Uliye mrejea umemuelewa vibaya,kuna wengine wanaposema "Mungu" huwa wanamkusudia Allah,na kufanya hivi kiitikadi ni makosa,na kadhalika wapo wanaosema "Mwenyezi Mungu" wakimkusudia Allah nao pia wanafanya makosa,sababu majina ya Allah ni maalumu na ni yake ambayo amejiita kwayo mwenyewe au aliyoitwa na mtume wake,hii ni kwa mujibu wa Itikadi ya Uislamu.
Kwahiyo Waswahili wanatumia majina hayo pia hasa jina "Mungu" kuwasudia pia miungu wao,sababu Mungu lina wingi na Mwenyezi Mungu halina wingi.
Kiuhalisia ni vitu viwili tofauti,ila kimakusudio wanamkusudia mmoja na kufanya hivyo ni makosa.