Naibu waziri anadai kodi ya majengo ambayo hayajasajiliwa wala kupewa na ya utambuzi malipo serikalini kwa kutumia sheria gani?
Jengo lolote ambalo serikali halikulisajili ni sharti waanze kulitambua mmiliki wake kisha wampe namba ya kulipia (Control Number) na risiti ya mashine ya EFD itolewe. Malipo yafanyike benki iliyoteuliwa kwa malipo na serikali sio mamlaka ya serikali za mtaa ambazo tutakuwa tunazalisha utapeli wa kuneemesha mabwanyenye huku mwananchi akikamuliwa hata damu ilnayomfanya afanye kazi na kuzalisha.
Walidai utaratibu wa upimaji wa kurasimisha makazi ungepunguza karaha ya upatikanaji wa hati kwa kutumia muda mfupi angalau miezi sita, lakini kwa sasa mtu kapimiwa hakuna 'Beacon' zilizowekwa wala dalili za hati kutolewa pamoja na kwamba kalilipia gharama zilizotakiwa-hii ni dhuluma ambayo haikubaliki chini ya jua.
Wasije wakageuza suala hili kama usumbufu na kuamsha hasira zenye nongwa (pandora box) kama ilivyokuwa kwenye kodi ya kichwa na kodi ya baiskeli miaka ya sabini, themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini ni sawa na mtu unamvamia nyumbani kwake, hataogopa kujilinda kwa kupambana. Kilichotakiwa ni kutoa elimu hiyo kwanza kwa miezi angalau sita kuhusu hizo kodi kuliko kupanga wazo la kupata kodi na kuanza kutekeleza kana kwamba wananchi wanakosa.
Honorable deputy minister is cautioned to handle this matter carefully otherwise she may end up regretting. Tanzanians have now reached zero tolerance, if she doesn't understand what the situation is all about the hardship they currently encounter, let her cruel task force attempt depriving their welfare the true color will be precisely exposed.