Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
642
[h=3]Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.[/h][h=3]“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa na kitu moyoni. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.[/h][h=3]Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilikwishahamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu, nilimtusi vibaya kwa ajili ya Jane![/h][h=3]Huku moyo wangu nikijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.[/h][h=3]Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa uchungu na sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu na kuongeza kiburi kwamba mimi ni mshindi.[/h][h=3]Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa miaka mitano na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.[/h][h=3]Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.[/h][h=3]Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.[/h][h=3]Kama kawaida kesho yake nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu, kwani kila tulichokuwa tukiongea na mke wangu hata kutoelewana kidogo lazima nikamweleze malkia wangu. Jane alicheka sanaaaa, aliona ni ujinga mtupu. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Jane tena kwa dharau kubwa mno. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana kwa miaka miwili tangu Jane apate kutambua nampenda na kumthamini kuliko mke wangu. Alitumia kila njia hata madawa akawa anapulizia kitandani nikifika kwakwe nakuta kitanda kimerembwa kwa mapambo mbalimbali na nyumba kunikia marashi kumbe ni madawa, Nikijilaza pale naona kama nimefika mbinguni na nikirudi nyumbani ugomvi, hasira na chuki zinaanzia nje ya geiti hadi kufika ndani ni ngumi na mateke tuu yanatawala.[/h][h=3]Mke wangu alikuwa mzuri kuliko Jane, mwaminifu, mwenye upendo na uvumilivu mkubwa. Nilianza kutimiza masharti ya kuachana na mke wangu kwa mbeba; kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.[/h][h=3]Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda kumchukua Jane nimpeleke ofisini kwake. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi? Nae analia na Mungu kila wakati?[/h][h=3]Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami, kanizalia kijana na tumeishi kwa miaka kumi sasa. [/h][h=3]Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Nilijitahidi kutomwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi, na akili yangu ikaanza kufunguka.[/h][h=3]Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma moyoni... mke wangu ana uchungu mwingi na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo wa ajabu. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka na kunikosesha amani sana.[/h][h=3]Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini bila kumpitia Jane…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango, Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapanda ngazi. Jane sikumfuata nyumbani kwake nimpeleke kazini ila nilimwona asubuhi na mapema, akifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani ila wewe ndio umekuwa sumu ya ndoa yangu. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’[/h][h=3]Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi? Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.[/h][h=3]Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane nikamsahau mke wangu mpendwa pamoja na mwanetu. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.[/h][h=3]Angalau machoni mwa mwanangu, ndugu, jamaa na marafiki naonekana ni mume mwema….[/h][h=3]Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha wala faraja ya moyo wako. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenu ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao. Yakikufika yaliyonipata utajuta na kutubu sana lakini muda utakuwa umeisha. Maji yakimwagika kuyazoa ni kitendawili![/h][h=3]Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa. [/h][h=3] [/h][h=3][/h]
 
Natamani kila mwenye ndoa na anayetarajia kuipata asome stori yote hiyo maana kuna mengi ya kujifunza hapo. Tatizo ni kwamba shetani mvuruga ndoa atawapa uvivu watu wasisome ili wasijifunze na wazidi kuharibu maisha yao ya ndoa.
 
Ina ujumbe mzuri sana, tatizo binadamu tunasahau mapema na kuishi hapa duniani kama tutaishi milele!!
 
Hadithi nzuri, iweke katika magazeti ya Shigongo, au Mpe Ally Yakuti atengeneze film script
 
Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.

"Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa na kitu moyoni. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.

Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?' Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!' Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilikwishahamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu, nilimtusi vibaya kwa ajili ya Jane!

Huku moyo wangu nikijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa uchungu na sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu na kuongeza kiburi kwamba mimi ni mshindi.

Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa miaka mitano na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.

Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.

Kama kawaida kesho yake nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu, kwani kila tulichokuwa tukiongea na mke wangu hata kutoelewana kidogo lazima nikamweleze malkia wangu. Jane alicheka sanaaaa, aliona ni ujinga mtupu. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima', alisema Jane tena kwa dharau kubwa mno. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana kwa miaka miwili tangu Jane apate kutambua nampenda na kumthamini kuliko mke wangu. Alitumia kila njia hata madawa akawa anapulizia kitandani nikifika kwakwe nakuta kitanda kimerembwa kwa mapambo mbalimbali na nyumba kunikia marashi kumbe ni madawa, Nikijilaza pale naona kama nimefika mbinguni na nikirudi nyumbani ugomvi, hasira na chuki zinaanzia nje ya geiti hadi kufika ndani ni ngumi na mateke tuu yanatawala.

Mke wangu alikuwa mzuri kuliko Jane, mwaminifu, mwenye upendo na uvumilivu mkubwa. Nilianza kutimiza masharti ya kuachana na mke wangu kwa mbeba; kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake'. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda kumchukua Jane nimpeleke ofisini kwake. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi? Nae analia na Mungu kila wakati?

Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami, kanizalia kijana na tumeishi kwa miaka kumi sasa.

Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Nilijitahidi kutomwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi, na akili yangu ikaanza kufunguka.

Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa'. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma moyoni... mke wangu ana uchungu mwingi na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini'. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo wa ajabu. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka na kunikosesha amani sana.

Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini bila kumpitia Jane…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango, Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapanda ngazi. Jane sikumfuata nyumbani kwake nimpeleke kazini ila nilimwona asubuhi na mapema, akifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu'. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?' Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani ila wewe ndio umekuwa sumu ya ndoa yangu. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.'

Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi? Nikatabasamu na kuandika "Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha". Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane nikamsahau mke wangu mpendwa pamoja na mwanetu. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.

Angalau machoni mwa mwanangu, ndugu, jamaa na marafiki naonekana ni mume mwema….

Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha wala faraja ya moyo wako. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenu ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao. Yakikufika yaliyonipata utajuta na kutubu sana lakini muda utakuwa umeisha. Maji yakimwagika kuyazoa ni kitendawili!

Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa.
ki ukweli machozi yamenitoka. funzo zuri kweli.
 
Back
Top Bottom