Songea na Bus Stand za katikati ya mji

Songea na Bus Stand za katikati ya mji

kimatire

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2008
Posts
371
Reaction score
94
Ni hapo jana tu Madiwani wa Manispaa ya Mji wa Songea wakilumbana kurudisha stand ya mabasi katikati ya mji wa Songea kutoka pembezoni eneo la Msamala,Nje kidogo ya mji barabara ya kuelekea Njombe,ilikohamishiwa kwa muda.
Ni habari za kusikitisha kuona kwamba viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza hawafikirii mbali hata kidogo.Kinyume chake wanafikiria mapato yatokanayo na maegesho maeneo ya mjini.Mji huu wa Songea unatanuka japo si kwa haraka sana lakini unapanuka kutokana na shughuli nyingi za kibiashara na huduma.Leo hii ukifikiria kuingiza mabasi makubwa hata madogo mjini ni kero kubwa ,mbali ya kutokuwepo na msongamano wa magari.Pia ufinyu wa eneo la maegesho, barabara siyo kwamba ni pana za kutosha.Lakini pia shughuli za waenda kwa miguu ndani ya mji zimeongezeka sana kiasi kwamba idadi ya wakaazi pia nayo imeongezeka vile vile.Wazo la kupeleka stend eneo la Msamala lilikuwa ni ili kupisha ukarabati wa stend ya zamani,Hata hivyo ulikuwa uamuzi maridhawa sana kwani ilikuwa fursa pekee ya kuondoa maegesho hayo katikati ya mji, Ukizingatia mji unapanuka na eneo hilo tayari ni makazi ya watu , tena isitoshe ni njia ya kutokea na kuingilia mjini .Sasa jana ukawa ubishani usio na tija kurudisha stend katikati ya mji.Nachelea kuwashangaa viongozi hawa wa Manispaa ya Songea kwamba hata hawajifunzi kutoka kwa miji mingine?Uamuzi wa kuhamisha hiyo stend hawaoni umechelewa sana? Watafakari upya maamuzi yao.
 
mm nafikiri stand ya mjin ambayo imekarabatiwa kwa sasa ibaki kuwa stand ya magari ya mikoani na ile ya msamala iwe ni stand ya magari yanayoenda wilayani pamoja na daladala nafikiri hii itapunguza msongamano wa magari mjin
 
mm nafikir kwa mtazamo wangu stand ya mjini ambayo imekarabatiwa ibaki kuwa stand ya magari ya mikoan na ile stand ya msamala iwe stand ya magari ya wilayani pamoja na daladala kwa sababu ni kubwa na hii itasaidia kupunguza msongamano wa magari mjini
 
Kwahiyo kimeamuliwa nini?? Punguza jazba.
 
Ila kati ya miji ambao ina poor siting of the bus terminal ni Songea..sema hao wafanya biashara hapo wamewashika mipango miji . Ni muhimu Ihame.
 
Ni hapo jana tu Madiwani wa Manispaa ya Mji wa Songea wakilumbana kurudisha stand ya mabasi katikati ya mji wa Songea kutoka pembezoni eneo la Msamala,Nje kidogo ya mji barabara ya kuelekea Njombe,ilikohamishiwa kwa muda.
Ni habari za kusikitisha kuona kwamba viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza hawafikirii mbali hata kidogo.Kinyume chake wanafikiria mapato yatokanayo na maegesho maeneo ya mjini.Mji huu wa Songea unatanuka japo si kwa haraka sana lakini unapanuka kutokana na shughuli nyingi za kibiashara na huduma.Leo hii ukifikiria kuingiza mabasi makubwa hata madogo mjini ni kero kubwa ,mbali ya kutokuwepo na msongamano wa magari.Pia ufinyu wa eneo la maegesho, barabara siyo kwamba ni pana za kutosha.Lakini pia shughuli za waenda kwa miguu ndani ya mji zimeongezeka sana kiasi kwamba idadi ya wakaazi pia nayo imeongezeka vile vile.Wazo la kupeleka stend eneo la Msamala lilikuwa ni ili kupisha ukarabati wa stend ya zamani,Hata hivyo ulikuwa uamuzi maridhawa sana kwani ilikuwa fursa pekee ya kuondoa maegesho hayo katikati ya mji, Ukizingatia mji unapanuka na eneo hilo tayari ni makazi ya watu , tena isitoshe ni njia ya kutokea na kuingilia mjini .Sasa jana ukawa ubishani usio na tija kurudisha stend katikati ya mji.Nachelea kuwashangaa viongozi hawa wa Manispaa ya Songea kwamba hata hawajifunzi kutoka kwa miji mingine?Uamuzi wa kuhamisha hiyo stend hawaoni umechelewa sana? Watafakari upya maamuzi yao.
wajifunze kwenye Halmashauri zingine wanafanyaje...! Waangalie zile ambazo stand zipo ktkt ya mji, waone kero iliyopo mjini asbh
 
Back
Top Bottom