SONGWE: Wakazi walalamika kupelekewa condoms nyingi kuliko dawa

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
19,315
56,318
Wananchi wa Songwe wameilalamikia serikali kwa kitendo cha kuwapelekea kondom nyingi kuliko dawa nyingine na kudai kwamba kitendo hicho ni udhalilishaji kwa wananchi.
07fdc7f62b9086424efddae498a22b8e.jpg
 
Waambie waache uthenge! Hakuna dawa ya UKIMWI ndio maana wanapelekewa ndom wasije wakaukwaa... Waambie waache ujuaji... Kwanza utapelekewaje dawa wakati hauumwi?
 
itakua za msd hzo ndo maana wanalalama, kavp wamwape 3bomba au rough rider
 
Juliana Shonza mbunge wa viti maalum CCM mwenyeji wa Songwe kutwa yuko mitandaoni na ID tatu-tatu kutwa kueneza propaganda za buku 7 kwa thread alafu ndugu zake na wazazi wake huko Songwe wamejaziwa Kondom na Paracetamol kwenye maghala ya dawa.


Nakupa assignments nitaisahihisha baada ya vikao vya bunge:

Ewe Juliana nshonza ingia field, pata ukweli, fata protocal kufatilia ikiwezekana ufike hadi kwa waziri husika pata majibu ukiiingia bungeni vikao vinavyoanza kesho, wasemee watu wa Songwe taarifa utakua nazo kwa wingi,
sasa hivi wagonjwa wanaandikiwa kondom na daktari badala ya dawa kwakuwa hakuna dawa.
Kuwa na roho ya kibinadamu achana na siasa za mtaroni walau kwa siku moja andaa points andika jina kwa speaker wasemee shangazi zako wa Songwe walau kwa hili la dawa pekee alafu baada ya hapo ndiyo uendelee na biashara yako kichaa ya mapovu mitandaoni.
 
Depopulation agenda hiyo! Inawezekana wala sio mkakati wa serikali.It could be a gift from an NGO!Ndio zao hizo.
 
Serekali ingekuwa inanunua kondomu kwa fedha zake isingepeleka kondomu nyingi Songwe lakini kwa kuwa zinanunuliwa na wafadhiri ndiyo maana serekali imegeuza Songwe kuwa dampo la kondomu.
 
Back
Top Bottom