Songwe: Naibu Waziri Mabula ataka makusanyo ya kodi ya ardhi yafike 50% ifikapo Machi 31

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,037
20,333
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angelina Mabula amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na wakuu wa Idara ya Ardhi kwenda kukusanya kodi ya Ardhi na ifikapo Machi 31 2021 iwe imefika 50% au 75% kutoka 23% iliyopo sasa ambayo imekusanywa ndani ya miezi 8 tu ya mwaka wa fedha 2020/2021.

"Yeyote ambaye atashindwa ni kufikisha asilimia 50% au 75% ifikapo Machi basi ajitathimini kama anaweza kuendelea kuwa Mkuu wa Idara au Mteule" Naibu Waziri, Dkt. Angelina Mabula.

Pia, Naibu Waziri amezitaka Halmashauri kupitia vikao vyao vya kila mwezi kufuatilia makusanyo ya Ardhi kwani watalamu wa Ardhi bado kiutendaji wako Halmashauri ila Wizarani wapo kwa mambo mawili ya nidhamu na ajira tu.
 
USIMLAUMU wakuu wa vitengo vingi vya kiserikali WAMEPEWA MALENGO NA VITISHO LA SIVYO WANATUMBULIWA. Maagizo yanatolewa na rais then yanashushwa kwa wakuu wa mikoa then ma DC then kwa kwa hao wakuu wa idara na vitengo.

Nimeshangaa kuona hadi ma RTO na ma DTO wamepewa malengo as if kama nchi inafurahia ongezeko la makosa ya barabarani? TUTAJIONEA MENGI MUHULA HUU
 
Naibu waziri anadai kodi ya majengo ambayo hayajasajiliwa wala kupewa na ya utambuzi malipo serikalini kwa kutumia sheria gani?

Jengo lolote ambalo serikali halikulisajili ni sharti waanze kulitambua mmiliki wake kisha wampe namba ya kulipia (Control Number) na risiti ya mashine ya EFD itolewe. Malipo yafanyike benki iliyoteuliwa kwa malipo na serikali sio mamlaka ya serikali za mtaa ambazo tutakuwa tunazalisha utapeli wa kuneemesha mabwanyenye huku mwananchi akikamuliwa hata damu ilnayomfanya afanye kazi na kuzalisha.

Walidai utaratibu wa upimaji wa kurasimisha makazi ungepunguza karaha ya upatikanaji wa hati kwa kutumia muda mfupi angalau miezi sita, lakini kwa sasa mtu kapimiwa hakuna 'Beacon' zilizowekwa wala dalili za hati kutolewa pamoja na kwamba kalilipia gharama zilizotakiwa-hii ni dhuluma ambayo haikubaliki chini ya jua.

Wasije wakageuza suala hili kama usumbufu na kuamsha hasira zenye nongwa (pandora box) kama ilivyokuwa kwenye kodi ya kichwa na kodi ya baiskeli miaka ya sabini, themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini ni sawa na mtu unamvamia nyumbani kwake, hataogopa kujilinda kwa kupambana. Kilichotakiwa ni kutoa elimu hiyo kwanza kwa miezi angalau sita kuhusu hizo kodi kuliko kupanga wazo la kupata kodi na kuanza kutekeleza kana kwamba wananchi wanakosa.

Honorable deputy minister is cautioned to handle this matter carefully otherwise she may end up regretting. Tanzanians have now reached zero tolerance, if she doesn't understand what the situation is all about the hardship they currently encounter, let her cruel task force attempt depriving their welfare the true color will be precisely exposed.
 
serikali imetibua vyanzo vya hela vya nje na sasa ipo bize KUKAMUA WANANCHI MPAKA WATUBU.
 
USIMLAUMU wakuu wa vitengo vingi vya kiserikali WAMEPEWA MALENGO NA VITISHO LA SIVYO WANATUMBULIWA.
Maagizo yanatolewa na rais then yanashushwa kwa wakuu wa mikoa then ma DC then kwa kwa hao wakuu wa idara na vitengo.Nimeshangaa kuona hadi ma RTO na ma DTO wamepewa malengo as if kama nchi inafurahia ongezeko la makosa ya barabarani? TUTAJIONEA MENGI MUHULA HUU
Kweli mkuu
 
'
JamiiForums970533619.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom