.... Jamani, hivi mtu akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!
Nimewasoma wote, ni kweli mnayosema. Ila mimi naona hata kama ni kujikwamua kimaisha amekuja kwa kasi sana. Kwa tamaduni zetu za kiafrika inakuwa tabu sana mwanamke kumsumbua mwanaume kihivyo, ila kwa siku hizi mambo yamebadilika sana.
Hivi karibuni nilisafiri kutoka Dar kwenda mikoa ya kusini. Ndani ya gari nikakuta nimekaa siti moja na mdada mmoja mdogo, umri waweza kuwa kati ya miaka 16-18. Kawaida yangu huwa siyo mzungumzaji sana, labda mpaka mtu mwingine aanzishe mada. Kwa mvao na mwonekano wake alikuwa amependeza vizuri tuu, lakini ikaonekana hakuwa vizuri kiuchumi. Alikuwa ananunua vitu rahisi sana, hata maji alikuwa anauliza kama kuna ya 300.
Tukafika sehemu tukashuka kwa mapumziko ya dk kumi kununua mahitaji na kuchimba dawa. Nikafanya manunuzi ya chakula na vinywaji mara mbili ili nimgawie na yeye. Akafurahi sana na tukajaribu kufahamiana. Nikataka kujua anafanya nini. Akaniambia kuwa aliacha shule akiwa form 2 mwaka jana kwa sababu za kiuchumi, ndo akawa ameenda Dar kutafuta kazi za kuuza duka.
Nikampa pole kwa maswahibu yaliyomkuta. Tulivyokaribia kushuka akaniuliza kuwa nafanya kazi wapi? nikamweleza, akaniomba namba. Tukaachana huku akinishukuru sana kwa msaada wa chakula njiani. Ikawa kila siku usiku ananibip ili nimpigie. kimsingi hakuna hata mada serious za kuzungumza, basi tu kujuliana hali. Baadaye akaanza kunitumia msg za kuniita mpenzi, baby, etc. Akaanza kuniambia ametokea kunipenda, na anataka nimtumie hela na vitu vingine kibao. Jamani, hivi mtu akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!
....Kosa nililoliona haraka haraka ni kutoa namba ya simu kwa huyo dada mara baada ya kumnunulia chakula. Kwa kawaida, hata kama nia yako ya kumsaidia ni njema, kitendo cha kutoa namba ya simu ni kuruhusu MAWASILIANO zaidi baada ya kuachana hapo. Na mimi sishangai kabisa yeye kuendelea kukutafuta maana ndiyo kazi halisi ya simu!.....
Hivi karibuni nilisafiri
kutoka Dar kwenda mikoa ya kusini. Ndani ya gari nikakuta nimekaa siti
moja na mdada mmoja mdogo, umri waweza kuwa kati ya miaka 16-18. Kawaida
yangu huwa siyo mzungumzaji sana, labda mpaka mtu mwingine aanzishe
mada. Kwa mvao na mwonekano wake alikuwa amependeza vizuri tuu, lakini
ikaonekana hakuwa vizuri kiuchumi. Alikuwa ananunua vitu rahisi sana,
hata maji alikuwa anauliza kama kuna ya 300.
Tukafika sehemu tukashuka kwa mapumziko ya dk kumi kununua mahitaji
na kuchimba dawa. Nikafanya manunuzi ya chakula na vinywaji mara mbili
ili nimgawie na yeye. Akafurahi sana na tukajaribu kufahamiana. Nikataka
kujua anafanya nini. Akaniambia kuwa aliacha shule akiwa form 2 mwaka
jana kwa sababu za kiuchumi, ndo akawa ameenda Dar kutafuta kazi za
kuuza duka.
Nikampa pole kwa maswahibu yaliyomkuta. Tulivyokaribia kushuka
akaniuliza kuwa nafanya kazi wapi? nikamweleza, akaniomba namba.
Tukaachana huku akinishukuru sana kwa msaada wa chakula njiani. Ikawa
kila siku usiku ananibip ili nimpigie. kimsingi hakuna hata mada serious
za kuzungumza, basi tu kujuliana hali. Baadaye akaanza kunitumia msg za
kuniita mpenzi, baby, etc. Akaanza kuniambia ametokea kunipenda, na
anataka nimtumie hela na vitu vingine kibao. Jamani, hivi mtu
akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!
Hebu shangaa na wewe bro ..yaani utoe namba ya simu mwenyewe..halaf uanze kupigiwa simu malalamiko kibao hadi MMU..aaarghhh...This is not fair bwana..Ulitakiwa uwe nunda in the first place..duh!!
Kuna ubaya gani "kumpenda" mtu anayekusaidia katika matatizo? Labda kama issue ni suala la umri... Jamani, hivi mtu akikusaidia ndo inakuwa automatic gear ya kuwa wapenzi? Mmmh!!!
Halafu namba yenyewe ya simu ameitoa kwa kitoto cha miaka 16-18, imagine! Huyo si mtoto kabisa?! Alitegemea kungea naye nini mtoto kama huyu?
Labda si uzee umeshika kasi tunashindwa kwenda na kasi ya sayansi na teknolojia!!!!
Ni njaa tu ndo inayomsumbua wala sio kwamba we mzuri sana hadi anahitaji kuwa na wewe.