Soma uone ilivyo bora kubaki njia kuu kuliko kuwa na kamchepuko

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,893
Soma uone ilivyo bora kubaki njia kuu kuliko kuwa na kamchepuko

BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Arusha kwenye mkutano fanya mipango yote.

SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Arusha kwenye mkutano.

MUME (anampigia nyumba ndogo): Mambo safi, wife anaenda kikazi Arusha jitayarishe tujirushe.

SMALL HOUSE (anamwambia mwanafunzi wake wa twisheni): wiki hii nina kazi fulani hakuna twishen mpaka wiki ijayo.

MWANAFUNZI (anampigia simu babu yake (BOSI)): Babu hakuna twisheni wiki hii nakuja kwako.

BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Arusha mjukuu wangu atanitembelea.

SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Arusha.

MUME: Aise mpenzi jamaa haendi mipango imeharibika.

SMALL HOUSE (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida.

MWANAFUNZI: Babu twisheni iko, nakuja wiki ijayo.

BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Arusha iko palepale.
 
Ha ha haha hahaa...Nimecheka sana...Ila kuna ukweli kuhusu hiyo Chain......Bora kubaki njia kuu...SERVICE ROAD Haifai
 
Hahahaha nimependa hii.......hapana chezea michepuko!!
 
Michepuko ni deal sometimes hasa kwa wanandoa. Ina punguza sana stress, tatizo sasa ikijulikana kwa umpendaye, hapo ndo balaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom