Nadhani mpaka akuibie mkeo ndio utajua jamaa ni mwizi...vinginevyo tukikuambia ni mwizi utakataa tu. Ubovu wa Lowasaa ni uroho wa mali, anakwapumua mali za umma kila kukicha. Hata scandal ya Richmond nawe hukusikia? Kampuni ya kuuza stationaries kupewa tender ya kufua umeme kwa ajili ya grid ya taifa, wewe unaona alifanya tu hivi hivi. Kwa taarifa yako, wataalamu waliojitahidi kushauri walitishiwa uhai...galamaho! Nyerere asingeweza kumsingizia ile 1995, kwamba haka ni kachafu tayari.
Akawe rais nyumbani kwenu aroo.!
Mkuu Chiwa nimeipenda hii'kuhis ni kosa kuhisiwa ni kosa zaidi'.tuko million 40 hivi lazima tumpe lowasa urais? mimi nakereka sana na watu wanaobeba upuuzi .huyu afanye asifanye aachane na siasa muda wake ushapita head master wangu mmoja alikuwa anasema kuhisi ni kosa lakini kuhisiwa ni kosa zaidi sasa mnataka ushahidi gani? ikiwa polisi mwenyewe halali mlango wazi wakati kazi yake ni kulinda raia na mali zao tena kwenye mto analala na bastola! sasa hapa hakieleweki nini? angalia tusipitie kwenye screen kwa hasira! kwa kifupi tunafikilia ni jinsi gani tuachane na ubinafsi lakini tunashindwa lakini kwa imani yangu kamwe hatakuwa rais na nadhani binafsi analijua hilo anachofanya ni kutengeneza mtandao mwingine kwa jinsi ingine ila si dhani kama antegemea hivyo japo ana utaka
Kama ni kweli Sokoine alim-groom Lowasa, basi tumpe 2015 japo atukomboe hii miaka michache aliyobakiza,
Kama kuna mtu anajua ni mwizi aseme kaiba nini, mana kama kujiuzuru hata Mwinyi aliwahi jiuzuru hafu akaja kuwa Rais wa Zanzibar, na URT - kwa hiyo kujiuzuru ni swaga!