Soma hapa: waraka huu kwa Rais na uwajibikaji wa viongozi kwa Taifa letu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soma hapa: waraka huu kwa Rais na uwajibikaji wa viongozi kwa Taifa letu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Sep 16, 2012.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Mh. Rais Nikusalimu kwa salamu.
  Mh. Rais nitumie njia hii ya maandishi baada ya kutumia njia ya majukwaa na matamko mbalimbali kuikosoa serikali yako na chama chako cha ccm..
  Mh. Rais nimeamua kuandika baada ya leo kusikiliza mjadala mkali sana wa Amani ya nchi yetu ambao ulikuwa unaendeshwa na kituo cha STAR TV leo 16/10/2010 Wazungumzaji wa mjadala huu walikuwa ni Mh. Tundu Lissu Mkurugenzi wa chama changu wa sheria na haki za binadamu na Mbunge wa Singida, Nape nauye katibu wako wa uenezi wa chama chako,pamoja na muwakilishi kutoka chama kingine cha siasa.

  Mh.Rais. baada ya mjadala huwo mkali ambao kama kawaida wa viongozi wa chama Tawala kutumia fursa kama hizo kuhadaa umma, ukanipekea kukumbuka utawala wa awamu ya tatu na awamu hii ya nne.

  Mh.Rais. Kabla ya ujio wa Awamu ya Tatu ya uongozi wa serikali,watu waliaminishwa kupitia ahadi za TANU (1962) haswa ahadi ile ya Tano(UTUMISHI KWA UMMA NA UWAJIBIKAJI) wengi hatukuweza kujua madhara yanayoweza kulikumba taifa kama ahadi(utumishi kwa umma NA HAKI YA MWANANCHI) hii inakiukwa.

  Mh.Rais. Katika awamu ya tatu,madhara yalijithihirisha wazi wazi kwa uamuzi wa viongozi wa serikali ya chama cha mapinduzi(ccm) kuuziana nyumba kwa bei ya kutupa na kukiuka sheria ambazo zilitungwa na serikali hiyo hiyo kuhusu kanuni za uuzaji au ubinafisishaji wa mali na huduma za serikali.Mh. Rais Hatua hiyo sikwamba ilikuwa inakiuka maadili ya chama Tawala chenyewe yaliyomo katika ahadi hiyo ya Tano-chama amabacho ndicho kinachozihodhi Ahadi hizo za Uraia Mwema, lakini Mh Rais. ni uamuzi ambao umekiuka misingi ya utawala bora.

