Songea: Basi la kampuni ya Super Feo lapinduka na kuua

Songea: Basi la kampuni ya Super Feo lapinduka na kuua

Barabarani tunakumbana na changamoto nyingi sana, zikiwemo za reckless driving ya vyombo vya usafiri na mabodaboda, rough overtaking, etc.
 
nimeangalia picha kwenye blog kwa hiyo link hapo juu kuna picha ya basi kabla halijaanza safari likiwa stend na baada ya ajari, inamaana aliyepiga picha alijua kuwa kuna ajari itatokea au!? kama sio ina maana huwa anapiga picha mabasi yote kabla hayajatoka!

tushangae wote!
Ushetani tu umetawala hzi biashara.
 
hapa unawasingizia wachina..
1. ajali ya kule mara uso kwa uso...inamaana wachina wanafanya dereve aone barabara haina gar kumbe lipo?
2. Basi lililotumbukia korongoni huko moro baada ya dereva kushindwa kulala na kona.....speed 140km/hr kwenye kona bado unamlaumu mchina?

Labda tumlaum mchina kuleta kitu lain ukikanyaga inaserereka tu...waturudishie letland Daf max speed 55km/hr

fanya utafiti kwa kujaribu kuuliza ma driver wa hayo mabasi ya yutong watakuambia, kuwa yana matatizo kiasi fulani hasa kwenye gear na balance,.Sawa ajari nyingi ni uzembe wa madreva ila wahusika wajaribu kuangalia na ubora wa haya magari.Kwani kuna siku moja nilikuwa mtwara na kwenda dar, basi la mining nice tulichelewa sana kutoka mtwara kisa dreva aliamka anaumwa, sasa kumtafuta ambaye ataweza kuendesha hilo gari la yutong hata day worker tu ilikuwa shida, kila mtu anasema kwenye gear na kulala nalo kwenye kona ni shida!! ilibidi wamkodi jamaa tu aendeshe hadi lindi mjini tu, ndio tukapata dreva pale, mzoefu.hata hivyo kutoka hiyo mtwara hadi lindi mwendo mdodo mdodo sana!!Yaani haya mabasi yanakuwa na balance ndogo sana liwapo barabarani hususani likiwa kwenye mwendo kasi!!halitulii barabarani na hatari zaidi ni kwenye kona lazima uianzie kona mbali, ili ulale nalo taratibu,
 
kwani ukimsindikiza mtu na ukapiga picha kuna kosa?

Kwahiyo yule mwenye blog ile wataka sema alikuwa anamsindikiza nduguye akaamua apige picha kabisa na gari aliyopanda, baada ya ajari akaifuata tena gari akaipige picha aweke kwenye blog yake!?
 
Kwahiyo yule mwenye blog ile wataka sema alikuwa anamsindikiza nduguye akaamua apige picha kabisa na gari aliyopanda, baada ya ajari akaifuata tena gari akaipige picha aweke kwenye blog yake!?

una bonge la LOGIC ndg...
 
ujue sehemu iliyopata ajali sio mbali na town bodaboda just dk 15 pia waweza pata picha kwa watu wa sten ni mtazamo tu
 
nakumbuka kanisani Ngurumo Ya Upako-tuliambiwa Neno la kinabii kuwa tutoe sadaka ya kujiepusha na ajali maana zitafululiza,tamko hili lilitolewa kwenye mwezi June or July.. sasa naona huo Unabii..Mungu aturehemu na atuepushe wajaa wake
 
si huwa yanapishana hivi naabiria wanakuwa kimya??
 
Attachments

  • 1410358968393.jpg
    1410358968393.jpg
    64.4 KB · Views: 336
nimeangalia picha kwenye blog kwa hiyo link hapo juu kuna picha ya basi kabla halijaanza safari likiwa stend na baada ya ajari, inamaana aliyepiga picha alijua kuwa kuna ajari itatokea au!? kama sio ina maana huwa anapiga picha mabasi yote kabla hayajatoka!
Dah' , hata mimi nashangaa
 
Kwahiyo yule mwenye blog ile wataka sema alikuwa anamsindikiza nduguye akaamua apige picha kabisa na gari aliyopanda, baada ya ajari akaifuata tena gari akaipige picha aweke kwenye blog yake!?

Sio lazima iwe picha ya siku ya tukio coz wabongo unawajua kujifanya wapo up-to-date, utakuta picha ya mwez akasema ya leo.. Pia inawezekana alipoga picha ndiyo kwan ww hujawahi kupiga picha gari? Kama umewahi ingetokea gari hiyohiyo ipate ajari huwezi kuonesha hizo picha?? Take it easy buddy..
 
Ni mtazamo tuu, inategemea wewe unalichukulia vipi hilo tukio. Myself siwezi from nowhere nikaanza kupiga picha basi lililopaki, angalia zile picha zilizopigwa zikapostiwa humu kwenye ile thread nyingine yaan ukiziangalia unajua kabisa aliyepiga alikuwa na strong reason ya kufanya vile sio huyu aliyepiga picha coaster iliyopaki.
 
Back
Top Bottom