Somalia wafanya uchaguzi wa Urais leo; Huku milipuko ikisikika

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_94014270_doorashadasoomalaiya.jpg

Milipuko imesikika katika mji Mkuu wa Mogadishu nchini Somalia usiku wa kuamkia leo wabunge wanapotarajiwa kukutana kumchagua rais mpya.

Kumekuwa na taarifa kuwa mizinga imelipuliwa karibu na uwanja wa ndege ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika, huku wakazi wa eneo la Waberi iliyoko Kusini Magharibi mwa Mogadishu pia wakithibitisha kusikia milipuko.

Kufikia sasa hakuna maafa au majeruhi walioripotiwa ingawa hali ya wasiwasi imetanda Mogadishu.

Babarabara zote zimefungwa. Uwanja wa ndege hakuendeki. Na hata wakazi wengine hawawezi kuvuka kutoka barabara hii hadi ile.

Mahali pa kufanyia uchaguzi pamehamishwa, kutoka Chuo cha Polisi hadi Uwanja wa ndege wa Mogadishu wenye ulinzi mkali. Sababu ya kuongezeka kwa vitisho vya usalama na rushwa .

Hivi leo ndege hazitaruhusiwa kutua au kupaa kutokea uwanja huu, kwa kuwa ni siku ya kupiga kura.

_94219657_mogadishu.jpg

Mfumo wa uchaguzi nchini Somalia umeharibika kama ilivyo miundombinu yake.

Haina daftari la wapiga kura. Wabunge mia tatu na ishirini na tisa ndio watakaomchagua Rais ajaye.

Lakini sasa tuhuma za rushwa zinatishia kuvuruga mchakato mzima. Kuna tuhuma nzito kuwa wabunge wengi wamelipwa mamilioni ya dola kushawishi upiga-kura wao.

_94219653_somali.jpg

Wanawake wengi zaidi watashiriki kupiga kura wakati huu, hivyo kufanya asilimia ishirini na sita ya kura zote za bunge.

Ingawa wanawake wawili waliotangaza nia ya kuwania Urais akiwemo Fatuma Dayyib aliyetangazwa sana, walijitoa.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Back
Top Bottom