Wanajidanganya tu! Nafasi ambayo ameipata huyu MAMA ningeipata mimi! Hakika ningejiandikia na mimi kahistoria kangu kazuri, ka kuja kukumbukwa vizazi na vizazi!
Ningeangalia tu hitaji kuu la Watanzania walio wengi kwa sasa ni nini? Kujenga uchumi ambao ulishajengwa tangu miaka ya 1960's, au Katiba Mpya ambayo itarejesha matumaini mapya kwa Watanzania walio wengi?
Baada ya hapo, naamini Watanzania wangenikumbuka milele! Ningeweka mifumo ya haki na usawa kwa Watanzania wote (ingawa natambua fika watu kama akina mwigulu na ubinafsi wao wasingekubali), na ningeimarisha uzalendo wa kweli na kwa vitendo!
MAMA, bado hujachelewa! Do something!! Unadhani ukiwapatia Watanzania Katiba Mpya, hayo Makongamano mnayo yapiga marufuku kupitia policcm, yatatokea wapi?