Sometimes namuonea huruma sana Zitto Kabwe

Sometimes namuonea huruma sana Zitto Kabwe

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,042
Reaction score
134,330
16606_10203755676268866_6217485468627324127_n.jpg

Rudisha kumbukumbu nyuma mpaka kipindi cha Saga la Buzwagi, Zitto akatimuliwa bungeni, nchi ikazizima kwa ajili yake, ''Baba yake'' Dr.Slaa akamtia moyo kijana akamwambia tunaenda kuishitaki CCM kwa watanzania juu ya huu ufisadi. Zitto akashika hatamu, akawa mtu muhimu mbunge wa kitaifa. Akawa mwenyekiti wa kamati nyeti sana, akalipua ufisadi, chama kikamwamini zaidi kikampa uwaziri kivuli Mambo ya Fedha.........................................................................Zitto akashika hatamu mitandaoni, akawa mwana JF, ikiletwa mada ya Zitto humu page si chini ya 20. Hata mimi nikawa CHADEMA aliyevutiwa na Zitto. Na wengi tu humu tuliipenda CHADEMA because of Zitto

Hali ya Sasa
Hali ya sasa inatia simanzi sana, japo hatua zilizochukuliwa na Chama naziunga mkono mia. Lakini namuonea huruma sana. Watu hawamuamini tena, amebaki Zitto wa facebook na twita. Sio yule tena wa kuitisha press conference akiwa na Dr.Slaa pembeni. Hata anapoibua ufisadi facebook/twita hakuna wa kumuunga mkono, watu wanamzodoa tu.Zitto amekuwa mtu wa kuzodolewa wakati alikuwa role model wa vijana katika siasa? Jamiiforums ndio usiseme,
shukrani kwa Mods kwa kuficha threads zinazomnanga Zitto.
Kibaya zaidi haheshimiwi tena,wanaPAC hawamuheshimu tena chair wao.Kuna tetesi zinaenea kwny duru kuwa Zito amekula kichapo katika kugombea demu huko Malaysia.habari kamili zitawajia
My Take: Zitto ni case study ya Vijana wanasiasa
 
...disposable zikitumika unatupa mbali na watoto zinaweza kugeuka sumu,usiogope simba kula swala,raha ya swala ni kuliwa na simba na anakushangaa ukimuhurumia...
 
Hilo ndilo tatizo la wanasiasa walio wengi hapa Tanzania na Africa kwa ujumla _U_S_A_L_I_T_I. WANASIIASA WOTE NI WASALITI NA NI WANAFIKI WAKUBWA WOTE WANAOJIFANYA WANATETEA WANYONGE SUBIRI WASHIKE HATAMU NDIO MTAWAJUA. SIWAAMIN CCM WALA SIWAAMIN CHADEMA NA SITAHANGAIKA NA CHAMA CHOCHOTE BALI NTAUNGA MKONO MAPINDUZI YOYOTE YA KIJESHI AU YA KUINGIA MSITUN IWE KIJESHI AU KIKUNDI CHOCHOTE CHA WAASI
 
Hata mie namuonea huruma sana zitto facebook alikamata followers wengi kwenye page yake lakini akitoa habari yeyote ya ufisadi anapata comments mbili au tatu sometimes anakosa comments kabisa mtu wa followers zaidi ya 30,000 inasikitisha sana.
 
Hii ni kama thread ya tatu ama NNE....ulizoanzisha kuhusiana na Zitto...yaonekana mahaba yako kwake bado yanashamiri
 
Zitto maadamu hakutaka kufuata ushauri wangu,umaarufu wake utazidi kuporomoka siku hadi siku,mambo yatamuendea magumu zaidi pale atakapokosa kila kitu ifikapo 2015na akijidanganya kuamia chama chochote ndio atapotea kabisa kwenye jukwaa la siasa
 
Zitto yuko clouds fm anongea unafiki mtupu.
Tamaa mbaya sana huyu kijana anapenda sana fedha zinamponza.

ZZk ameji aribia kabisa.
 
Hii ni kama thread ya tatu ama NNE....ulizoanzisha kuhusiana na Zitto...yaonekana mahaba yako kwake bado yanashamiri

Kwa kuwa ni politician aliyenifanya niipende Chadema. Sina budi . Sababu nyingine ni Mods kufuta threadz zangu juu ya Zitto , sasa kiu haikatiki
 
Unamwonea huruma? Basi huyajui mambo mengi. Siku hizi siasa biashara ni mmoja wapo wa njia za mafanikio. Wakuonewa huruma ni wananchi wanatumika vilivyo kwa ajili ya wachache. Huwezi tibu malaria sugu kwa panadol. Usimwonee huruma mwanasiasa yeyote.
 
Hata mie namuonea huruma sana zitto facebook alikamata followers wengi kwenye page yake lakini akitoa habari yeyote ya ufisadi anapata comments mbili au tatu sometimes anakosa comments kabisa mtu wa followers zaidi ya 30,000 inasikitisha sana.
Mkuu hizi hapa habari zake na comments mbili tatu aizopata, zingine hakuna kabisa utadhani ametupia ''just now''



 
Mkuu hizi hapa habari zake na comments mbili tatu aizopata, zingine hakuna kabisa utadhani ametupia ''just now''




acha tu ni shida.
 
Back
Top Bottom