Somo kuhusu WhatsApp

quantumania

Senior Member
Joined
Dec 23, 2015
Posts
117
Reaction score
367
*WAPENDWA WOTE*

Leo nitawaletea somo la namna ya kupangilia fonts za maandishi yako katika Whatsapp
Kina wakati unataka kuonyesha Kichwa cha habari ama msisitizo kwa ku-bold ama ku-highlight kipengele katika sentensi yako

Fuata njia hizi;
Ku-bold:
Weka alama ya nyota au arsterisks kama ionekanavyo kwenye mabano (*) kila mwanzo na mwisho wa neno/ maneno unayotaka kuyakuza
Kwa mfano;

*Tukiweka kando itikadi zetu*

Vile vile ukitaka kufanya herufi ziwe za mlalo au italic kwa kingereza inakubidi uweke alama ya underscore kama ionekanavyo ndani ya mabano(_) mwanzo na mwisho wa neno/ maneno uliyokusudia
Kwa mfano

_Hakika tutasonga mbele_

Na iwapo utataka ku-strikethrough (nimekosa neno mbadala sahihi la kiswahili)
Basi yakupasa kabla na baada ya neno/ maneno uliyokusudia uanze na kialama kiitwacho "tilde" chenye muinekano huu ndani ya mabano (~)

Kwa mfano

~Vinginevyo maendeleo na demokrasia kwetu itakuwa ndoto za mchana~

Nakutakia majaribio na uandishi mpya.....

***"******"""""****""""***

*MAY THE ALMIGHTY GOD GUIDE AND PROTECT ALL OF US, LOVE YOU ALL*.....

_Best regards_
 
Hiyo mbna ijuwa iyo sema kwenye whatsapp tu ndio inakubali kufanya ivyo
 
Je huu mfumo nitaweza kutumia kwenye Gbwhatsapp?
 

Umetisha sana mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…