Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,276
Wanajeshi hao kutoka Uganda walikamatwa kwa tuhuma za wizi wa bidhaa za kijeshi ikiwemo mavazi silaha na mafuta.
Mahakama ya kijeshi ya Uganda iliandaa kikao hicho maalum mjini Mogadishu kufuatia shinikizo kutoka kwa serikali ya somalia iliyowakamata.
Kikao hicho ni cha kwanza kabisa kuwahi kuandaliwa nje ya Uganda.
Wanajeshi wa Uganda waliingia Somalia yapata miaka 9 iliyopita.
Kesi yao inasikilizwa na maafisa 7 katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo.
Mwanajeshi mmoja tayari amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kukiri makosa yake na atatumikia kifungo chake nchini Somalia.
Uganda ndio taifa liliochangia idadi kubwa zaidi ya wanajeshi nchini Somalia chini ya mwavuli wa Amisom.
Chanzo :BBC news