Solution biashara ya mitihani

tetere

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
963
430
Tunaongelea aibu na tatizo ambalo ni la muda mrefu sana, na sisi wenyewe, kaka, dada, baba, mama, wajomba zetu ni sehemu ya tatizo hili la mitihani.
Biashara ya kuuza mitihani ina pesa nyingi na za haraka. Kwa mtu yeyote mwenye fununu ya maswali yatakayotoka kwenye mitihani basi huyo ana hakika ya kujenga nyumba au walau kutimiza ndoto yake ya kuwa na pesa nyingi, kununua gari zuri.(hizi ndio ndoto za watanzania tulio wengi)

Mwizi anaeiba au anaevujisha mitihani:
1. hana shida ya wanunuzi - wanunuzi wapo wengi sana,kila mahali hawalali usingizi wakisubiria pepa itoke, na baba na mama na kaka na dada wakihangaika kujua wapi,nani anayo, na ni kiasi gani cha pesa kinahitajika.
2. ana chance kubwa ya kuto kufahamika - na hata akifahamika, hatafanywa lolote( hapa kwa kutegemea kiasi cha fedha alichokipata katika biashara yake hii.
Hivyo, so long as there is a demand there will always be a supply, especially where the commodity itself is precious one. The only way to deal with this problem is to disrupt the supply chain. But the hard battle which we need to win is the one with the DEMAND SIDE. Tunawezaje kubadili mawazo na nia ya jeshi hili la wahitaji????????
Hapa ndipo tunapotakiwa kupaangalia,
 
Back
Top Bottom