SOLOMON MAHLANGU NA LEGACY ALIYOICHA AFRIKA

Suzi Rafael

Member
Joined
Sep 5, 2026
Posts
11
Reaction score
5
By Suzi Rafael

July 10 mwaka 1956 huko Pretoria, Afrika Kusini alizaliwa Solomon Mahlangu. Baba yake alitoweka mwaka 1962 kwenda kutafuta maisha lakini hakurejea, hivyo Solomon alilelewa na mama yake aliyeitwa Martha Mahlangu.

Akiwa sekondari yalitokea mauaji ya Soweto na akakimbilia Msumbiji katika kambi ya wakimbizi Xai Xai. Akiwa hapo alichukuliwa na viongozi wa ANC na kupelekwa kwenye mafunzo ya kijeshi nchini Angola.

Baadae yeye na kaka yake George Mahlangu na Mondy Motlong walipelekwa nchini Swaziland kwenye kambi ya ANC kwa mafunzo zaidi ya kijeshi.

June 1 mwaka 1977 walivuka Swaziland kwenda Johannersburg wakiwa na silaha kwenye mabegi. Walipofika wakachukua taxi.

Siku chache kabla ya kufika Johannersburg kulitokea mauaji. Watu wenye silaha walivamia duka moja, wakaua walinzi wawili na kupora. Polisi walikua katika harakati za kuwatafuta washukiwa wa tukio hilo.

Walipoliona gari la kina Mahlangu wakalitilia mashaka. Wakasimamisha na kupekua. Kwenye mabegi wakakuta baadhi ya silaha zikiwemo AK47.

Solomon na wenzie wakafanikiwa kukimbia, wakimuacha dereva taxi na mabegi yao. Solomon na Mondy Motloung walikimbilia sehemu moja huku George Mahlangu akikimbilia kivyake.

Baadae Solomon na Mondy walikamatwa na kuhusishwa na tukio hilo la mauaji. Mahakama kuu nchini humo ikawahukumu kunyongwa hadi kufa. Mawakili wao wakaomba kukata rufaa lakini wakakataliwa. Wakapeleka maombi mahakama ya rufaa ili itengue uamuzi wa mahakama kuu wa kuwakatalia kukata rufaa, lakini bado wakakataliwa.

April 06 mwaka 1979 wakanyongwa. Wakati wakipelekwa kwenye eneo la kunyongewa, Solomon alisema "Waambieni watu wangu kuwa nawapenda, na ni lazima waendelee na mapambano. Damu yangu itanyunyizia mti utakaozaa matunda ya uhuru. Aluta continue" Baada ya kusema maneno hayo akanyongwa na kufa.

Katika umri wa miaka 22 tu aliyobahatika kuishi, Solomon aliacha historia kubwa nchini Afrika kusini na barani Afrika kwa ujumla. Nchi nyingi zimekuwa zikimuenzi kwa namna mbalimbali. Nchini Tanzania, chuo kikuu cha Sokoine (SUA) kimeipa campus ya Mazimbu jina la Solomon Mahlangu campus.

VIJANA wa Karne hii, watakumbukwa Kwa kuendeleza anasa, michezo na mambo ambayo hayana mustakabali Kwa Taifa letu.
 
Mambo yamebadilika sana kizazi hiki

Ukiwasikiliza wanajinasibu kuwa vijana ndio nguvu ya Taifa utafikiri hizo nguvu wanazo kweli

CCM imefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana "kuwaua" vijana! Haijawaua kimwili lakini imewaua kifikra na kijasiri

Ukisoma historia ya wapigania uhuru wengi wa Afrika walipigana wakiwa bado vijana wadogo kabisa na walikuwa moto wa kuotea mbali

Kina Patrice Lumumba, J.K.Nyerere, hao kina Solomon nk

Sasa angalia vijana wa siku hizi wenye miaka 22 hadi 35 halafu sikiliza fikira zao, pima uelewa wao....aibu utaona wewe

Yaani wamewaachia wazee kama kina Warioba, Prof. Shivji, Jenerali Ulimwengu, "Prof" Lisu ndio wapiganie nchi kana kwamba wao ndo wana umri mrefu wa kuishi kuliko hao vijana!!

Inashangaza
 
Ni kweli kabisa Vijana ambao walipaswa kuwa mstari wa mbele kupinga mifumo kandamizi, utekaji na utawala WA Kidhalimu, lakini wamekuwa docile bodies Yaani watu ambao wanajua Matatizo yanayoliksbili taifa letu ila wanadhani hiyo sio kazi Yao.
Ukiwafikiria Hawa
Malcolm X
Frantz Fanon
Ahmed Bella
Thomas Sankara
Ni Vijana wenye mchango mkubwa sana ktk ukombozi wa mtu mweusi na waliokuwa na umri mdogo sana
VIJANA wa Sasa ni aibu kabisa Kwa taifa
Ila yote ni Kwa sababu CCM wamejaribu uwezo wa VIJANA wa Taifa hili kuhusu Historia Yao Kwa kupitia mifumo ya Elimu , udhibiti wa vyombo vya habari na Viwanda vya starehe

Tanzania ni nchi namba 5 Kwa kubeti AFRIKA, hiyo sio Kwa sababu hakuna Cha kufanya Bali serikali Hutumia soft power kama celebrities (watu maarufu ) wanamuziki, mipira, selta za Burudani kama vile betting, Pombe n.k

Inasikitisha Serikali kwenye bajeti ya Mwaka huu imeongeza Kodi kwenye usajili wa boda boda huku Kodi kwenye imbe na betting zikiachwa

Itoshe kusema CCM haiwezi Toka Kwa njia ya maandamano, Bali Kwa kuanza kujua mbinu wanayotumia kutawala taifa hili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom