Someni hii mtapata ujasiri na mafanikio. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Someni hii mtapata ujasiri na mafanikio.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tasia I, Apr 8, 2011.

 1. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Siri za kufanikiwa chochote unachotaka


  Thursday, 07 April 2011 08:17
  Na Dismas Lyassa
  KWANINI katika maisha kuna watu wengine hawafanikiwa na wengine wanafanikiwa? Ni swali ambalo limekuwa likiumiza vichwa vya wengi.

  Wapo ambao wanawianisha mafanikio ya mtu na elimu, lakini hiyo haina ukweli sana, japo kuna watu ambao mafanikio yao yametokana na elimu waliyonayo. Kusoma au kutosoma kwa maana ya kupata elimu ya kutosha siyo ile ya kufuta ujinga haina maana kwamba mtu atakuwa na maisha mazuri au atafanikiwa katika maisha au laa.

  Tunasisitiza kuwa elimu ni muhimu sana katika masiaha ya sasa. Lakini hiyo unaitumia vipi hilo ndilo suala au jambo la msingi sana ambalo wengi wanashindwa kulitambua. Kutokana na kushindwa kujua hilo wengi huishia kutoa wasifu wa viwango vya elimu.

  Aah! Unajua mimi nimesoma na Rais wenu… alikuwa kilaza sana, mara oooh usinione hivi nimesoma sana, nimetembelea nchi nyingi sana hapa duniani au aaah… nimeonana na wakubwa wengi katika dunia hii na mengine kama hayo.

  Kila mtu anapenda kufanikiwa, anapenda maisha mazuri, lakini si wengi wanatimiza azma hiyo. Kwanini? Kuna sababu nyingi, lakini kubwa ni woga wa kuthubutu kujaribu kufanya jambo fulani.

  Je wewe una shauku ya kufanya nini? Yawezekana unataka kuwa na biashara kubwa, unataka kujiajiri na hata uajiri wengine, basi acha woga.

  Wengi wanaishi katika hofu na kuamini kuwa maisha bofra yako katika ajira ya mshahara pekee. Siyo kweli. Thubutu utaona jinsi unavyoweza kupiga hatua kubwa na tena ya ajabu. Usichelewe.

  Kushindwa kuthubutu kunaashiri mwisho mbaya wa maisha yako hapa duniani na hasa kama hutakuwa na mradi wowote wa kukuongezea kipato zaidi ya mshahara wako.

  Watafiti wengi duniani wanabainisha kuwa yeyote ambaye anaishi kwa kutegemea ajira pekee, lazima atakuwa na hali ngumu, kwani baada kustaafu atapata mafao yake na kukaa nyumbani akicheza na wajukuu au kukaa tu tofauti na aliyekuwa na mradi baada ya kustaafu ataendelea na biashara yake na kipata hakitabadilika sana.

  Msingi wa kuwa na mafanikio kwa chochote unachotaka ni kuthubutu, ni lazima kutafakari namna ya kujiajiri. Ni lazima ujiulize kama wengine wameweza kuniajiri, kwanini siku moja na wewe usiajiri watu wa kukufanyia kazi? Kwani wao ni akina nani hadi waweze na wewe ushindwe? Tafakari, chukua hatua.

  Ukweli ni kwamba msingi wa mafanikio yetu kwa asilimia 99 unatokana na kufanya kazi kwa bidii, na asilimia 1 ni bahati. Ndio kusema usitegemee kufanikiwa kwa misingi ya bahati, fanyakazi kwa bidii na umakini.

  Je kuwa na fedha ndio msingi wa mafanikio? Hapana, huo ni uongo. Fedha, si ufunguo wa mafanikio, ingawa ni kigezo muhimu sana katika uanzishwaji wa biashara na mambo mengine.

  Hapa tunajifunza kitu kingine kwamba kuzaliwa kwenye familia maskini au tajiri, haina maana kwamba utakuwa tajiri au maskini. Kuna watu wamerithi fedha au mali lukuki lakini wakaishia kuwa masikini wa kutupwa kwa kjukosa maarifa ya kuzisimamia.

  Ni ujinga mkubwa kwa mtu hasa kijana kuringia mali za wazazi wake, badala yake anapaswa kujifunza namna ya kutafuta zake.

  Je kuwa na uzoefu na jambo fulani ndio huleta mafanikio? Hapana. Lakini pia ni kweli uzoefu unaweza kumfanya mtu kufanya kazi kwa mafanikiotofauti na asiyekuwa na uzoefu.

  Uzoefu ni siagi kwenye mkate!
  Kufanya kazi kwa bidii ni muhimu kwa mafanikio? Jibu ni NDIYO. Hakuna mafanikio pasipo kufanya kazi kwa bidii.

  Mafanikio yoyote ni matokeo ya moja kwa moja ya masuala mengi lakini lililo kubwa ni ile ya kufanya kazi kwa bidii, umakini na kutumia fedha kwa uangalifu wakati wote.

  Pamoja na kufanyakazi kwa bidii, kazi lazima ifanywe kwa kushirikiana na wengine kwani tunaishi kwa kutegemeana, usimdharau mtu kutokana na hali yake unaweza kupata kitu ambacho wewe huna.

  Kila mara jibidiishe na kupata elimu mpya. Elimu haina mwisho. Tafuta elimu wakati wote itasaidia kukuweka sawa katika kuendesha shughuli zako kisasa na kwa mafanikio zaidi.

  Ili kufanikiwa ni lazima uwe na kiu ya kujifunza, uwe na kiu ya kusoma vitabu vinavyohusiana na ujasiriamali na siri za mafanikio.
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mwenye sikio ameshakusikia!!!

  na mwenye macho amekwisha kuona!!!!

  Nimeipenda, ngoja nivute msuli zaidi!!
   
 3. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  susy,
  tatizo watu hua hawasomi hizi thread ndefu.wanasahau kua kinachofanya kua ndefu ni content zake.
   
Loading...