Sonona! imenielemea. Msaada!

Sonona! imenielemea. Msaada!

inakuaje watoto wako wanafaliki kirahisi namna hio bila sababu ya msingi ...
 
Pole sana mkuu. That's life pengine jaribu kuongea na watu wazima wa ukoo au viongozi juu ya unayoyapitia wanaweza kukupa ufumbuzi wa changomoto zako. I know it's hard but you have to find solution
 
Pole sana Mungu akutetee. Mtafute mchungaji lubuva atakupa msaada maombi hiyo roho iondoke mpigie 0657578803
 
Tumia karafuu ndo dawa ya ugonjwa uo wa sonona

Mwaka jana nilikuwa nimepigwa na ugonjwa uo baada ya kupitia matukio fulani katika maisha yangu.

Nilipata matatizo kweli kweli

Mwanzo nilikuwa nafikiri nimerogwa kabisa

Na kila nikienda hospitali kinaonekana sina tatizo lolote kabisa linalo ni sumbuwa

Nilikuwa ninahisi ninaweza kukimbia porini

Nilihisi nina matatizo ya moyo kwasababu mapigo ya moyo yalikuwa wanapiga kasi

Nilitamani kufa kwasababu ya mateso ambayo nilikuwa nayo bila msaada

Lakini kuna mtu ambaye aliniambia dawa ya ugonjwa uo ni karafuu mimi nilikuwa sijui sonona
Mimi nilikuwa nafikiri ni uchawi tu.

Lakini baada ya mtu fulani kusikia maelezo yangu ndo akaniambia wewe una matatizo ya sonona na dawa yake ni karafuu nilivyo anza kutumia karafuu akili yangu niliona imeanza kutulia uoga umenitoka.

Mpaka nikapona.

Na nimesaidia watu wengi na wao wamepona kabisa.

Kwa hiyo ndugu yangu kama una matatizo ya sonona kweli sio mengine dawa ya ugonjwa uo ni karafuu
 
Tumia karafuu ndo dawa ya ugonjwa uo wa sonona

Mwaka jana nilikuwa nimepigwa na ugonjwa uo baada ya kupitia matukio fulani katika maisha yangu
Nilipata matatizo kweli kwel...
Karafuu unaitumiaje?
 
Poleh kaka
Mrejee muumba kwa sala

Naomba nikupe aya moja tu kuwa Mwenyezi hampi mja majaribu zaidi ya uwezo wake
Sali tu muachie Mungu
Poleh sana
B3B69F1F-243F-4E5F-9946-D6A0031570A6.jpeg
 
Karafuu unaitumiaje?
Unatengeneza chai yake.

Alafu unakuwa unakunwa kikombe kimoja asubuhi na jioni kwa mda wa siku tano au zaidi upendavyo wewe ila mimi nilitumia kwa mda wa siku tano na Nikaona akili yangu imetulia.

Uoga na mawazo potofu yakanitoka.

Maana sonona ni ugonjwa wa saikolojia tu ambao unahasiri akili ya mtu
 
Mkuu

Hongera sana KWA kuandika!

Hongera KWA kutojiua hadi Sasa!

Hongera kwakua Mama yako mzazi alizaa Mwanamme wa shoka!

Hongera KWA kuwa mpambanaji!

Hongera kwa kuwa wewe ni mtu muhimu Sana Tanzania imewahi kumpata!

Hongera KWA kuuona mwaka huu!

Hongera KWA kuwa wewe ni mshindi wa yote!!


Sasa Basi!


Ingia chumbani mwako umshukuru Mungu umwambie unamshukuru KWA wewe ni mshindi!

Halafu kuhusu wanaokutegemea Hao wagonjwa mwambie hivi

"Ewe Mungu Hawa ni Watoto wako umewaumba wewe !Amua mstakabali waO Sasa hivi ,kama ni mapenzi yako waponye Sasa kama sio mapenzi yako wachukue Sasa na unipe ujasiri wa kuwazika KWA amani na furaha kuu!!!

Ongezea hivi

"Hatma ya Maisha yao ipo kwako mimi hata nikiwahangaikia kiasi Gani siwezi fanya chochote juu ya uhai waO!naomba uamue Sasa unawaponya au unawachukua!

"Inatosha Sasa naomba nipumzike na haya niishi VIZURI KWA furaha tele!!NATAKA HAYO SASA NIMECHOKA!

Baada ya hapo utatoka ukiwa Mpya kabisa!
 
mkuu ukijishangaa wewe kuna wenzio wanapitia mazito kuliko wewe ndani ya miaka miwili wamepukutika namaanisha kufariki watu sita kwenye familia moja kwa kufatana, alianza mama yao hawakumaliza arobaini akafariki mdogo wao kwachangamoto ya uzazi wakapumzika miezi kadhaa akafariki kaka yao aliekua msaada sana kwao haukupita mwezi akafa mdogo wao wa mwisho haukupita mwaka akafa kaka yao aliebakia hakupishan sana na mdogo wake wakike hivi nikuambiavyo wamebaki wawili tu mmoja anaumwa mmoja haeleweki makaz maalum

viatu vyako ni vizito mno, lakini jikaze wewe ndio faraja ya mkeo, ndio faraja ya mama yako, hio itoshe kukupa nguvu na ujasiri wa kuyashinda hayo, Muombe sana Mungu akusaidie utavuka ukikaza kiume hayo ni majaribu hicho kikombe utakivuka kwa uwezo wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom