Sola ni nini?

naongea kwa uzoefu kwangu natumia mpaka friji la sola no tanesco umeme,kuna siku mvua inachesha siku 3 na hamna jua kabisa lakini kila kitu kipo safi taaa 24 zinawaka natumia tv blender etc.it depends na ukubwa wa panel zungumza na wataalam,nina root 2 za solar ipi ile inayotumia system 1 na tanesco na ipo ta independent ambayo ina system yake pekee ambayo ina panel ndogo hii hapa siku jua lisipowaka inasema low charge
 
MziziMkavu Mkuu Taa 5 za solar (dc), kuchaj simu 3 kwa siku, na radio ya 9v kwa pamoja vitahitaji package ya watt ngapi, na if possible bei yake mkuu
Mkuu Pokofame inakufaa hii hapa chini Bei itabidi uwasiliane na hawa Wauzaji wapo Dares-Salaam au Mwanza wapigie simu:



[TABLE="class: cms_table_contenttable, width: 100%"]
[TR]
[TH="align: center"]Saizi (Watts)[/TH]
[TH="align: center"]Sehemu ya mfumo[/TH]
[TH="align: center"]Mfano kwa matumizi[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]80W[/TD]
[TD]Sola panel 80W
Betri 120Ah
Kidhibiti chaji 8A
Kibadili umeme 300W
Taa 6W (*6)
Boksi kwa betri[/TD]
[TD]Taa sita
TV 21'' (saa ntatu)

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]



Ukikuwa na maswali mengine unaweza kututuma E-Mail au kutupiga simu!
Zara Solar Ltd. Mwanza
Nyerere Road
Simu: +255 28 2502910
Faksi: +255 28 2540561
Simu: +255 764 600825
zarasolar@yahoo.com
Zara Solar Ltd. Dar es Salaam
Bibi Titi / Morogoro Road
Simu: +255 22 2127450
Simu: +255 655 299500
 
Last edited by a moderator:
nashukuru mzizimkavu kwa maelezo hayo mazuri kwakweli ila mimi nina maswali mengi sana ila ya muhimu sana ndio nitauliza, mimi mwenyewe miaka minne imepita nilinunua umeme wa sola kulikuwa kuna kampuni ya kutoka ujerumani walikuwa wanauza vifaa hivyo na mafundi wao nilitumia kama 1,200,000/= nikapewa na fundi nikaenda nae mkoani kijijini kabisa kunifungia umeme nikawa natumia bulb 11 za watt7 na vile vile switch socket za ukutani za kuchanrge phone na kusikiliza radio, radio ndogo tu lakini waliniambia umeme wangu ni wa watts 90 sasa lile kumpuni liliondoka sio siri kutoka moyoni sina imani kabisa na haya mashirika mengine yanayotoa huduma hapa maana nimeshasikia malalamiko mengi sana kutoka kwa watu nilijaribu kuangalia kwenye mtandao nikakutana na shirika hilo hilo germany nikawaomba kama wanaweza kunitumia vifaa maana nataka kuongeza watts nimeangalia gharama nitatumia pesa nyingi sana kwa kweli nimeshindwa lengo langu nataka kuwa na taa 14 badala ya 11 pia nataka kuwa naangalia tv kwa masaa mengi about four to six hours sasa naweza kutumia watts ngapi kitalaam zaidi now niko kwenye 90w na gharama naweza kufanyiwa estimation tu? na kweli hawa jamaa wana vifaa vya uhakika? maana kuna shirika moja ndugu yangu alienda kununua akaambiwa yaani ikileta shida uje ila ukweli vile vifaa vilikuwa sio original alipata hasara sana alivyorudi hata kumsikiliza hawakuweza, inauma sana watz wanafany biashara y kutudanganya sana once wakipata pesa hawaangalii wateja wao wanaendeleaje, mwisho wa siku watu wengine wakija na huduma nzuri ndio sisi tunaanza kulalamika kuwa wanatuzibia, ilingali walikuwa wanatusaidia sana kupata huduma inayostahili.
 
[TABLE="width: 1013"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
Umeme wa jua unapunguza gharama za maisha

Shehe Semtawa
​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD]WAKATI nchi ikikabiliwa na tatizo sugu la upatikanaji wa nishati ya umeme Watanzania wametakiwa kubadilika na kuanza kujitokeza kwa wingi katika matumizi ya umeme wa mionzi ya jua.

Umeme huo wa mionzi ya jua ni umeme bora na hauna tofauti na umeme wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO).


Kwa kujiunga na umeme huo wanaweza kupunguza kero wanazozipata katika shuguli zao za kila siku ofisini au nyumbani.


Kampuni ya makandarasi maalumu wa nishati hiyo ya jua, (Ensol (T)LTD), ndio wasambaza wa huduma hiyo ikiwa ni pamoja na uuzaji, ufungaji wa vifaa na mitambo ya umeme huo wa jua.


Kwa kutaka kujua zaidi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hamisi Mikate, anaelezea teknolojia hiyo kwa undani zaidi hadi kumfikia mtumiaji.

Anasema teknolojia ya umeme wa jua ilianza kufanyiwa utafiti tangu miaka

1800 na utafiti huo ulianza kuzaa matunda katika miaka ya 1950.

Mikate anasema matunda ya utafiti huu yalipata nguvu miaka ya 1970 katika nchi za Ulaya na Marekani kutokana na mgogoro wa mafuta.

Anabainisha zaidi kuwa hadi sasa umeme wa jua unatumika sehemu nyingi sana duniani na Ujerumani ndiyo inayoongoza katika matumizi ya nishati hiyo.


Mikate anasema nishati ya umeme wa jua ni teknolojia ya uvunaji wa mwanga wa jua kupitia vifaa maalumu ambavyo hugeuza mwanga huo kuwa umeme.


Muunganiko wa vifaa hivi maalumu na vingine ndivyo vinavyounda mfumo kamili wa umeme huo wa jua. Mtaalamu huyo anatutajia aina ya vifaa vinavyounda mfumo kamili wa umeme wa jua.


Moduli ya sola (Solar Panel/Module)


Mikate anasema hiki ni kifaa mama katika mfumo wa umeme huo ambapo muduli hupokea mionzi ya jua na kuibadilisha kuwa umeme.

Anatoa ufafanuzi kuwa aina moja huitwa kristalini ambayo huonekana

kama kioo cha bluu , bluu-nyeusi chenye mistari iliyokatiza (draft), na aina nyingine huitwa amofasi huonekana kama kioo cheusi chenye mistari ilinyooka kuanzia juu kwenda chini.


Betri ya sola (Solar Battery)

Anabaisha kuwa betri ya sola ni muhimu kwenye mfumo wa umeme huu kwani hii hutunza umeme unaonaozalishwa na module/panel ya sola

wakati jua linawaka kwa ajili ya matumizi ya wakati ambao mwanga wa jua haupo (usiku/mawingu mazito).


Kudhibiti chaji (Solar Regulator)

Mikate anasema hii ndiyo akili ya mfumo wa umeme huu wa jua ambapo huhakikisha betri inapokea umeme unaolingana na uwezo wake tu na si zaidi.
Pia huhakikisha betri haitumiki zaidi ya chini ya kiwango kilichokadiriwa kitaalamu, hivyo kuifanya betri hiyo idumu kwa muda mrefu.
Kidhibiti chaji pia humsaidia mtumiaji kuelewa mwenendo wa mfumo wake wa umeme huo wa jua.

Kigeuza mkondo (Inverter)


Mkurugenzi huyo anazidi kufafanua kuwa umeme unaozalishwa na sola ni sawa na ule wa betri yaani volti 12, hivyo huwezi kutumia moja kwa moja vifaa vinavotumia umeme wa TANESCO, yaani wa volti 240.

Inveta hubadilisha umeme wa betri wa volti 12 kuwa sawa na ule wa

TANESCO wa volti 240 ili uweze kutumia vifaa vyako vinavyohitajika kama wa TANESCO ili viweze kuwaka.


Kishika moduli ya sola (Solar Mounting Structure)


Mikate anasema hii ni fremu ya kufungia moduli ya sola, hutengenezwa katika vipimo maalumu ili moduli ya sola ikifungwa iweze kumulikwa na

mwanga wa jua kuanzia asubuhi hadi jioni na katika majira yote ya mwaka.


Pamoja na vifaa hivyo, Mikate anasema vifaa hivyo vilivyoorodheshwa, mfumo wa sola hukamilishwa na vifaa vingine vya ziada kama waya, swichi na soketi.


Matumizi ya umeme wa jua


Mikate anasema umeme huu hutumika kuwasha vifaa mbalimbli vinavyotumia umeme wa betri au ule wa TANESCO ambapo umeme huu

pia hutumika kuwasha taa, redio, runinga, vifaa vya mawasiliano, chaji ya simu na vinginevyo.


Pia umeme huu hutumika mahala popote pale kama vile majumbani, zahanati, vituo vya afya, shuleni ofisini na mashambani.

Umeme huu ni rafiki wa mazingira, kwani hautoi moshi, hauna kelele,

hautumii mafuta yoyote na wala hauna matengenezo ya mara kwa mara kama ilivyo kwa jenereta, pia hakuna malipo ya kila mwezi kama ule wa TANESCO.


Aidha, Ensol inakufanyia ukadiriaji wa kiwango cha umeme kinachohitajika kwa matumizi ya vifaa vyako na kukupa makadirio ya gharama zake mara unapotoa maelezo ya mahitaji yako.


Mikate anasema kampuni itakufungia mfumo wako kwa kuzingatia kanuni za kitaalamu na miiko yake huku wakikuwekea kipaumbele cha usalama kwa watumiaji na vifaa vyao.


Kwa wateja wanaotoka nje ya Dar es Salaam, hawana haja ya kusumbuka hadi katikati ya jiji kwenye msongamano mkubwa wa watu na magari kutafuta huduma ya nishati hiyo.

Wapo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi ya mikoani na nje ya nchi

Ubungo (UBT), mahali ambapo itakuwa rahisi kwako kusafirisha vifaa vyako kwenda sehemu yoyote mikoani.


Mikate anasema Ensol (T) LTD ni kampuni ya uuzaji wa vifaa vya umeme wa jua (vifaa vya solar power), iliyoanzishwa na kuanza shughuli zake mwaka 2001.

Pia imesajiliwa na Bodi ya Makandarasi Tanzania (CRB), tangu mwaka 2002 kama makandarasi maalumu wa uungaji wa vifaa na mifumo ya umeme wa jua.

Anasema kampuni hadi sasa imefunga mifumo ya umeme huo wa jua wenye uwezo tofauti tofauti kwa watu, taasisi mbalimbali kama vyuo vya ualimu, mbuga za wanyama (Selous, Serengeti, Arusha, Muyovosi, Sadani na miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na mashirika ya kimataifa kama UNDP, UNICEF, DANIDA na Clinton Foundation.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

Brother long time no see, happy to see you here. Back to topic, i beg to differ and agree with Nivea. Panel haihitaji direct sunlight so as to work, remember kua light scatters so hata panel ikiwa kwene kivili be sure, enough radiation are falling on it maana it doesn't depend on Heat energy which u have plenty on direct sunlight but the UV spectrum of it, in fact nakumbuka watengenezaji wa solar wanasema if there is enough light for u to see its good enough. Ila if the place is cloudy all day long yeah power will be low but not out completely
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…