Soma haya matukio, halafu naomba ushauri

Soma haya matukio, halafu naomba ushauri

Ternado, Pole sana kaka. Hakuna mwanamke wa kuoa hapo na hiyo familia itakuyumbisha hadi ukonde. Achana nae kama aliwahi kwambia sio lazma mtoto awe na baba muachie kwani watoto wameisha kiunon utazaa wengne huyo muachie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uzoefu wa kuishi ktk ndoa zaidi ya 20yrs my friend hapo unakoelekea ktk hayo mahusiano utakuja kuteseka sana ukikubali kwa namna yoyote kumfanya huyo mwanamke kuwa mkeo. Licha ya kukuendesha hata kabla hamjahalalisha mahusiano yenu hata hiyo familia hawana maadili ya kiafrika kumheshimu mkwe wao mtarajiwa kama maelezo uliyotoa niya kweli. Utaendeshwa kama mkokoteni my friend. Mtunze mwanao na mahitaji muhimu kwa mama mtoto lakini sio kama mke. Jambo moja ukae ukitambua akumulikaye mchana usiku hukuunguza. Kazi kwako.
 
Nikisoma napata tafuatayo. Huyo manzi itakuwa kabebeshwa mimba na mtu mwingine, kwako ilikuwa chaka tu la kuzugia.

Baada ya kupata uhakika na huyo mchiz, akagoma kuendeleza hatua zaidi na wewe. Hapo kajirudishwa kwa sababu za kiuchumi tu.

Picha halisi ni mume mwenzio haeleweki na ndie anaye mzuzua, siku Akisomeka tu. Hutomuona tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom