John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 713
- 1,241
Askofu Mokiwa akemea viongozi wanaosaka utajiri kwa mbinu ya uchafu
Na Michael Uledi, Dodoma
ASKOFU wa Kanisa la Kianglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa, amewakemea viongozi wa serikali wanaosaka utajiri na heshima kwa mbinu chafu huku wananchi waliowapa dhamana ya kuongoza wakitopea katika umaskini.
Askofu Mokiwa alisema hayo jana alipokuwa akihuburi katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na Kasisi Jacob Kahemele ambaye amepewa daraja la upadri baada ya kuwa shemasi kwa miaka minane.
?Katika nchi hii iliyojaa watu maskini wanaoteseka, tunao viongozi waliopewa dhamana na hawa maskini ambao ghafla wamegeuka kuwa matajiri wa kutisha, tunao watu waliotumia mbinu chafu kuwa viongozi na wengine wanaendelea kutumia mbinu hizo kusaka nafasi za heshima ya kuwa viongozi,? alisema Askofu Mokiwa.
Alisema taifa kwa sasa linakabiliwa na viongozi wanaofuja mali ya umma katika maisha ya kifahari na kwamba tabaka kati ya maskini na matajiri limekuwa likiongezeka kwa kiasi kikubwa nchini hivi sasa.
"Mmepata wapi fedha na mali nyingi hizi? Viongozi ndiyo kabisa hamuwezi kuepuka kujibu swali hili. Waambieni wazi wazi Watanzania mlikopata fedha na mali mlizonazo na muache viini macho vya kudanganya watu kama vile hamna mali hizo, kwa sababu hamuishi hewani, mnakaa na Watanzania hawa na wanaowaona, hivyo waambieni mlikopata fedha hizo kama ni halali ili wasiwe na wasiwasi,? alisema Askofu Mokiwa.
Alisema Watanzania wanaponung'unika, wanayo haki ya kufanya hivyo kwani wanalipa kodi na kwamba wamewekwa na Mungu katika nchi yenye rasilimali, hivyo, wana haki kufaidi matunda ya rasilimali hizo na akahoji iweje leo wafaidike wachache tu.
?Tena vibaya zaidi ikiwa wachache hao ni watu waliopewa dhamana na wananchi hawa hawa. Ni laana kubwa kama watu wachache waliopewa dhamana yetu wakijinufaisha peke yao kwa kushirikiana na wageni, wakiwaacha kaka na dada zao wa kuzaliwa
wakiteseka na kufa na matatizo ambayo yangeweza kuepushwa kama kungekuwapo na usawa katika kugawana rasilimali zilizopo nchini mwetu. Ole wenu,? alionya Askofu Mokiwa.
Alihoji iweje kuna sauti kubwa ya kelele juu ya rushwa na kisha hakuna lolote linalotokea angalau kuonyesha dalili kuwa hali itabadilika na pia iweje rushwa imegeuka kuwa kama upepo usio na rangi kwa kuwa inatajwa kila mahali na wakati wote, lakini haishikiki au wanaoitishia nao ni wala rushwa.
"Kama siyo wao ni vipofu hawaoni? Au viziwi hawasikii?Labda ni ndoto tu hakuna ufisadi wala rushwa? Kuna vichaa tu wanajitokeza na kupiga kelele za mambo
yasiyokuwapo, wazimu umiengia Tanzania? alihoji Askofu Mokiwa na kuongeza:
"Ukiacha viongozi, watendaji katika ngazi mbalimbali serikalini na hata katika sekta binafsi ni kama kichaka kikavu kimeingiwa moto, homa wanazoamka nazo Watanzania wa leo ni kutaka kutafuta utajiri kwa njia yoyote".
Akizungumza katika hafla ya chakula kilichoandaliwa na Mchungaji Kahemele kwa ajili ya watu wanaoishi katika mazingira magumu, Askofu Mokiwa alisema sehemu kubwa ya maskini waliopo nchini wametengenezwa na matajiri wanaojilimbikizia mali kwa njia za wizi.
Aliwataka matajiri kujirudi na kurejesha utajiri walioupata kwa njia zisizo halali na kisha kuwasaidia maskini.
?Wanaoiba madini tunawaona, lakini pia Watanzania tuache kabisa uvivu na hata uvivu wa kufikiri, nashauri kila mtu aachane na uvivu,? alisema Askofu Mokiwa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mchungaji Kahemele alitoa changamoto kwa watu walio na uwezo wa kupata mavazi na chakula kutambua kuwa wakati wakiwa na neema hizo baadhi ya watu wanaishi katika mazingira magumu yasiyo na uhakika wa chakula na mavazi hivyo kuishi kwa huzuni na hofu.
Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la Roho Mtakatifu Dodoma ambako mbali ya chakula kilicholiwa kwa pamoja na waumini mbalimbali, ikiwa ni pamoja na watoto na watu wanaoishi katika mazingira magumu.
Katika hafla hiyo nguo na zawadi mbalimbali zilichangwa na marafiki wa Mchungaji Kahemele ambazo ziligawiwa kwa watu wenye uhitaji mkubwa.
Source: Mwananchi