Solution ya majanga ya moto mashuleni ni hii hapa

Solution ya majanga ya moto mashuleni ni hii hapa

INTROVERT MAN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
993
Reaction score
1,351
Majanga ya moto ni hatari sana hakuna asiyejua. Mali na rasilimali nyingi ikiwemo binadamu hupotea kimasihara tu.

Ajali za moto mashuleni kama iliyotokea jana imeleta simanzi nchi nzima.

Nimekaa na kufikiria kuwa dawa ya hili tatizo ni serikali kuamuru shule zote zenye mabweni ZIFUNGE UMEME WA SOLA badala ya umeme huu wa kawaida kwani ni nadra sana kuona sola imeleta moto.

Naomba Serikali isijali haya mabweni ya shule yako Dar es Salaam eti pana umeme au hapa ni bush Namtumbo yote yatandikwe sola.

Umeme wa TANESCO ni hatari kwani wanafunzi ni wakorofi kwa mfano matumizi ya simu kwa shule za sekondari ni yamekatazwa na hivyo mabweni mengi hayana socket kwa hiyo wanaomiliki hufanya utundu wa kuchubua nyaya ili wachaji simu. Ukiangalia hili ni kweli ndio maana vyuoni ni ngumu kuona majanga ya moto.

Wizara husika nawashauri agizeni shule zote zenye mabweni Tanzania nzima mabweni tu ndiyo yawekewe Umeme wa sola
 
... kwani imethibitishwa chanzo cha hizi ajali za moto mashuleni ni umeme?
 
Hata wiring zao ziangaliwe wanatumia nyaya za aina gani, kama utakumbuka kuna kipindi nyumba zilifululiza kuungua Dar kwa matatizo ya umeme lakini sababu kubwa ilikuwa ni nyaya feki. Pili, shule zote za bweni ziwe na sehemu kama laundry ambapo kutakuwa na facility ya sockets ili kila mwanafunzi aweze kuitumia pale inapohitajika badala ya kuweka ufinyu kwenye kwenye hili na matokeo yake wanafunzi wanabuni njia zao mbadala ambazo ni hatarishi.
 
Maisha yakulazana kwenye ma Hall ifike wakagi tuachane nayo.
 
Shule zinachomwa hizo.shura ya maimam na bakwata mjitafakari something smell fishy
 
... kwani imethibitishwa chanzo cha hizi ajali za moto mashuleni ni umeme?
kwa macho yangu me nimeona chanzo kikuu ni umeme na pia me nilikuwa mwanafunzi pia na niliona hii
 
Back
Top Bottom