Somo la maadili shuleni laja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo la maadili shuleni laja

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by sir.JAPHET, Sep 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Jumanne, Septemba 18, 2012 05:42 Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

  SERIKALI iko katika mikakati ya kuandaa mitaala kwa ajili ya somo la maadili, ili lianze kufundishwa kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu kwa lengo la kukabiliana na ukiukwaji wa maadili.

  Hayo yalisemwa jana na Naibu Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus, alipokuwa akizindua mradi wa uhamasishaji, uwajibikaji na uadilifu ulioanzishwa na Taasisi ya Save the Society.

  “Tatizo la ukiukwaji wa maadili linaanzia ngazi ya familia hadi taifa, si Serikali peke yake yenye jukumu la kukuza maadili, tunahitaji wadau wengine washiriki kukabiliana na tatizo hilo.

  “Serikali baada ya kuona tatizo hilo linaendelea kuwa kubwa siku hadi siku, imeandaa mikakati ambayo iko katika hatua za kati ya kuhakikisha somo la maadili linafundishwa kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu,” alisema.

  Alisema mikakati hiyo inashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambapo kwa pamoja wanaandaa mitaala ya kufundishia somo hilo, lakini haijajulikana litaanza kufundishwa lini.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Frank Soteri, alisema panapokosekana uadilifu na uwajibikaji, rushwa, ufisadi na ubinafsi hutawala na kukwamisha maendeleo.

  “Taasisi kwa kuzingatia nafasi na umuhimu wa uongozi bora na uadilifu katika kukua kwa uchumi wa nchi, tumeamua kuanzisha kampeni hii ambayo itakuwa endelevu kadiri taasisi na taifa letu tunavyoishi.

  “Tunaamini viongozi na watumishi bora wa umma, huandaliwa tangu mwanzo, kwa hiyo taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuchangia kuandaa viongozi watakaoleta mapinduzi chanya ya kiuchumi kwa nchi yetu.
   
 2. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,648
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Watanzania kwa kupenda njia za mkato hatujambo! Shule ya awali na muhimu kuliko zote za maadili ni katika ngazi ya FAMILIA. Kama wazazi, walezi na wanajamii kwa ujumla wao hawata kuwa na maadili na kuwafundisaha watoto wao,yawapasayo kulingana na miiko na taratibu za jamii husika, hayo maadili watakayofundishwa shuleni (maadili artificial)hayatazaa matunda yaliyokusudiwa. Our ealry relationships with parents or caregivers were the chief enviromental contribution to our personality!
   
 3. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Labda maadili ya mavazi, lakini mengine yanatakiwa kuanzia nyumbani, mzazi kama huwezi kumfunza mtoto maadili nyumbani shule ndio watamuweza? labda vyuo kukataza mavazi ya kihuni huni kama kata K, na vijisarawili vinavobana na nguo fupi kwa wanawake, ...hata hivo ni jambo zuri na inafaa liungwe mkono moja kwa moja.
   
 4. M

  Mr.Mpugusa Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni hatua nzuri sana. Walijisahau mno. wakitaka kufanikiwa katika somo hili ni kuwaajili walimu wa Kiroho. Kwani ili mtu awe na maadili lazima awe Imani ya kumtambua Mungu. Pia serikali ipige marufuku mavazi ya ajabu ajabu kuuzwa na kuvaliwa nje ya nyumba. Uniform za kumdharilisha mtoto zipigwe marufuku.
   
Loading...