Soma hapa mwana Jf unisaidie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soma hapa mwana Jf unisaidie

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Laurence, Sep 14, 2011.

1. Laurence

Laurence JF-Expert Member

#1
Sep 14, 2011
Joined: Jun 11, 2011
Messages: 3,106
Likes Received: 37
Trophy Points: 145
Ndugu wana Jf habarini za leo,
Nina ndugu yangu amefungwa miaka 15 tokea tarehe 8 mwezi wa pili mwaka huu kwa kosa la kupiga roba na kupora simu katika mahakama ya Mwanzo,ikumbukwe kua hukumu ilitolewa pasipo na ushahidi wa aina yoyote kwa mtuhumiwa,baada ya hukumu nilijitahidi kwenda huko nyumbani kwa wakwe zangu watarajiwa na kupata maelezo kamili ndipo nilipowashauri tukate rufaa kwa kipindi kilekile na kweli tulifanikiwa kesi ikaanza kusikilizwa upya kabisa huku mshitaki akishindwa kuhudhuria mahakamani kwa sababu mbalimbali na hata alipoambiwa atoe ushahidi au kuleta vidhibiti ameshindwa kufanya hvyo kadhalika,sasa leo ilikua cku ya hukumu kwa ile kesi lakn jana hakimu amemuita karani wa mahakama ambae tuna ukaribu nae na kumueleza kua pamoja na hii kesi namna ilivyo yule Mshitaki amempatia laki tano taslimu ili sheria ipindishwe na Hakimu amesema anaiahisha kesi mpaka tarehe 5 Oct ili afanye maamuzi yake anayoyajua yeye na leo ilikua ndio hukumu yenyewe,swali je tufanyeje wandugu maana sheria dhahiri inapindishwa hapa kwa mwenye hela na ukizingatia hakimu anamueleza kalani kua Mshitaki ameahidi kumuongezea fungu jingine je tufanyaje wapendwa kwa hali kama hii? Toa ushauri wako mpendwa kadiri uwezavyo kwani binafsi naumia sana kwa kesi hii.

2. S

SALOS Member

#2
Sep 14, 2011
Joined: Aug 27, 2011
Messages: 26
Likes Received: 1
Trophy Points: 0

3. S

SALOS Member

#3
Sep 14, 2011
Joined: Aug 27, 2011
Messages: 26
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Pole sana! Mshtakiwa hawez kushinda kesi bila kutoa ushahid,huyo ndugu yako anatakiwa atoe ushahid au atafute mashahidi wataoweza kumtetea aonekane hana hatia,ongea na wanasheria wakuu wajue cha kufanya kwa hao wanaotaka kupindisha sheria.

4. Laurence

Laurence JF-Expert Member

#4
Sep 14, 2011
Joined: Jun 11, 2011
Messages: 3,106
Likes Received: 37
Trophy Points: 145

Asante mkuu kwa ushauri wako

5. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#5
Sep 14, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Mkuu kama mshtaki hana ushahidi na hajaleta mashahidi wake hiyo kesi imesimamia wapi na ni nini hakimu anachotegemea katika kutoa hukumu yake
Anategemea ushahidi upi wakati mshtaki hajaleta ushahidi wala mashahidi kuthibitisha shtaka
Na then Mahakama ya mwanzo haina uwezo wa kutoa hukumu ya miaka kumi na tano hiyo inatakiwa itolewe na kuthibitishwa na mahakama ya wilaya au mkoa
Na wewe itakapotokea lolote na kama kweli kuna ushahidi wa rushwa na ukitibitika bado una nafasi ya kukata rufaa mahakama ya juu zaidi na kama una ushahidi wa rushwa upeleke kunakohusika hata wa kunasa mazungumzo kati ya huyo karani na hakimu mhusika
Vile vile ongea na Wakili wa serikali akuambie na akupe mwenendo wa kesi na hali halisi ya kesi husika

6. ERIC JOSEPH

ERIC JOSEPH JF-Expert Member

#6
Sep 14, 2011
Joined: Aug 10, 2011
Messages: 570
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Hapo mi naöna tumia ujanja wako wote elimu yako we utashinda ila cha msingi wa tumia njia yoyote uijuayo cha msingi upate mazungumzo ya kina na huyo kalani uyanasa vizuri nenda kwa watu wanaojua shelia wao watajua kipi ufanye na kipi usifanye ila usije ukaenda kwa watu wa kuzuia rushwa hao ni wamoja sili itavuja na watafikilia jinsi ya kukuangamiza wewe.pole sana usife moyo ndg yang ytaisha

7. Laurence

Laurence JF-Expert Member

#7
Sep 14, 2011
Joined: Jun 11, 2011
Messages: 3,106
Likes Received: 37
Trophy Points: 145

Mkuu asante sana kwa ushauri wako,inasemekana anaweza asiimalize hii kesi ati kwamba huyu mshitaki anadai kesi isije mgeukia lakn najitahidi kuonana na watu mbalimbali nipate ushauri wa kisheria maana ni kweli mshitaki ameshindwa kuleta ushahidi, da ila thanks mkuu

8. Laurence

Laurence JF-Expert Member

#8
Sep 14, 2011
Joined: Jun 11, 2011
Messages: 3,106
Likes Received: 37
Trophy Points: 145

Thanks Eric kwa ushauri wako

Loading...