  Mh Rais. kwa kuamua kuuziana mali za serikali bila kuzitangaza kufuatana na kanuni za Zabuni ili kutoa nafasi kwa kila mwananchi kuo nyesha nia yake ya kutaka kuzinunua mali hizo kwa bei anayoimudu, Mh Rais. Serikali ilidhalilisha taifa letu kwa njia zifuatazo>
  (a)Taifa lilinyimwa haki ya kupata mapato makubwa zaidi ambayo yangeliwezesha Taifa kuwasaidia wananchi wengi zaidi kupata nyumba nzuri za kisasa-jambo ambalo tunaelezwa kwamba ndilo hasa lilikuwa lengo la zoezi hili. Mh Rais Tutalifikiaje lengo kwa kuliingizia taifa mapato kidogo tu wakati amabapo tungeliweza kupata zaidi? Wahusika hao mpaka sasa wamechukuliwa hatua gani juu ya kuliingizia taifa hasara?
  (b)kwa kukiuka sheria zetu wenyewe za utangazaji wa zabuni tunapotaka kuuza ama kubinafsisha mali za umma au kununua mali (RADA) Au huduma ilikupata bei nzuri zaidi kwa kuchagua mzabuni amabaye angelinunua mali zetu(NBC) kwa bei ya juu zaidi au anauza mali au huduma zake kwa bei ya chini zaidi, Mh Rais. sielewi Amani ipi tunayoizungumzia ya Mtanzania kuendelea kukaa kimya huku taifa likitafunwa,Amani hiyo ipo kwa viongozi wa chache wanaoneemeka na mali za umma huku Mwananchi wa kawaida akiishi kwa maisha ya Hofu kwakutokujua kesho yake, Mnatoa polisi barabarani kwa wingi kuzuia maandamano ya amani ya CHADEMA na mikutano ya hadhara huku mkishindwa kuweka vizuizi vya kutumia askari kuweka mitengo kwa wala rushwa na kuwakamata,Mh.Rais.vibaka wanachomwa kwa moto ama kupigwa na kuuwawa na wananchi weney hasira kali kwa ugumu wa maisha, huku viongozi wanaoliibia taifa hili kwa kalamu wakiendelea kuitwa mafisadi na kuendelea kuishi bila wasi wasi kana kwamba hamna wa kuwawajibisha.mtawala mzuri anaheshimu sheria zake na kujali misingi sahihi ya uendeshaji wa mambo ya taifa kama walivyokuwa Hayati mwalimu Julius Nyerere,Hayati Abeid Amani Karume na Hayati Sokoine. Tuige Mifano yao ambayo ililijengea Taifa hili heshima kubwa sana ndani na nje ya nchi kwa mfano>
  (i)1978 kulitokea vifo katika Gereza la shinyanga katika hali ya kutatanisha,Hivyo serikali ilibidi iwajibike kwa tukio hilo maana lilitokea mikononi Mwake na mahabusu wale walikuwa wamewekwa humo ndani na serikali. Mh Rais. swali lilikuwa nani awajibike? Rais? Makamu wa Kwanza wa Rais? Makamu wa pili wa Rais na Waziri mkuu au nani?
  Mh Rais Kwa utaratibu mzuri anayewajibika ni yule kiongozi Mwenye Dhamana inayohusiana na tukio hilo maana yeye ndiye aliyekabidhiwa ya siku hadi siku ya kusimamia kazi za wizara au Idara yake kwa niaba ya serikali.
  Mh Rais.katika tukio hilo ilionekanika kwamba Wiazara Tatu ndizo zilihusika, ya kwanza ilikuwa ni wizara ya mambo ya ndani ambayo kiongozi wake alikuwa ni Mzee Alli Hassani Mwinyi. Lakini mshauri mkuu mwingine wa Urais alikuwa ni Waziri aliyekuwa na Dhamana ya kusimamia Usalama wa Taifa;ambaye kwa wakati huwo alikuwa ni Peter Siyovelwa. Wizara ya Tatu ilikuwa ni wizara ya Tawala za Mikoa ambayo iliongozwa na Peter Kisumo. Lakini Tukio lilitokea mkoa wa shinyanga ambako Mkuu wa Mkoa alikuwa ni Marco Mabawa.

  Mh Rais. kwa hiyo kwa heshima ya uongozi wa wakati ule, Rais aliona ni haki kuwawajibisha mawaziri hawo watatu pamoja na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, hivyo wote walilazimika kujiuzulu,na nchi ikawa na amani, Hivyo ndivyo waungwana wote duniani wanavyofanya.

  Mh.Rais katika awamu yako hii kumetokea mauaji mara kadha wa kadha badala ya viongozi husika kuwajibika serikali imekuwa ikikimbilia mahakamani huku waliyohusika na makosa hayo kuendelea kuwa madarakani wakati vyombo husika vikifanya kazi yake, ni hivi majuzi tu tukio la Mwandishi aliyekuwa mikononi mwa polisi na kufia mikononi mwa polisi mpaka sasa hakuna mkuu yeyote wa polisi ama waziri ama mkuu wa moa aliyewajibika katika sakata hilo, Utawala bora tunaowaimbia Watanzania ni upi? sijaona kiongozi akiwajibika kwenye maisha ama kwenye haki ya mtanzania kuishi bali nimesikia Mawaziri wakiwajibika kisiasa kupisha upepo upite huku wakilitia taifa hasara. Umma wawatanzania tungependa kujua amani hii ni ipi?

  (c)Kwa Halmashauri kuu ya CCM Kuruhusu uamuzi huu unaokiuka ''AHADI YAKE MUHIMU YA UADILIFU INAYOWAKATAZA VIONGOZI KUTUMIA VYEO VYAO KWA FAIDA ZAO"kutekelezwa bila halimashauri kuu hiyo kuikemea serikali yake, kunakiweka chama hicho katika MTIHANI MKUBWA WA IMANI,KAMA ILIVYOSASA WANANCHI HAWANA IMANI NA CCM. Mh Rais uamuzi huu unawafanya watu waaminifu,waadilifu,wasio na ubinafsi na wanaolitakia taifa lao mema kwanini wakiamini chama hiki kuwaletea utawala bora? Ni dhahiri ya kweli sasa yakuwa CCM ya kweli ilikuwepo kipindi cha Mwalimu nyerere.

