizuri.
 
1. Muombe mungu
2. Nenda kwa mchungaji akuongoze kwenye maombi yako na familia ili Mungu akuvushe kwenye hlo jaribu na kama mazindiko yatoke
3. Nenda hospital kwa psychologist
Akusaidie kisakolojia
4. Ukiwa kama mtoto wa kiume unapaswa kuvumilia na kutokata tamaa kwan ww ndio msaada wa pekee wa kuisadia familia yako upo vitani haupaswi kukimbia uwanja wa mapambano pambana kufa kupona mpk uibuke mshindi kwa familia yako ili ujenge heshima na uwe mfano kwa wanaopitia kama unayoyapitia. MUNGU AKUSAIDIE NA KUKUONGOZA KWENYE HILO JARIBU
 
- maisha safari ndefu sana
-Kesho ni fumbo
  • chochote kinaweza kutokea.
  • usipange sana mipango
-
pia usihesabu mabaya! maana mabaya yanaongozanaga kama mabehewa ya treni, Muburi 3:1 -8
Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake: kuna wakati wa kulia/kucheka wakati wa kupata/kupoteza ...wakati wa vita/amani..
Ulizaliwa pekeako, hukuja na mtu hatma yako ni yako! ni vile hatujiandai kuyakabili magumu tunajisahau sana..ila yote hayo hayana budi kutokea, yameshatokea jikaze mwanaume mambo ni magumu ila jikaze beba familia iliyobaki bado Mungu anampango na nyinyi... kama rdhiki inapatikana Mshukuru Mungu usonge mbele , hata usiku uweje patakucha tu hata pakikucha uko juu ya mawe ila pamekucha tayari... kwasasa unaweza usijue chanzo ila Move on ..

watakaovumilia mpaka mwisho ndio watakombolewa
 
Pole sana Mkuu.

Wewe ni jasiri sana, ipo siku Furaha yako itarejea na Familia itastawi tena..
 
Pole sana ndugu, hebu rudi magotini kwa kwa maombi ya mfungo. Omba kwa imani yako na muombe Mungu akutakase na atakase familia yenu.

Kama una chochote kitu nunua vyakula vyakula chagua kituo cha watoto wa mazingira magumu katoa hiyo sadaka yako na muombe Mungu akuguse kupitia sadaka hiyo.

Tafuta mtumishi wa Mungu unayeona ana nguvu za kiroho kushinda za kwako, mweleze na akuwekee mkono akuombee. NB: watumishi wa Mungu wenye nguvu sio hawa wamiliki wa makanisa haya makubwa makubwa.

Kuhusu mikopo inabidi ulisolve kibinadamu, kwa kubadili kazi yako ya sasa kama inawezekana, au kama una chochote muwekezee wife afanye aingize hata kidogo mjikwamue na mikopo.
 
Siku Mwenyezi Mungu atakufunulia yote yalojificha !

Kama uko honestly hujawaumiza watu kama makosa ni haya ya bahati mbaya ya kibinadamu Mungu atakuhurumia na kukusamehe na kukupa fidia ya ulowapoteza.

Achekae mwisho hucheka sana.

Mwenyezi Mungu atakufuta machozi yako.

Mtafakali yeye na kutenda mema.

Jivike subira na ustahamilivu Mkuu.

Imeandikwa;

“Kheri wanao subiri “
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…