Miaka mitano-saba kurudi nyuma Nissan Xtrail ilikuwa ni gari ambayo watz wengi hawakuikubali sana ikilinganishwa na gari kama Toyota rav4, na ijapokuwa Toyota rav4 ni gharama kwa maana ya bei ukilinganisha na Nissan xtrail bado watz wengi waliipenda sana rav4 hapa naongelea SUV cars. Kwa miezi kadhaa na pengine mwaka 1 uliopita hatimaye Nissan xtrail zinanunuliwa kwa wingi, kwa Dar nimeona nyingi zenye namba za hivi karibuni. Sababu za watu wengi kwa sasa kununua Nissan xtrail ni urahisi wa bei ukilinganisha na gari zingine ambazo ni SUV. Kwa mfano ukiwa na ml 12-14 unapata Nissan extrail za miaka ya 2007 kurudi nyumba. Ilihali gari kama rav4 ile ya engine ya 3s aka roho ya paka ina gharama kuzidi xtrail. Kingine ni kuwa kwa sasa angalau mafundi wanapatikana ambao sasa wanaweza kuziservice hizi gari.
Kiukweli xtrail kwa sasa ni budget suv car! Ingawa pindi mtu anaponunulia yamfaa afanye utafiti wa kutosha ili asijefanya makosa ambayo atayajutia baade! Kwa mfano kwa perception za watz wengi Nissan xtrail zina resale value ndogo!
Je mwanajamiiforums nini maoni yako kuhusu hiki nilichoandika?