  Nahitimisha.
  Mh Rais.
  jambo la kujiuliza ni kwanini tabia hii ya Rushwa imekithiri? jibu la haraka haraka ni kwamba hii imetokana na uamuzi wa Halimashauri kuu ya CCM mwaka 1991. ambao uliondoa miiko ya uongozi na kuwaruhusu Viongozi wa kujilimbikizia mali kwa kupokea mishahara zaidi ya mmoja,kufanya biashara wazi wazi bila miiko yeyote ile. Kiongozi asipotosheka na anayeweka tamaa za binafsi mbele badala ya utumishi kwa umma, anayo nafasi kubwa ya kuuza haki za wananchi na hata nchi yenyewe kwa faida zake binafsi. Hivyo ndivyo inavyotokea leo, na ndiyo maana watu wananunua uongozi.

  Mh. Rais HAtutasita kuusema ukweli kwa hofu eti ya kuwakosoa watawala na kuogopeswa kwa kifungo ama jambo lolote lile, Tutaendelea kuusema ukweli kwa usiku na mchana mpaka siku ya mwisho ya maisha yetu kwakuwa tunaamini mwenye kutenda haki ni mungu peke yake hapa duniani ni kanuni tu za kuishi....

  HAKI ITENDEKE KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KASHIFA MBALIMBALI WATOKE KWENYE MADARAKA KUPISHA SHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE, NENO AMANI LIWE AMANI KWELI KWA WATANZANIA WOTE KUTOKUWA NA HOFU NA KESHO YAO.

  Ahsante sana
  HENRY KILEWO
  KATIBU MKOA WA KINONDONI NA KANDA YA DSM
  MJUMBE MKUTANO MKUU TAIFA(CHADEMA)
  NEVER SAY NEVER M4C WE HAVE THE POWER,
  16/10/2012.
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Narudi kuimalizia
   
 3. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Kamanda kilewo, umenena mambo ya msingi sana, vijana Tuanze kuiga menendo kama hii ya kukosoa kwa hoja, Kilewo nakumbuka kauli yako ya Serena Hotel kwenye uzinduzi wa M4C ya kwamba, Dunia inateseka watu wanateseka si kwasababu ya vurugu,dhuluma au maasi bali ni kwasababu ya ukimya wa watu wema, yaani watu wema kukaa kimya na kutokukemea maovu, ujumbe huu ulimwingia kila mtu ni hakika Chadema ni chuo cha kufunda uuongozi. Tupo pamoja sasa magamba muingie mtukane weeeeee ila habari ndiyo hiyo.
   
 4. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Kaka weka hints kidogo kilitokea nini kwenye mdahalo huo make nikiona tu jina la tundu lisu najua kuna kitu muhimu kimesemwa hapo, si unajua si wa machakani hadi tusubili gazeti la kesho tutralipata keshokutwaaaaaaa
   
 5. M

  Martin Jr JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani magamba mmeusoma waraka huwo wa kamanda kwa umakini sana, tukiwaambia chadema inavijana wenye upewo wa hali ya juu mnakuja na matusi, hebu aniambie kijana waccm aliyekuwa anajua mambo matamu ya tanu, Heko Kilewo na hongereni viongozi wa cdm kwakutukuzia vijana kama hawa.
   
 6. a

  arusha 1 Senior Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kilewo na mimk Nikusalimu.

  Ukosoaji huu usiishie tu hapa hakikisha unafikisha ujumbe huu na kuupanua zaidi sehemu za vijijini maana hata kwenye hili jukwaa unaona watu wanaacha kuchangia vitu vya maana wanaenda kuchangia udaku, Naamini tukiwa na misingi imara taifa hili litaweza kunyanyuka na kila kiongozi ataweza kutambua wajibu wake katika kulitumikia taifa.
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kilewo, asante umesomeka.

  Naomba niongeze hivi; sisi wananchi tunajali, tunaipenda na tunaithamini nchi yetu. JK na CCM yake hawaipendi, haiwajali wala kithamini nchi hii. MATENDO na MWENENDO wao ndio unaosema na kutabainisha hivyo.

