Fuel consumption ya Nissan x trail 2007/2008 ikoje?

Mb-one

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
882
1,282
Wakuu habari,

Poleni na janga la corona. Nilikuwa nauliza kuhusu matumizi ya mafuta ya hi gari Nissan xtrail 2007 au 2008 ikoje kiuhalisia kwa wale waliotumia hii gari au wanijua vizuri.

Kutokana na specification Yake ni 1990CC

Nitashukuru

images (2).jpeg
\
Ukweli ni huu.

-Nissan X-trail ni miongoni mwa magari yenye reputation mbaya zaidi kutoka kwa wamiliki wake hapa Tanzania (Kwanini? Mategemeo waliokuwanayo kabla ya kumiliki hiyo gari yamekuwa tofauti na uhalisia wake baada ya kumiliki).

-Gharama za kuimiliki hiyo gari ziko chini, lakini gharama za kuendelea kulimiliki hilo gari (service&fuel) ziko juu ukilinganisha na gari zingine zenye bei za level hiyo hiyo wakati wa kununua.

-Watu wengi waliozinunua hizo gari baada ya muda mfupi sana walitamani kuziuza, na waliofanikiwa kuziuza basi waliziuza kwa shida au kuziuza kwa bei ya chini sana.

Kwa kifupi sana ninaweza kuhitimisha kwa kusema haya kuhusu Nissan X-trail. Ni gari nzuri kimuonekano, zina nafasi kubwa ya kutosha ndani, ziko comfortable ukikaa ndani, ziko stable barabarani, ziko juu (hivyo kuna nafasi ya kutosha uvunguni, na kuruhusu kupita barabara zote bila kugonga chini kirahisi), affordable price kulinunua, lakini ziko kiasi delicate, matumizi ya wastani ya mafuta (it is not a fuel economy car!) spear zake ziko juu kiasi na zinahitaji service kubwa mara kwa mara.
 
Kuna mwamba majuzi juzi alikuwa anahitaji nimtafutie Rav 4 old model toka show room ila tulishindwana bei. Akaja kunitumia pics za Nissan xtrail anataka aishi humo. Nikampa wazo ukiwa uko fresh financially chukua ila kama hautakuwa poa iweke hela uje kuvuta rav 4 uliyoitaka.

Jana naona ananitumia picha za gari Xtrail ipo kwake Mimi navunga sasa ila pale ndiyo kipimo cha kuja kujua kuwa mwamba ana deep pocket ama laah.

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom