Somo kwa kina dada

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,290
[h=5]MWANAMKE MPUMBAVU

1.Anamkomoa mmewe

2.Analala mapema kabla ya mmewe

3.Anachelewa kuamka kabla mmewe

4.Mbishi,anahisi kuonewa mda wote

5.Anadhani kumnyima mmewe uny-
Umba ni kumkomoa

6.Mmekaa sebuleni anahadithia tu
Mafanikio za familia za watu
Wakati ye ndo kigezo cha kero.

7.Hataki kuzungumzia mshara wake

8.We unajenga family ye anajenga
Kwao

9.Mkikaa tu anaanza umbea kuponda
Ndugu na majirani

10.Haridhiki(mwanaume unatoa jasho ila ye anakudiscourage wakati Ye akishuka kwenye kochi anakaa
Kwenye jamvi na baadaye anelekea saloon kupiga umbea kuhusu mama joyce kafumaniwa gesti.

11.Nyumbani housegirl hapunziki.

12.Anajali ajira yake hataki kufuatiliwa mambo yake.

13..Anakera sana,siwezi kuacha kazi yangu hata kama anaumwa,kajikata kucha halafu anadai apelekwe Agha Khan au India.
NOTE:akikutana na mwanaume kichwa ngumu anamrudisha kwao ameshazalishwa watoto 3,anaenda kwa mwingine anaongezewa watoto 2,anazinguliwa anapigwa toto lingine mmoja mtaani,unakuta kazaa na kila familia mtaani baadaye anaishi ghetto au kwao.

MWANAMKE MWEREVU.

1.Unaamka yeye kashaamka na kusema "baby amka maji ya kuoga yapo bafuni"(mwanamke adimu sana)

2.Unajiandaa kwenda kazini khaa,nguo zishapigwa pasi(jamani hiyo kazi kafanya saa ngapi?unajikuta unaenda kazini upo kwenye daladala kimoyo moyo unamwambia "I love u honey"

3.Unarudi jioni unakuta anakuvua soksi acha tu hujui hata anazifua saa ngapi maana huwa hujui anazifua saa ngapi?

4.Umejipunzisha kwenye kochi au
Au kitandani mara kakukalia
Mgongoni anakufanyia mesaj
Mgongoni,khaa alijuaje unataka
Ufanyiwe masaj?unaishia kusema
Thanks baby.

5.Kila anachotaka kufanya kujiendeleza anakuambia na unaweza kumpa mtaji mana ni mkweli(ni baraka kwenye familia)

6.Anapenda ndugu zako(siyo mama mkwe akija anasimamisha pua juu kama kitimoto)

7.Anakupa moyo kwenye wakati mgumu,mf,umefukuzwa kazi anakushauri (baby hayo ni maisha tu,usijali utafanikiwa kama vipi tusimamie ule mradi wangu mpaka uajiriwe)khaa jamani yupo kama huyu fb?upareni?uchagani?usukumani je?

8.Ukirudi nyumbani unakuta anamfundisha mtoto wako maadili ya kimungu(wow heri tuzae tu wa pili)

9.Anakufariji.(Baby usiogope ni mapito ya dunia,jikaze mme wangu,nipo upande wako),hehhehe hata ukinuna unabembelezwa.

10.Mwenye kushukuru na suprises,hawezi kukusahau,(baby hii zawadi kwa ajili yako,umenisaidia sana mme wangu,you changed my life,""baby leo birthday yako,khaa unaona keki mezani"),kuna mke kama huyo?
11.Ana uhakika mimba yako ("baby nina suprise,kumbe mwezi uliopita ulinipa toto,nina mimba yako(siyo ooh khhaaa tumefanya mapenzi juzi tu umenipa dragon mwingine)

NB.Mwanamke kama huyu ni blessing,kila jioni unaona toto zako
zimekaa kwenye kochi yaani vitoto vizuri miguu mifupi hata vikikaa kwenye kochi miguu hazifiki kwenye sakafu vinaangalia cartoons.
Hehehe mtazamo tu najua mmewaza sana[/h]
 
Ngoja waje,andaa kabisa kofia ya kuzuia mawe.
"
Watakuja na uhoji kuhusu mwanaume,utadhani mwanaume akiwa wa hovyo itamuondoa mwanamke kwenye hatia.
"
Hawachoki kujilinganisha na mwanaume,hawajui wanadhihirisha udhaifu.
"
Jamani msinielwe vibaya,sijahalalisha makosa ya wanaume!
 
kwa werevu huo lazima mwanaume na yeye atapiga saluti na yeye atakuheshimu tu
 
Kweli wanawake wana majukumu, hayo ni yale yanayoandikika, bado yale yasiyoandikika
 
I was privileged to know and have one mwerevu woman. RIP Amie....
 
hajazaliwa bado hao!
siku hizi wanataka haki sawa ili upunguze uanaume wako mkutane kati ila wakati huo huo wanataka mtimize wajibu wenu kama wanaume wa enzi za ujima
 
What's wrong with me sleeping earlier than him? Mbona kama mateso hayo. lol!
 
nikianza na wanawake wapumbavu,
hapo namba mbili, ina maana mume akirudi saa nane usiku, atike kwenye starehe zake na beer plus vimada mke akae anatumbua mijicho kumsubiri?

namba tatu, mke kakesha hadi saa nane tisa kumdubiria mume arudi, inategemea alale aamke saa kumi na nusu kuandalia maji mume? na huyo mume na joto lote hili anaoga maji ya moto ana agenda gani na sperm zake?(sayansi ya uswazi hii, staki maswali)

No 4; Mke akionewa awe mtiifu kama kondoo???? Akihoji anakuwa mbishi???

No 6; mume alotegesha misikio kusikiliza umbea wa mkewe yeye sio mmbea? Halafu kwa nini mume usichukulie mafanikio ya wengine kama changamoto, mkapanga mipango mkakati na mkeo ya kujikwamua?

No 7; je mume anazungumzia mshahara wake? Je mume na mke wanaketi kuzungumzia kipato? It seems kama familia ya namna hiyo swala si mke mpumbavu bali wanandoa wapumbavu, wabinafsi na wasiokuwa na mawasiliano ndani...


No 10; perfomance hafifu nalo ni swala la mke???????? Yeye ndo mwenye dushelele?

No 12&13; mke asijali ajira yake? Kweli?????

Hizo ulizoziweka kama mke mwenye hekima, sio kuwa ni mke mwenye hekima bali nyumba yenye mawasiliano ndani..........

Ila ndoa ni vile muijengavyo......na hao wake zenu mnakumbuka kuwavua hereni na pochi? Au mnategesha tu miguu mvuliwe soksi? Wajanja wakimcare mkeo msilie.....

Ndoa/mahusiano ni nipe nikupe....mkiwa watu wa kupokea tu bila kutoa itakula kwenu......

Sikukuu njema

 
andazi la kuchoma siafikiani na wewe kabisa mwanamke sio mtumwa wako ! utamkuta mtu anasema mi nataka kuoa kazi ya kufua,kuosha vyombo imenishosha khaa sa mkeo housegirl?
 
Last edited by a moderator:
hahahaaa... dozi nzito kawapa huyu jamaaa....

hakuna dozi hapo......

Mshahara wa mke anataka kuujua, wakati huo huo analalamika mke kujali kazi zaidi??????? Anajiparaganya.......

Ndo maana mnapotafuta wenza mnapaswa kuwa makini vijana....kuna wanaume wengine hovyo heri ufuge bata utakula nyama, na kuna wanawake hovyo bora ufuge kuku utafaidi mayai...... Ukibugi kuchagua hayo yatakukuta......

Na ndoa imara msingi huanza kujengwa toka u-bf na ugf.......

So far naona kazungumzia ndoa zenye mushkeli...... Na ndoa ambazo mume ni mungu mtu......... Plus ndoa za uswazini kutwa kushinda vibarazani....... Ndoa mabazo wanaume kutwa kurudi usiku ilhali hawezi kumtosheleza mkewe na anatarajia apate huduma za kifalme, ndoa za mtwana na mjakazi..... Ndo za mke kushinda na mashosti (sijui ndo kupunguza stress za kutofikishwa)

Na si ndo za waliokomaa, wanaojua wajibu wao kama wanandoa, na wanandoa daily wanabuni njia za kufurahishana na kuliwazana, wanaoheshimiana na ambazo kila mmoja anajua wajibu wake kwa mwenzie, kila mmoja anataka kuwa karibu na mwenzie.............
 

wote wazaman tu ninyi,na nnawaonea huruma wake zenu
 

wafikishie ujumbe hao,
nione malkia nkuone mfalme sio mie nkuone mfalme we unione kijakazi!! hiyo haipo hata uoe std 7
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…