  Haiwezekani mtu ametumia zaidi ya trilioni 50 na rasilimali nyigine kibao ktk utawala wake mpaka sasa halafu:-

  1) Mafisadi bado wanadunda mitaani, mahakama zetu na ofisi za DPP na DCI zinachagua kesi za kufungua/kupeleleza licha ya ushahidi mkubwa uliopo dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

  2) huduma za afya na elimu zimezidi kudorora kwa kasi ya jumbo jet. Migomo ya madaktari na walimu ni viashiria chanya vya ukubwa wa matatizo sugu ktk sekt hizi muhimu,


  3) Hali ya usalama wa ndani wa nchi si nzuri. Usalama wa raia na mali zao kwa sasa ni mdogo kuliko wakati wowote tangu uhuru wa nchi hii. Jeshi la Polisi kwa sasa limetelekeza kazi na makusudio ya kikatiba ya kuwepo kwake. Mnajue wanabodi madudu ya Jeshi la Polisi kuanzia rushwa, ujambazi na sasa uuaji wa kimpangilio (serial killings).

  4) Mihimili ya Bunge na Mahakama, licha ya gharama kubwa ktk kuwekeza kwenye majengo mihimili hii miwili imebaki kuwa ni vibaraka vya Rais na CCM. Havina ufanisi wala havionekani kutekeleza majukumu yake kama vyombo huru vya kimfumo.

  Kwa hiyo kwa miaka hii saba mpaka sasa, tumebaki nyuma lakini tumelipia gharama ya huko kudumaa. Tumetumia fedha za walipa ambazo zilipaswa kulipia maendeleo yao na si vingnevyo, kulipia kudumaa, umaskini na matatizo ya kutengenezwa na watawala.
   
 8. a

  arusha 1 Senior Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jukumu lingine la mwananchi wa kitanzania> ni kuhakikishia anashiriki kikamilifu kumuwajibisha kiongozi wake, kwani sisi wananchi ndiyo mabosi wa viongozi wote wa kuchaguliwa na wasiyo wakuchaguliwa, kwa kuwa hawa wote wanaishi kwa kodi zetu, polisi wasiye na kiburi cha hali ya juu kumuelekezea mtanzania mtutu wa bunduki na kumtisha kwa kuidai haki yake, badala yake polisi wawe marafiki kwa wananchi na kuwaongoza kufikisha ujumbe sehemu husika.
   
 9. R

  Red one Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Hoja ya Kilewo inahitaji majibu ya kina, Ama ningalisema mjadala mpana sana, Wanajf tulikuwa tumekosa vitu kama hivi muda mrefu ambavyo unajua kabisa kuwa hapa mtu alikaa chini akafikiri kisha aakaandika siyo kukurupuka na kutaka kuandika ili ajaze profile yake vitu.

  Mimi ningalizadhani tujadili ni jinsi gani hojaa hii ataipata Rais kama mwenye alivyoiandika, ila tungejikita zaidi kwenye maswala ambayo na amini usalama kwasasa wanapitia waraka huu, uliandikwa kwa waledi wa hali ya juu sana kuliko tunavyodhani humu JF, Kipaji cha kuandika kinahitaji kuheshimika.

  Vile vile ninaimani Rais hata kasirika kwa waraka huu mwemba wenye ukweli mtupu kila neno la mstari ni ujumbe kwa serikali yetu. Tanzania ya sasa tunahitaji vijana kama hawa waupinzani wanaokaa na kutafakari na kuamua kutumia kalamu ya kuandika kufikisha ujumbe, Hii msg natamani kule kwetu Bukoba wangeipata, ama watu wa net waprint wanaraka huu wa usambaze ili jamii ione watu wanavyoijua ccm kuliko tunavyo dhani.

  Kiukweli nahifadhi ujumbe huu siku nikikutana na kileo akiwa kiongozi nitamkumbusha baadhi ya majukumu yake, japokuwa ni kiongozi wa chama sasa na subiri akiwa kiongozi wa umma.
   
 10. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nyumba za serikali lazima zirudi hata kama ni baada ya miaka mia, hata kwa kumwaga damu. Mliouziana ni kama mnapangisha tu
   
 11. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  sichoki kusoma waraka huu, boss wa magogoni hajaupata mpaka sasa?
   
Loading...